Huwa napatwa na ukakasi kusikia kwamba Ikulu ni mahali patakatifu. Utakatatifu ni zaidi ya heshima. Utakatifu unahusiana na Imani ambapo lazima yawepo mawasiliano ya ki- Imani kupitia maombi kati ya mwombaji na Mwenyezi Mungu.
Mahali patakatifu ni sehemu ambayo kupitia maombi miujiza inaweza kujidhihirisha au kupata majibu ya maombi. Ukichukulia Ikulu zetu hizi na hasa za Kia-Afrika ambapo viongozi tunaowapa dhamana au wanaojipa dhamana ya kuongoza watu wao huwa wamezungukwa makandokando aidha kabla hawajaingia na baada ya kutoka, ni dhihaka kubwa kusema Ikulu ni mahali patakatifu.