Ikulu mpya na maswali

Ukubwa wa eneo wala sioni kama ni tatizo, mkuu. Kosa lao ni kulifanya kipaumbele kana kwamba bila hiyo ikulu Mtanzania wa kawaida atashindwa kula na kulala.

Viongozi wa Afrika wako busy kujipalia sifa uchwara, wakati raia wao ni hohe hahe. Hawa wala-nchi ni shida kweli kweli.
Mbona hukupinga Ujenzi wake
Leo hii kinawekwa Bustani na Njia Yakuruka Ndege Unapiga kelele.
Acheni Nongwa.Tafuta Pesa
 
Pia sikuona sababu ya Ikulu kuwa na eneo kubwa vile, operations costs ni kubwa sana

Yaani umeona kama mimi,majengo yote yale for what?si yangejengwa hata matatu tu?Kuna maeneo ya Tanzania hakuna maji safi na salama,hospitali wala shule.
 
Je, kuna ulazima wa yafuatayo au ni kupoteza pesa za walipa kodi?
  1. Kujenga Njia ya Kuruka Ndege Ikulu.
  2. Ujenzi wa Viwanja vya Golf.
  3. Ujenzi wa Complex ya watu 2000-3000
NB: Kama wanatimiliza Ndoto ya Nyerere kwanini Complex isiitwe Nyerere Complex au iitwe aliyeanzisha Ujenzi Magufuli Complex. Kwanini iitwe Samia Complex?

Je, Watanzania tuna kodi kiasi hicho kujenga Ikulu ya namna hiyo? Kuna ulazima gani?

Je, nani mnufaika wa hayo yote?

Kwanini hizo pesa zisiende kwenye elimu ya awali na msingi maana huko ndo chanzo cha madudu ya huku juu?
Kulikuwa hakuna haja ya kuhamishia makao makuu ya serikali kwenda Dodoma.

Hii ilikuwa project ya anasa za kisiasa tu.

Tumetatua tatizo ambalo halikuwapo, wakati matatizo yetu mengi yaliyokuwapo mpaka leo hatujayatatua.
 
NB: Kama wanatimiliza Ndoto ya Nyerere kwanini Complex isiitwe Nyerere Complex au iitwe aliyeanzisha Ujenzi Magufuli Complex. Kwanini iitwe Samia Complex?
Kati ya aliyeiota, aliyeisimulia na aliyeifanyia kazi ikatimia, ni nani wa thamani kwako?
 
Ukimkuta masikini ananua gari la kutembelea halafu baadaye kidogo anakopa pesa ya kulipia watoto wake shule na kuwapelekea hospitali utamfikiriaje??
Ujue hana watoto kwa hiyo shule sio kipaumbele chake, hivi wewe unadhani shule ndio kapaumbele kwa kila mtu. Sasa kama hiyo gari ndio chanzo cha kuleta mapato. Halafu haya mambo ya kujiita maskini mtakuwa maskini kweli nchi sio masikini wala haitakuwa masikini kama hoja yako tunakopa hivi unajuwa USA nchi tajiri duniani na imekopa zaidi ya 100% ya GDP na hivi sasa wanazozana huko kutoongeza kiwango cha juu cha kukopa ikifika June wasipokubaliana basi itabidi wa default mikopo yao na kuwavunjia heshima watashindwa kulipa hata mishahara ni kama mtu ku fail kulipa mkopo wake bank, na hii ni USA huko ndio nataka kuondoa huu ujinga wa kujiita sisi masikini sisi sio masikini na muache tabia ya kuita watoto zenu majuto na watajuta kweli..🤣
 
Wewe na ndugu zako walio masikini mngependa vipaumbele vyenu katika nchi viwe vipi?
Unataka kujuwa vipaumbele vyangu? nchi ina wizara na hizi wizara ndio vipaumbele vya nchi ndio maana wako bungeni wanagawa cake kwa hizi wizara na wote wanapata na kila kitu unachoona kinafanyika kimetengewa pesa sasa maoni yangu binafsi sio muhimu hapa. Kitu nataka mfute kila pesa ikitengewa sehemu nyingine mnaruka hii sijui ingejenga madarasa mangapi kwani kipaumbele madarasa au mfumo wa elimu yetu?
 
Mimi nimejiuliza mbona majengo ni mengi hivi? Kuna taasisi nyingi kiasi gani ikulu. Je ystakuwa yanatumika au yatakuwa tembo mweupe. Mimi nauliza sijui vizuri establishment ya Ikulu
 
Sasa hiyo complex ya watu 2000 ikulu ya kazi gani🤔🤔 yani wana jifaharisha kwa ugumu huu tulio kua nao, na utakuta hiyo fedha ni yamkopo inapelekwa kuchezewa huko, lakini ingekua ni kwenye mambo ya maana kama afya na Elimu wanasema hakuna fedha, hii awamu itavunja rekodi ya upigaji
 
Je, kuna ulazima wa yafuatayo au ni kupoteza pesa za walipa kodi?
  1. Kujenga Njia ya Kuruka Ndege Ikulu.
  2. Ujenzi wa Viwanja vya Golf.
  3. Ujenzi wa Complex ya watu 2000-3000
NB: Kama wanatimiliza Ndoto ya Nyerere kwanini Complex isiitwe Nyerere Complex au iitwe aliyeanzisha Ujenzi Magufuli Complex. Kwanini iitwe Samia Complex?

Je, Watanzania tuna kodi kiasi hicho kujenga Ikulu ya namna hiyo? Kuna ulazima gani?

Je, nani mnufaika wa hayo yote?

Kwanini hizo pesa zisiende kwenye elimu ya awali na msingi maana huko ndo chanzo cha madudu ya huku juu?
Acha wivu, hilo eneo kubwa unataka wafuge tu fisi
 
Tatizo Afrika sio pesa, pesa ipo ila vipaumnele. Hapo wakikwambia zinahitajika pesa kwa ajili ya mashine za kusaifisha damu kwa wagonjwa wa figo ziwekwe kila hospitali ili gharama zishuke waweze kuafford watakujibu budget haitoshi.
Complex ya watu 2000 ikulu ya kazi gani?
Watakapokuwa wanatembelea Ikulu Makatibu kata wote Tanzania unataka wakae wapi?
 
Usiposema samia complex utahalishaje upigaji wa fedha? Yaani hapo upigaji umehalishwa. Ni mwendo wa kula tu.

Huyu mama kwakweli anawaangusha sana wanawake wenzie kiuongozi.
Wewe ulitaka iitwe nani Complex?
 
Back
Top Bottom