Ikulu ilivunja Tume ya Katiba kimya kimya bila wajumbe kujua

Kageuka

JF-Expert Member
Jun 22, 2012
241
59
RAIS Jakaya Kikwete ameivunja rasmi Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika hatua ambayo imewashutukiza wajumbe wa Tume hiyo, imefahamika.

Taarifa ya kuvunjwa kwa Tume hiyo, maarufu sasa kama Tume ya Warioba, iliyokuwa chini ya uenyekiti wa Jaji Joseph Warioba, ilisambazwa jana Jumatano na Ikulu ikieleza kwamba Rais aliivunja Jumatano iliyopita, Machi 19, siku moja tu baada Warioba kuwasilisha kwenye Bunge la Maalumu la Katiba, Rasimu ya Katiba, katika hotuba iliyoeleza kwa uwazi, pamoja na mambo mengine, matatizo ya Muungano yatokanayo na muundo wake.

Katika taarifa yenye kichwa cha habari: Tangazo la Serikali kuhusu kuvunjwa kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu ilisema:

"Mhe. Rais aliunda Tume ya Mabadiliko ya Katika kwa mujibu wa kifungu cha 5 na 6 cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83 kwa Tangazo la Serikali Na.110 la Mwaka 2012.

Tume ilikusanya maoni na kuandaa Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo imewasilishwa kwenye Bunge Maalumu.

Kwa mujibu wa kifungu cha 31 cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 3, Rais amepewa mamlaka ya kuvunja Tume ya Mabadiliko ya Katiba baada ya Rasimu ya Katiba kuwasilishwa bungeni.

Mnamo tarehe 18 Machi, 2014 Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Sinde Warioba aliwasilisha Rasimu ya Katiba kwenye Bunge Maalumu. Kutokana na hatua hiyo, na kwa mujibu wa kifungu cha 31 cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Rais wa Jamhuri ya Muungano alivunja rasmi Tume ya Mabadiliko ya Katiba tarehe 19 Machi,2014 kwa Tangazo la Serikali Na. 81 la tarehe 21 Machi, 2014.

Hivyo kwa Tangazo hilo, shughuli zote za Tume ya Mabadiliko ya Katiba zimemalizika rasmi tarehe 19 Machi, 2014".

Jumanne wiki hii, Jaji Warioba aliliambia Raia Mwema kwamba hawakuwa wamepata taarifa rasmi za kuvunjwa kwa Tume hiyo mapema, na ilibidi wafuatilie wenyewe Ikulu baada ya kuona katika mitandao na baadhi ya waandishi wa habari kuwapigia simu.

Alisema Jaji Warioba: "Mpaka sasa (saa 7:30 mchana-Jumanne) tulikuwa hatujui. Tumeuliza baada ya kusikia. Wametuletea taarifa nadhani ni kama mliyonayo ninyi na barua ya Ikulu kutueleza hilo.

"Tuna wajibu sasa kukabidhi. Maana hapa tuna mali nyingi ya Taifa. Kuna ofisi, lakini pia kuna wafanyakazi na magari. Wajumbe wote wana magari, na wale ambao hapa si majumbani kwao, walikuwa wamepangishwa. Naona kama muda wa kufanya yote hayo ni mfupi mno."

Mmoja wa wajumbe wa Tume hiyo, Profesa Mwesiga Baregu aliliambia Raia Mwema: "Mimi ndiyo kwanza unaniambia wewe kwamba Tume imevunjwa. Ndiyo, nilijua itavunjwa kwa mujibu wa sheria, lakini uamuzi umefanyika lini sikuwa na taarifa."

Taarifa zaidi kuhusiana na Tume hiyo zilieleza kwamba wajumbe wengi hawakuwa wameridhishwa na kilichoonekana kuwa ni majibu ya Rais Kikwete kwa maoni yaliyowasilishwa na Jaji Warioba katika kuwasilisha Rasimu ya Katiba.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, maoni ya baadhi ya wanaTume yalikuwa ni kwamba watafute wasaa wa kuweza kujibu baadhi ya hoja alizoibua Rais Kikwete ili zieleweke vyema.

"Sheria ya Mabadiliko ya Katiba haimpi Rais nafasi ya kufanya kile alichofanya. Kwamba amekwenda kuhutubia Bunge baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba kufanya uwasilishaji. Kitendo hicho hakikidhi matakwa ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba hata kidogo. Kwa hiyo, wamefanya uchakachuaji tu ili kuvuruga matakwa ya kisheria na shughuli za Bunge," alisema Baregu katika mahojiano na Raia Mwema na kuongeza:

"Alichofanya Rais Kikwete ni kama amefanya kuvamia Bunge...ni uvamizi hivi na taratibu zilipangwa kinyemela ili azungumze baada ya Warioba. Huu mchakato wa Katiba umekuwa na matatizo tangu kwenye mabaraza ya wilaya, kulikuwa na njama za kuuvuruga," alisema Baregu na kuonya kwamba yanaweza yakatokea ya nchi jirani ya Kenya ambapo rasimu ya Katiba ilichakachuliwa na ilipopelekwa kwa wananchi kwa ajili ya kupigiwa kura ya maoni ilikatatiliwa.

Mjumbe mwingine wa Tume akizungamza kwa sharti la kutokutajwa gazetini alisema: "Baada ya hotuba ile ya Rais, yalizuka mawazo katika kikao cha kuhitimisha. Ilizungumzwa kwamba palihitajika ufafanuzi katika maeneo fulani fulani.

"Maana sasa imekuwa kwamba viongozi wengi wanawasema sana wajumbe wa Tume, lakini wao hawawezi kujibu. Wajumbe wa Tume wameambiwa wasijibu, wasiseme. Hatujui kwa nini wao wasemwe halafu waambiwe wasiseme.Halafu hata ukiangalia siku ya kuvunjwa kwa Tume ni siku ambayo wajumbe walikuwa safarini kutoka Dodoma baada ya Mwenyekiti kuwasilisha, mambo haya hayajakaa sawa."

Upepo mbaya kuhusu Tume ya Warioba ulianza bungeni Dodoma wakati alipotaka kuwasilisha kwa mara ya kwanza Rasimu ya Katiba Machi 17, mwaka huu.

Katika tukio hilo, Jaji Warioba alijikuta akisimama kwa dakika tatu mbele ya kipaza sauti, lakini akashindwa kuwasilisha Rasimu ya Katiba kutokana na vurugu zilizojitokeza bungeni.

Vurugu hizo zilitokea muda mfupi baada ya Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta kumwalika kuwasilisha Rasimu ya Katiba kwa ndani ya muda wa dakika 120.

Hata hivyo, kabla ya Jaji Warioba kuanza kusoma hotuba yake ya kuwasilisha Rasimu hiyo, baadhi ya wajumbe walisimama na kuomba mwongozo wa Mwenyekiti.

Profesa Ibrahimu Lipumba, James Mbatia, Freeman Mbowe na Tundu Lissu walikuwa miongoni mwa wajumbe waliosimama kuomba mwongozo kabla ya Jaji Warioba kuwasilisha Rasimu yake bungeni.

Mwenyekiti Sitta aliwakatilia wajumbe hao kuomba mwongozo kwa kuwambia: "Hakuna mwongozo hapa, naomba Mwenyekiti uendelee…waheshimiwa wabunge, hakuna mwongozo naomba Mwenyekiti uendelee kwa ajili ya hansard."

Kauli hiyo ya Sitta ilizidi kuchafua hali ya hewa bungeni humo na hivyo Jaji Warioba kulazimika kusitisha uwasilishaji wa Rasimu, tukio ambalo hata hivyo alilitekeleza kesho yake asubuhi baada Bunge kuahilishwa ya siku hiyo.

Chanzo: Raia Mwema

Mwandishi Wetu Toleo la 345 2 Apr 2014

345_warioba.jpg

ALIYEKUWA Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, amesema kwamba matukio ya kuelekea kuvunjwa kwa Tume yake yanaashiria kuwa walifukuzwa.

Ameliambia Raia Mwema katika mahojiano maalumu wiki hii, yaliyochapishwa katika kurasa za katikati za toleo hili, kwamba japo wajumbe hawana kinyongo na jinsi walivyoondoka baada kufanya kazi ambayo kwao ni kubwa kwa Taifa, walitarajia kuondoka kwao kufananefanane na jinsi ilivyokuwa walipoitwa kuanza kazi.

" Tulielewa ya kwamba kuvunjwa kwa Tume kutafanywa kisheria kwa kutoa notisi. Tulijua hiyo ni muhimu kwa sababu notisi ingetoa muda ili tuweze kukamilisha shughuli za Tume.

" Hizo ni kama kurudisha mali za Serikali na kuandaa utaratibu wa kuwarudisha wajumbe walikotoka," anasema Jaji Warioba.

Aliongeza Jaji Warioba: "Baada ya mkutano huo wa Machi 24 nikaletewa swali linalouliza kwamba kwa nini bado mko hapo na Tume imevunjwa?

"Nikashangaa. Lakini nikawaambia Sekretarieti wafuatilie serikalini kujua kama kweli Tume imeshavunjwa. Kesho yake Machi 25 nikaambiwa kwambaTume ilivunjwa Machi 19 na tangazo kwenye Gazeti la Serikali lilitoka Machi 21.

"Nikazungumza na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali (George Masaju) nikijua kwamba taratibu za kutoa matangazo kwenye Gazeti la Serikali huwa zinafanywa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

" Akaniambia kwamba ni kweli Tume imevunjwa, lakini shughuli zote hizo zilifanywa Dodoma, na yeye alikuwa hajapata notisi ya kisheria. Nikamwambia lakini ingekuwa vizuri kutupa taarifa kwa sababu na sisi hatuwezi kushughulikia mambo kwa taarifa za kusikia tu."

Alisema baada ya kupata taarifa hizo waliitisha mkutano na wajumbe Jumatano Machi 26 lakini kabla hawajakutana Wizara ya Katiba na Sheria ilileta taarifa ya kuwataka wakabidhi jengo mara moja.

"Nilipoona hiyo "mara moja" nikamuomba Katibu wa Tume amuulize Katibu Mkuu wa Wizara hiyo "mara moja" maana yake ni nini? Kwa sababu haikutupa muda kamili.

"Jibu lililokuja ni ya kwamba shughuli zote kufika Ijumaa ziwe zimekamilika, na tuwe tumeondoka.

"Ijumaa saa nne nilipofika nikaambiwa kuna maagizo kwamba gari yangu ifike Ikulu saa sita. Ilikuwa tumekubaliana ningeirudisha Jumamosi. Kwa hiyo, nikaondoa vitu vyangu kwenye gari, ikapelekwa Ikulu.

"Kisha tukaendelea na shughuli, na haikuwezekana kukabidhi siku hiyo ya Ijumaa kwa sababu Wizara ya Katiba na Sheria walitaka wapate muda kwa kuhakiki mali. Waliona kwa siku hiyo wasingeweza kufanya hivyo, wakaomba wafanye hivyo Jumamosi, na makabidhiano yawe Jumatatu, Machi 31, 2014."

- See more at: Raia Mwema - Warioba: Ikulu imetutupia virago-
 
Wabunge wa CCM wameendelea kuirarua Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa bungeni na Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba.

Wabunge hao ni Diana Chilolo na Dk Haji Mponda ambao kwa nyakati tofauti walisema mjadala usingefika hapa kama sio mawazo binafsi ya Warioba.

Chilolo alimtuhumu Warioba kuwa aliingiza mawazo yake na kuacha walichochangia wananchi.huu ni utomvu wa nidhamu tume ilikuwa na watu wengi warioba alikuwa m/kiti tu sasa nashangaa vijana wadogo wanamkashifu jaji warioba kama huyu Chilolo huu ni upuuzii!!
 
Jaji na waziri mkuu mstaafu Joseph Sinde Warioba uungwana, uadilifu na ujasiri wako wa kuisimamia kweli ndiyo chanzo cha dhihaka, kejeli na matusi toka kwa wale waliokupa kazi nyeti na ngumu ya kuwa mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Umeifanya kazi hii ngumu kwa umakini na uadilifu mkubwa huku ukiamini kuwa kile unachokifanya ndiyo kile wanachokitaka waliokuteua.
Ulisahau jambo moja kubwa kiongozi wangu mpendwa ndg Warioba, nalo ni unafiki na usanii vilivyojaa mioyoni mwa watz. Wanaposema tafuta jembe inabidi uulize mara mbili mbili maana wao humaanisha kisu, koleo, kijiko ama uma. Wanaposema tunalia, uliza mnalia kilio cha namna gani? Cha furaha ama karaha? Hii yote ni kitokana na unafiki uliopevuka mno hapa Tz.
Umeteuliwa ukapangiwa muda wa kukusanya maoni. Ukazunguka nchi nzima bara na visiwani na ukamalizia kwa kuwahoji viongozi wote waliostaafu na waliopo madarakani, kisha ukaandika rasimu ya kwanza. Mabaraza yakaundwa nchi nzima yakaijadili rasimu ya kwanza na kutoa maoni yao, kisha ukaandika rasimu ya pili.
Siku ya kukabidhi rasimu ya pili sote tulishuhudia pongezi lukuki zikitolewa na aliyekuteua na vigelegele vingi. Hadi siku unakabidhi tatizo la kilichomo ndani ya rasimu hakikuonekakana kama ni tatizo lako wala takwimu hazikutiliwa shaka. Hadi siku ya uzinduzi ndiyo kasoro zinatolewa. Eti umekusanya maoni ya wachache, hawakuona haya ktk hatua zote hizo?
Kwann aliyekuteua na kukupangia muda asilione hili mapema? Kwann asikwambie kasoro hizi kabla hujafika bungeni kuwasilisha rasimu? Kwann ulaumiwe wewe huku wakijua fika kuwa si maoni yako bali ni ya watz?
Ndiyo maana nafikia hatua ya kusema uadilifu ulionao umepelekea haya yote. Yawezekana walikutaka upindishe maoni ya watz ukagoma kutokana na uadilifu wako. Hasira ya waliokuteua inajenga mazingira ya mm kuamini hilo.
Hiv sasa wamemnunua nguli wa uchambuzi wa masuala ya sheria na mhadhiri wa siku nyingi ktk chuo kikuu cha DSM ndg yangu Shivji. Amefika mahali anakana na kuyapakisogo machapisho yake mwenyewe yaliyopelekea hata Zanzibar kubadili katiba yake 2010. Machapisho yake yalionyesha na kubainisha wazi kuwa yeye ni muumini wa serikali tatu. Hivi sasa kwa kukosa uadilifu anakana.
Historia itakukumbuka Warioba, acha wakupore heshima yako hawa watawala wa sasa. Lkn jina lako litaandikwa kwenye vigae vya vyungu endapo ikulu itagoma kufanya hivo.
 
Mwandishi Wetu Toleo la 345 2 Apr 2014

345_warioba.jpg

ALIYEKUWA Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, amesema kwamba matukio ya kuelekea kuvunjwa kwa Tume yake yanaashiria kuwa walifukuzwa.

Ameliambia Raia Mwema katika mahojiano maalumu wiki hii, yaliyochapishwa katika kurasa za katikati za toleo hili, kwamba japo wajumbe hawana kinyongo na jinsi walivyoondoka baada kufanya kazi ambayo kwao ni kubwa kwa Taifa, walitarajia kuondoka kwao kufananefanane na jinsi ilivyokuwa walipoitwa kuanza kazi.

" Tulielewa ya kwamba kuvunjwa kwa Tume kutafanywa kisheria kwa kutoa notisi. Tulijua hiyo ni muhimu kwa sababu notisi ingetoa muda ili tuweze kukamilisha shughuli za Tume.

" Hizo ni kama kurudisha mali za Serikali na kuandaa utaratibu wa kuwarudisha wajumbe walikotoka," anasema Jaji Warioba.

Aliongeza Jaji Warioba: "Baada ya mkutano huo wa Machi 24 nikaletewa swali linalouliza kwamba kwa nini bado mko hapo na Tume imevunjwa?

"Nikashangaa. Lakini nikawaambia Sekretarieti wafuatilie serikalini kujua kama kweli Tume imeshavunjwa. Kesho yake Machi 25 nikaambiwa kwambaTume ilivunjwa Machi 19 na tangazo kwenye Gazeti la Serikali lilitoka Machi 21.

"Nikazungumza na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali (George Masaju) nikijua kwamba taratibu za kutoa matangazo kwenye Gazeti la Serikali huwa zinafanywa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

" Akaniambia kwamba ni kweli Tume imevunjwa, lakini shughuli zote hizo zilifanywa Dodoma, na yeye alikuwa hajapata notisi ya kisheria. Nikamwambia lakini ingekuwa vizuri kutupa taarifa kwa sababu na sisi hatuwezi kushughulikia mambo kwa taarifa za kusikia tu."

Alisema baada ya kupata taarifa hizo waliitisha mkutano na wajumbe Jumatano Machi 26 lakini kabla hawajakutana Wizara ya Katiba na Sheria ilileta taarifa ya kuwataka wakabidhi jengo mara moja.

"Nilipoona hiyo "mara moja" nikamuomba Katibu wa Tume amuulize Katibu Mkuu wa Wizara hiyo "mara moja" maana yake ni nini? Kwa sababu haikutupa muda kamili.

"Jibu lililokuja ni ya kwamba shughuli zote kufika Ijumaa ziwe zimekamilika, na tuwe tumeondoka.

"Ijumaa saa nne nilipofika nikaambiwa kuna maagizo kwamba gari yangu ifike Ikulu saa sita. Ilikuwa tumekubaliana ningeirudisha Jumamosi. Kwa hiyo, nikaondoa vitu vyangu kwenye gari, ikapelekwa Ikulu.

"Kisha tukaendelea na shughuli, na haikuwezekana kukabidhi siku hiyo ya Ijumaa kwa sababu Wizara ya Katiba na Sheria walitaka wapate muda kwa kuhakiki mali. Waliona kwa siku hiyo wasingeweza kufanya hivyo, wakaomba wafanye hivyo Jumamosi, na makabidhiano yawe Jumatatu, Machi 31, 2014."

- See more at: Raia Mwema - Warioba: Ikulu imetutupia virago-
 
Labda ni kwa sababu hawakuwasilisha Rasimu aliyoitaka Bwana Mkubwa...
 
Yote yana mwisho wake, pole sana mzee wetu. Kazi umeifanya tena ni kazi nzuri sana hata kama ccm wataikataa sisi wananchi wote tunaithamini sana.
 
Mara zote binafsi nimeamini kwamba ktk nchi yoyote ile, kuna sekta ambazo ni muhimu na ni lazima nchi itambue hilo na ajira ktk ofisi hizo iwe ni kwa watu ambao ni wazuri kichwani. Central bank, Ikulu, planning unit. Hizi siyo sehemu za kumwaga wachovu kichwani.

angalia nchi hii TZ, angalia walioko ikulu, angalia walioko BOT, ni tatizo. Ukiona matendo ya aina hiyo, ni ishara kwamba ikulu yetu imejaa makapi. Ikulu imejaa marafiki wa Rais badala ya watendaji ambao wangemurudisha kwenye mpangilio rais, hata kama ni -----.

nchi kama hii usitegemee kwamba itaendelea. Hawa mabwege wanachokifanya ni kuiba na kutamba kwamba sisi ndo wenyewe. Hawana lolote wanaloweza kufanikiwa.
 
Pole warioba inchi imekamatwa na wahuni tulia mzee

Kwani Warioba hakujua kuwa akishawasilisha Rasimu Bungeni Tume inavunjwa? Kwa hiyo alitakiwa ajiandae mapema wakati anawasilisha Rasimu wanatume wenzake wangekuwa wanamsaidia kupaki virago kuliko "kusubiri taarifa!"
 
Pole sana mzee wetu.....kwa kweli serikali hii ya maccm inaendeshwa kihuni. Hata wewe muasisi wanakutenda namna hiyo?
 
Mara zote binafsi nimeamini kwamba ktk nchi yoyote ile, kuna sekta ambazo ni muhimu na ni lazima nchi itambue hilo na ajira ktk ofisi hizo iwe ni kwa watu ambao ni wazuri kichwani. Central bank, Ikulu, planning unit. Hizi siyo sehemu za kumwaga wachovu kichwani.

angalia nchi hii TZ, angalia walioko ikulu, angalia walioko BOT, ni tatizo. Ukiona matendo ya aina hiyo, ni ishara kwamba ikulu yetu imejaa makapi. Ikulu imejaa marafiki wa Rais badala ya watendaji ambao wangemurudisha kwenye mpangilio rais, hata kama ni -----.

nchi kama hii usitegemee kwamba itaendelea. Hawa mabwege wanachokifanya ni kuiba na kutamba kwamba sisi ndo wenyewe. Hawana lolote wanaloweza kufanikiwa.
Lkn mkuu haya mambo yanafanyika wtz wanaona nihuuni bei gani.tume imetumia mkuu anza kuchukua hatua wengine watafuata
 
ah! Waziri wa sheria na katiba kama sikosei ni Asha Rose Migiro, je, ana maelezo gani kuhusu hii taarifa? Nani alitoa amri toka Dodoma yenye maneno "kabidhi jengo mara moja?". Na iweje amri zinatoka Dodoma lakini malumbano na kebehi dhidi ya Tume yaendeshwe Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu?

Baada ya Jaji Warioba kutoa vitu vyake kwenye gari alirudi nyumbani kwa usafiri gani?

Taarifa ya jana ya Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu inasema kuwa Tume imefanya kazi nzuri na rais anafikiria kuwapa kama kinuua mgongo. Mimi ningeshauri Wajumbe wa Tume wasipokee hicho kinachoitwa kiinua mgongo maana ni sawa na bloody money. Dharau gani hii?
 
Back
Top Bottom