Iko siku nchi nzima itakuwa giza kwa sababu ya kukumbatia walamba asali kina January Makamba

Paulsylvester

JF-Expert Member
Oct 15, 2021
1,467
3,381
Nasema hivi! Haiwezekani kuwa matatizo ya Tanesco yalikuwa sugu kiasi hiki

Ni mwaka sasa na miezi tangu tuambiwe Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) linaundwa upya na mitambo yake kufanyiwa ukarabati muda wa miezi miwili kwamba hatutaona tena kukatika kwa Umeme wala mtandao wa manunuzi ya Umeme, hakutajitokeza tena.

Cha ajabu sasa, ni mwaka na.... Umepita na matatizo yanazidi kuongezeka kila uchwao.

Yaani kununua Umeme imekuwa kero mpaka namtukuna matusi ya moyoni waziri wa hili dubwasha linaloitwa Nishati.

Sielewi ni kwa nini mh Waziri anapendelea kudharaulika kiasi hiki!

Sielewi kwa nini Waziri anakuwa hana ukweli wowote kwenye kila anachokisema kwa umma.

Sielewi kwa nini aamimiwe yeye tuu, Je wasomi wameisha kwenye nchi hii.?

Sielewi kwanini hata wawakilishi wetu hawawezi kusimama na wakasema na wakaonyesha msimamo wa kutokuwa na Imani naye! Na wakasema, sasa basi, January hufai na hutoshi kwenye Wizara hii na kwamba anaaibisha hata chama chao?

Sielewi kwa nini, sasa karibu wote watetezi wetu wa wananchi wameamua kuwa walamba asali na hawasemi, wapo tuu, akitokea mwenye kusema anaambiwa ni msaliti, Kwa namna hii, sahau maendeleo ya aina yoyote

Mh Waziri, ukweli hautoshi, na sasa hii wizara imekufanya uonekane kuwa mtu wa hovyo na ndoto zako zote za wewe siku moja uwe rais wa nchi hii, rasimi umezizika mwenyewe hutoaminiwa tena.

Huna mvuto tena, hufai tena, kwa nini Umeme unaweza kutokupatikana siku nzima kwa njia ya mtandao?

Iko siku moja, nchi italala Giza kwa sababu tuu walioko juu ni walamba asali.
 
Mmh really? Basi kwetu ulikuwa unakatika katika lkn baada ya Yale matengenezo kiukweli kabisa tuna Raha yaani umeme uko sawa kabisa, may be huko kwegine.
 
Binafsi niwe honest nimetokea kumchukia Sana January Makamba ni waziri wa ovyo ambaye anakingiwa kifua na kiongozi wake mkuu
 
Umejaribu kuandika kwa chuki binafsi pasipo na hoja ya kueleweka,

Kesho na genge lenu tapikeni Bungeni.
 
Inakaribia masaa 24 sasa hakuna huduma ya luku
Screenshot_20220624-014340_Messages.jpg
 
Back
Top Bottom