Ikiwa Uchaguzi 2015 Utaahirishwa, Nani kunufaika kati ya CHADEMA na CCM?

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,987
20,271
Kumekuwa na mtazamo na tetesi yakwamba huenda uchaguzi mkuu 2015 ukasogezwa mbele kupisha ujio wa Katiba MPYA,

Lakini ndani ya vyama vya siasa ambavyo kwa Tanzania ni viwili tu, (vingine ni matawi ya ccm) kumekuwa na mitazamo tofauti pia,

Baadhi ya Wanachadema wanasema utakinufaisha chama chao, na wengine wanasema utakidhoofisha, hivyo bado kuna mkanganyiko,

Vivyo hivyo baadhi ya Wanaccm wanasema sasa chama chao ndio kitakufa rasmi, kwa baadhi ya nilioonana nao nakuzungumza nao wanalaani sana kitendo cha serikali kufikiria kuahirisha uchaguzi huo,

Lakini kinyume baadhi ya wanaccm wamepokea tetesi za kuahirisha uchaguzi kwa furaha sana,

Wanajamvi naomba tuliangalie na kulichambua kichama zaidi sio kitafa!
 
Bila kujali nani atanufaika; Kuahirisha uchaguzi ni hila na hila ni jambo baya kabisa.La msingi uchaguzi ufanyike kwa wakati bila kujali nani ananufaika na nini. Huo ndio usahihi na uungwana.
 
Ikitokea ukaahirishwa nani atanufaika kati ya vyama hivi mkuu?
 
Mkuu hapo kwenye heading panastua kidogo kwa sisi wateja wao...
 
Wakati mwingine jitahidi kuwa msomaji siyo kila ukiamka unawaza unaanzisha uzi.

Sasa unataka watu wajadili tetesi ambazo hazipo, uchangu ndiyo nini?

Lini utaenda Butiama.
 
Please Yeriko turekebishie kichwa cha habari hapo juu neno (Uchangu).... Otherwise una mawazo mazuri
 
Last edited by a moderator:
Mkuu hapo kwenye heading panastua kidogo kwa sisi wateja wao...

mimi mbona nimeelewa kuwa amemaanisha UCHAGUZI?
hizi shule za kata zimetuharibia sana watu,ndio maana ukipewa ka tshirt tu roho safiii na kura unatoa
 
Kumekuwa na mtazamo na tetesi yakwamba huenda uchaguzi mkuu 2015 ukasogezwa mbele kupisha ujio wa Katiba MPYA,

Lakini ndani ya vyama vya siasa ambavyo kwa Tanzania ni viwili tu, (vingine ni matawi ya ccm) kumekuwa na mitazamo tofauti pia,

Baadhi ya Wanachadema wanasema utakinufaisha chama chao, na wengine wanasema utakidhoofisha, hivyo bado kuna mkanganyiko,

Vivyo hivyo baadhi ya Wanaccm wanasema sasa chama chao ndio kitakufa rasmi, kwa baadhi ya nilioonana nao nakuzungumza nao wanalaani sana kitendo cha serikali kufikiria kuahirisha uchaguzi huo,

Lakini kinyume baadhi ya wanaccm wamepokea tetesi za kuahirisha uchaguzi kwa furaha sana,

Wanajamvi naomba tuliangalie na kulichambua kichama zaidi sio kitafa!
Yaani hapo nilipo bold red sijakuelewa! mimi kwa mtazamo wangu umekurupuka jipange baba
 
Back
Top Bottom