Ijue Asili ya Siku ya Wajinga "The Fools Day"

Peter Mwaihola

JF-Expert Member
Jun 23, 2022
227
333
April mosi kila mwaka watu kutoka mataifa mbalimbali duniani huadhimisha siku ya wajinga "Fools Day".

Siku hii huambatana na matukio mbalimbali ikiwemo utani, fujo zisizoumiza na mitego ya matumizi ya akili baina ya watu na Watu au vyombo vya habari na hadhira yake.

Ingawaje haieleweki moja kwa moja asili ya siku hii lakini imekua ikivuta hisia za watu wengi duniani na kuhusisha shamrashamra kibao.

Baadhi ya wanahistoria wanaelezea kuwa siku ya wajinga ilianzishwa miaka ya 1582 wakati ufaransa ikihama kutoka kwenye matumizi ya Julian kalenda na kuanza matumizi ya Gregorian Kalenda.

Kwenye Julian kalenda mwaka mpya huanza siku ya April mosi kama ilivyo kwenye Kalenda ya kihindu.

Watu walioendelea kutumia Julian kalenda na kusherehekea siku ya mwaka mpya April mosi waliitwa wajinga wa April "April Fools".

Nchini uholanzi siku ya wajinga inaelezwa kuwa chanzo chake ni 158
72 ushindi wa wadachi dhidi ya Duke Álvarez de Toledo.

"Op 1 april verloor Alva zijn bril" ikiwa na maana kuwa "April mosi ndiyo siku ambayo Alvarez alipoteza nguvu yake".

Nchini Uingereza siku ya wajinga inasherehekewa tangu karne ya 18.
April mosi 1698 mamia ya watu mjini London walidanganywa kufika katika mnara wa jiji "London Tower" ili washuhudie Simba akiogeshwa kwa mara ya kwanza.

1992 nchini Marekani, redio za umma zilifanya mahojiano na Rais mstaafu, Richard Nixon akidai kuwa atagombea tena kiti cha Urais...kumbe hakuwa Nixon bwana, alikuwa ni mwigizaji tu aliyefanana sauti na Nixon na hiyo yote ilikuwa ni fujo ya siku ya April mosi kuwatania wasikilizaji.

Peter Mwaihola
IMG_16803261068710560.jpg
 
Back
Top Bottom