Igunga: CHADEMA na CCM watoana jasho, Magufuli akataa kwenda mahakamani

Mkwawa

JF-Expert Member
Jun 8, 2011
1,334
1,464
Hatimaye mahakama ya Igunga inayosikiliza kesi ya kupinga matokeo ya Ubunge Igunga inazidi kuwa ngumu baada ya habari kuwa waziri wa barabara nk kukataa kufika mahakamani kutoa ushahidi.

Magufuli anatakiwa mahakani kudhibitisha au kukanusha ahadi alizotoa kama waziri wakati wa uchaguzi. Kama mahakama itaridhia kufuta matokeo ya uchaguzi itailazimu tume ya taifa ya uchaguzi kuita uchaguzi upya.

Chaguzi zinagharama kubwa sana na zinakuwa ni za walipa kodi.

Katiba mpya lazima ingeweka hivi mapingamizi yote yasikilizwe kabla ya kutangazwa kwa mshindi ili kama kuna matatizo yaamuliwe na haki itendeke mapema na kama kuna kesi ifunguliwe ili kama kuna kasoro zirekebishwe na mshindi atangazwe bila kurudia uchaguzi.

Na vile vile makosa yawekwe bayana na kama ni ya kichama yaani ni matatizo ya wapiga debe chama kigharamie gharama zote za uchaguzi kwa uzembe wa kutumia watu wasio makini na janga kwa Taifa.

Igunga huenda uchaguzi ukarudiwa na hii itaonyesha matumizi mengine ya fedha za walipa kodi.

Je uchaguzi ukirudiwa tena mbwembwe za awali zitarudiwa ?? bastola, vituko vya wakuu wa wilaya, matumizi makubwa ya fedha lugha za matusi, dharau na minengua ya ajabu tutaviona??? Ahadi zile zile na kutekwa watu, kuumizwa na kuuliwa vitarudiwa tena???

wananchi wako roho juu roho chini. Tisa kumi uchaguzi unanukia kurudiwa huku Kafumu akiachwa haamini. Usichanganye siasa chafu na elimu haviendani.
 
ahadi kutimizwa zinahusiaana na uchaguzi kuwa halali?

Basi ccm wataondolewa pale karibu na ferry.
 
Mazingaombwe bado yanaendelea naona! Najua mkulu wa kaya hajapewa report, subiri utaona itakavyopinduliwa labda kama kuna connection za Kafumu na akina EL & Co. Hapo lazima wachinjie mbali
 
"MAHAKAMA IGUNGA YAMFUMUA KAFUMU"
*Yasema uchaguzi urudiwe ndani ya siku 70
*CCM yamlilia Magufuli, wasema amewahujumu
*CHADEMA wajipanga,wasema Hakuna kulala.

Nasubiri kichwa hiki cha habari soon!.
 
hii ndio bongo mkuu......naamini kuna watu huwa wanatengeneza mazengwe ili ukirudiwa tu wananyaka chao........
 
Namwomba Mungu ampe hekima
huyu Jaji afanye maamuzi yaliyo sahihi naamini akifanya hivyo hata Amani moyoni atakuwa nayo.ukweli sikuzote hukuweka huru!...
 
"MAHAKAMA IGUNGA YAMFUMUA KAFUMU"
*Yasema uchaguzi urudiwe ndani ya siku 70
*CCM yamlilia Magufuli, wasema amewahujumu
*CHADEMA wajipanga,wasema Hakuna kulala.

Nasubiri kichwa hiki cha habari soon!.

Mkuu< ebu funguka basi, umepandisha presha yangu mkubwa...........................
 
Hatimaye mahakama ya Igunga inayosikiliza kesi ya kupinga matokeo ya Ubunge Igunga inazidi kuwa ngumu baada ya habari kuwa waziri wa barabara nk kukataa kufika mahakamani kutoa ushahidi.

Magufuli anatakiwa mahakani kudhibitisha au kukanusha ahadi alizotoa kama waziri wakati wa uchaguzi. Kama mahakama itaridhia kufuta matokeo ya uchaguzi itailazimu tume ya taifa ya uchaguzi kuita uchaguzi upya.

.
Usipotoshe Umma Mahakama inayosikiliza kesi ni Mahakama ya Wilaya ya Nzega, Pia kuhusu suala la Magufuli limeisha tolewa uamuzi na Jaji na mjadala wa etetezi umekwishafungwa kilichobakia ni Hukumu tarehe 20.08.2012.
 
Mkuu Acha ubishi suala ni kwamba Magufuli alikataa kwenda kutoa ushaidi wakati kahusishwa kwenye mashtaka Jikite kwenye hoja acha longo longo
 
Haki ina gharama kuliko hizo pesa zenu za walipa kodi, ambazo kila siku ni "kasungura kadogo"
 
Nyinyiemu itamrudisha tena mkuu wa kaya wa zamani kuwa kampeni meneja. na hapo hapatatosha. nyinyiemu juuuuuuuuu!!!
 
Haki inathamani kubwa kuliko hizo fedha, swala hapa ni kila mtu kuwajibika kutimiza wajibu wake kama sheria na kanuni za uchaguzi zinavo taka na si kuamua kuilinda ccm iendelee kutawala hata kama wananchi hawaitaki,
 
Kule kwa rostamu ambaye ni gamba tamu kwa ccm................kweli ccm ni chama cha kinafiki sana na viongozi wake wanafiki...ndiyo maana nepi hakwenda kwenye kampeni kwa sababu ya unafiki huu nnaousema......mtu mnamuona mchafu na ni gamba afukuzwe lkn hapohapo mnamuomba awasaidie na mnawaacha wale mnaofikiri ni wasafi wasiende kumnadi mgombea..............kumbe kweli ccm inategemea uchafu kushinda chaguzi na mfano mzuri ni yaliyotokea igunga.....rostamu naye mshamba tu hata km ana hela zake, inakuwaje uojivue ubunge kwa sababu ya siasa uchwara za ccm alafu umpigie kura mgombea wa ccm kwa kutumia zilezile siasa uchwara
 
Mkuu Acha ubishi suala ni kwamba Magufuli alikataa kwenda kutoa ushaidi wakati kahusishwa kwenye mashtaka Jikite kwenye hoja acha longo longo
Sina ubishi na kilichoandikwa jana nilipost thread iliyoelezea mambo yote kuhusu Magufuli na majibu aliyotoa Magufuli huyu alietowa mada hii hayupo sahihi sana na isitoshe yupo mbali na tukio lilipo ndo maana ameshindwa kujua hata kesi inafanyika mahakama ipi, mi nafikiri we ndo unaleta longo longo jaribu kila siku kupita humu JF ili uwe updated huyu aliyeleta huu uzi kama jana angekuwa kapita humu leo angetulia Coz kila kitu kinaeleweka tangu jana.
 
Nilkuwa kwenye Ban kwi! kwi! kwi! kwi!
 
Back
Top Bottom