Ifahamu Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma na Majukumu yake

Da Prok tusaidie kujibu hapa
Daah, kuhusu kupoteza vyeti naona afanye inquiry na TCU ama Necta kama ni vya shule. Kwenda kule bila vyeti sio excuse bado hautafanya mtihani. Ingekuwa ni majina hapo ningeweza mshauri vizur zaidi awe na deed poll kwa usalama zaidi ama kama ana kitambulisho akafate barua ya utambulisho kwa mwenyekiti wa mtaa.
Inshort ukishafanya application, kama huna vyeti ama una vyeti copy, anza mapema mchakato na TCU ama chuo husika, au Necta kama ni vya shule. Ukishaenda kule wanapresume ulikuwa na muda wa kufanya yote hayo.
Ni hayo tu labda kama kuna mwenye mawazo zaidi au ushauri zaidi.
 
Nina swali: Ni hivi kwenye enterview kama mtu kapoteza vyeti lakini baadhi anavyo, je ni vitu gani anatakiwa aje navyo ili kuweza kufanya enterview?
huwezi fanya usahili kama huna kitambulisho tu hata kama vyeti vyako vinapicha hachilia mbali kupoteza vyeti

unachotakiwa kufanya tembelea TCU, NACTE au NECTA watakupa taratibu zao za kupata cheti mbadala na kwa kudokeza tu taratibu zenyewe mlolongo mpaka utangaze kwenye gazeti sijui miezi kadhaa
 
Sekretarieti ya Ajira kesho tunatimiza miezi minne(4 months) tangu mmetangaza nafasi za kazi za TPDC...mjitahidi kuchangamka kidogo. Au muwe mnatangaza when you are ready
20221226_200754.jpg
 
Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma imeanzishwa kwa mujibu wa kifungu cha 29(1) cha Sheria ya Utumishi wa Umma, Sura ya 298 (iliyorejewa 2019) kwa ajili ya kushughulikia mchakato wa Ajira katika Utumishi wa Umma na kuanzishwa rasmi tarehe 1 Machi, 2010.

Majukumu ya Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni;
  • Kutafuta wataalamu wenye ujuzi maalum na kuandaa mfumo wa kuhifadhi taarifa (kanzidata) za wataalamu hao ili kurahisisha utaratibu wa kuwaajiri pindi wanapohitajika;
  • Kuandaa orodha ya wahitimu wa Vyuo Vikuu na wataalamu wenye weledi kwa madhumuni ya kurahisisha rejea na ujazaji wa nafasi wazi za ajira katika Utumishi wa Umma;
  • Kutangaza nafasi wazi za kazi zinazotokea katika Utumishi wa Umma;
  • Kuhusisha wataalamu maalum kwa ajili ya kufanya usaili kulingana na mahitaji;
  • Kutoa ushauri kwa waajiri kuhusu masuala mbalimbali yanayohusiana na ajira; na
  • Kufanya kazi nyingine yoyote inayoendana na majukumu yake kadri itakavyoelekezwa na Waziri.
Idea ni nzuri,lakini uhalisia,ni madudu matupu,Rushwa tupu,watoto wa wakubwa wanapata ajira bila kupitia huu mfumo,huko wamewekewa watoto wa maskini ambso wazazi wao hawana connections/pesa.
Usome shule ya kata,uende chuo kwa mkopo,uombe ajira kupitia huu mfumo,harsfu upste nafasi wizara ya pesa,tra,madini,au bandarini!!ni rahisi ngamia kupita Tundu la sidano,kuliko kupata hiyo nafasi
 
Utumishi naomba kuuliza huu utaratibu wa kumpangia mtu kituo cha kazi unakuta unatokea mkoa wa mbali kwenda kureport alafu ukifika wanakupokea then wanakwambia ondoka tutakupigia simu siku ya kureport rasmi... inakuwaje kwamba hamjawasiliana na hizo taasisi zikawapa tarehe husika za watu kuhitajika kule ili kuepusha usumbufu na garama!
Taasisi pia inataratibu zake za kukamilisha ajira kwa watumishi.

Mambo mengi hufanyika kama uhakiki nyaraka zako hatimaye uungwe kwenye mkongo wa Taifa wa Asali(Cheque number).

Wakikuambia rudi kwanza watakujulisha ni ili washuguulikie hayo yote.

Bila kupata Cheque namba hutaweza kupata mshahara, kuwa mpole hadi wakuite na kukukabidhi cheque namba na kusaini mkataba ndipo uanze kazi
 
WADAU🛑 WADAU🛑WADAU🛑WADAU🛑



Nina swali Moja namba mnisaidie kupata majibu please.





Wadau hebu tuassume mtu umeomba kazi kwenye Taasisi mbili, Moja ni Chuo kikuu ambapo umeomba post ya TUTORIAL ASSISTANT na nyingine ni Taasisi ya kawaida ya serikali ambayo umeomba post ya MCHUMI.



Halafu ikatokea mfano mtu umeitwa kazini kwenye hiyo post ya TUTORIAL ASSISTANT ambapo baada ya muda ukaitwa kwenda kuchukua barua.



Mara baada ya kuchukua barua ukaitwa tena kwenye interview nyingine ya Taasisi nyingine hiyo ambayo uliomba post ya MCHUMI ambayo hapa sasa sio Taasisi ya ufundishaji ila nako ukaenda ukapiga interview ukatoboa mpaka oral.



Sasa swali langu ni Je kama ukitoboa mpaka Oral na oral pia ukafanya poa Je unaweza kuitwa kazini ilihali tayari ulishaenda kuchukua barua ya Ufundishaji ya post ya TUTORIAL ASSISTANT ambayo uliichukua chuoni ?



Na Je what if mtu umeanza kazi ya TUTORIAL ASSISTANT, let's say una miezi mitatu tokea uanze kazi je hapo inawezekana kwenda kuomba kazi ajira portal na kupita written na oral na kuitwa kazini ukapige kazi kama MCHUMI ilihali una miezi mitatu tu tokea uanze kazi chuoni kama TUTORIAL ASSISTANT?







Naombeni majibu kwa anayefahamu please🙏
 
Nyie watu wahuni wahuni tu mm nilifanya usaili mkasema majina mnaweka database cha ajabu mmeisha ita watu wengi wenye vigezo kama vya kwAngu bila kutoa database bora na nyie mkose ajira
 
Back
Top Bottom