If our President has more than one wife: The question of human rights

As long as hao wanawake hawakulazimishwa, mimi sioni sababu ya kupiga kelele kama waliolewa kwa hiari yao wakifahamu kuwa watakuwa wake wawili wakishea mme.


Nadhani jambo la kujiuliza ni kama itakuwa sahihi kwa serikali kuweka sheria ama za kupiga marufuku au kuhalalisha polygamism kwa pande zote mbili. Yaani kama polygamism inaruhusiwa, basi iwe pia halali kwa mwanamke kuolewa na wanaume zaidi ya mmoja naye awe anawapangia zamu za kula nao uroda, yaani ziwe ndoa za waume wengi wake wengi; na kama inapigwa marufuku basi iwe ni ndoa za mme mmoja mke mmoja.

Hii polygamism ya mme mmja wake wengi inawanyanyasa wanawake na kuwafanya waonekane kama ni sehemu za assets za mwanamme, na mwanamme ana haki ya kuongeza assets hizo kadri ya uwezo wake. Lakini kama itakuwa ni polygamism ambamo mwanamme na mwanamke wana haki sawa, mimi sina noma. Najua sitaoa mke wa pili ili nimtunze mke wangu huyu asije akaolewa na mme wa pili, unaweza kukuta yule mme wa pili anajua sana matindo kunizidi mie.

Ndugu yangu penda usipende "HAKUNA USAWA KATI YA MWANAUME NA MWANAMKE" hii wanayosema ati haki sawa ni propaganda tu lakini ujue kutokana na Muumba alivyotuumba tofauti basi na haki zetu ni tofauti pia. muhimu ni kwa wanawake kudai haki zao zisidhulumie na wanaume lakini sio kutaka usawa ambao hautapatikana hadi kiyama kitasimama.
Hebu chukuwa mfano wa mwanaume mmoja akatembea na wanawake kumi na wote wakapata ujauzito. wakizaa watoto wote watamjua baba yao ni mmoja. sasa mwanamke akitembea na wanaume wawili tu akipata ujauzito haitakuwa rahisi kujua ni wa nani na kama mtoto akizaliwa bila ya kufanana na mmoja wao pia italeta utata kujua baba ni yupi hivyo kimaumbile tu haifai kwa mwanamke kuwa na wanaume wengi ila mwanaume anaweza bila shaka.
unajua binaadamu wa siku hizi tumezidisha sana kuharibu maadili tukijidai na utandawazi/kwenda na wakati na kutaka usawa. hebu angalia mfano hata kwa wanyama, utakuta kundi kubwa la wanyama wengi wakiwa majike na madume machache yakiwahudumia wote bila tatizo. haya ndio maumbile tusitafute usawa hapa tukaacha maumbile
 
Ni kweli wanawake sio sawa na wanaume. Wanaume wanaodhani wanawake ni sawa nao ndio wanaodhani men and women are interchangeable na matokeo yake wanaoa wanaume badala ya kuoa wanawake.

Wanawake wanapashwa kuwa na haki sawa na wanaume. Equal dignity.

Kuhusu uwiano, ukweli ni kwamba idadi ya wanawake katika nchi karibu zote inalingana, kwa karibu, na idadi ya wanaume. China ina wanaume wengi kuliko wanawake, na Botswana ina wanawake wengi kuliko wanaume.

Huu mlingano wa idadi ya wanawake na wanaume duniani ni ishara wazi, toka kwa Mwenyezi Mungu, kwamba ndoa iwe kati ya mwanamke mmoja na mwanamme mmoja.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom