Ndimbo M
Member
- Aug 30, 2023
- 13
- 62
Watu wengi wamepotosha kwa kutokujua kuhusu kitendo cha Tanzania kupiga kura katika baraza la Umoja wa mataifa ijumaa iliyopita kuhusu mzozo baina ya Israel na Hamas/ Palestina. Nasema kupotisha bila kujua kwa vile kuna mmoja kwa mfano,jioni ya leo kafikia hatua ya kusema Tanzania imepiga kura ya veto kuiunga mkono Palestina.
Kwanza anaonesha wazi kabisa haelewi maana kura ya veto, na pia haelewi ukweli kwamba ni nchi tano tu(America, Russia, China, France na UK) ndizo zenye kupiga kura ya veto. Na kura ya veto maana yake ni kupinga,..siyo kura ya kuunga mkono hoja au azimio.
Kwanza ieleweke, Tanzania ilishatoa msimamo wake ambao unataka pande zote zinazohusika katika mapigano katika huo mzozo zisitishe mara moja ili hatua za mazungumzo ya amani zichukue nafasi yake.
Pili, wiki hii kulikuwa na azimio katika baraza la umoja wa mataifa lililotaka wanaohusika kusitisha mapigano ili kuruhusu amani ya kudumu kutamalaki,na ili watu waweze kutoa misaada ya kibinadamu kwa wahanga.
Sasa azimio ili lipite ni lazima lipigiwe kura...,na kwa vile azimio lenyewe limeendana na msimamo wa Tanzania kwamba pande zote mbili zisitishe mapigano ili kupisha mazungumzo, ndo maana ikapigia kura. Tanzania haijapiga kura kuiunga mkono Palestina kama watu walivyopotosha, imepiga kura kusitisha mapigano ili kupisha huduma za kibinadamu (humanitarian truce)