Idd Simba ahusishwa na ufujaji wa mabilioni

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
Na Chalila Kibuda

KAMPUNI ya East African Meat ambayo mwenyekiti wake wa bodi alikuwa Waziri wa zamani wa Viwanda na Biashara, Idd Simba, inatuhumiwa kuchota na kutumia vibaya mabilioni ya shilingi zilizokuwa zitumike kwa ajili ya ujenzi wa machinjio ya kisasa jijini Dar es Salaam.

Ubadhirifu huo wa kutisha umegunduliwa jana na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) ilipokutana na uongozi wa Manispaa ya Kinondoni, ambapo hata matumizi ya kiwanja kilichokuwa kijengwe machinjio hayo yamebadilishwa.

Mwenyekiti wa LAAC, Augustine Lyatonga Mrema, alisema fedha hizo zilitolewa na Manispaa ya Ilala sh mil. 364, Kinondoni sh mil. 223, Temeke sh mil. 224 huku Halmashauri ya Jiji ikichangia zaidi ya sh bilioni moja.

Mrema alisema kuwa watu wanaotuhumiwa kuchota fedha hizo ni viongozi makini ambao pia wanatajwa kuwamo katika sakata la Shirika la Usafiri Mkoa wa Dar es Salaam (UDA).

Mrema alisema fedha hizi ni nyingi, na zingeweza kufanya kazi nyingine kwa ajili ya kuwahudumia wananchi lakini matokeo yake zimekwenda kwa wajanja wachache.

Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Dk. Didas Masaburi, alikiri kutoweka kwa fedha hizo na kudai kuwa zilikusanywa chini ya Idd Simba, ambaye alikuwa mwenyekiti wa bodi ya kampuni hiyo.

Hata hivyo, Masaburi alisema kampuni ambayo ilitatakiwa kuendesha machinjio hayo ilikwisha kufilisika kabla ya kuanza ujenzi huo na wanaotakiwa kuhojiwa ni waliokuwa watendaji na wajumbe wa bodi ya kampuni hiyo.

Waziri huyo wa zamani anatuhumiwa pia kuhusika na sakata ya uuzaji wenye utata wa Shirika la Usafiri la UDA ambapo inadaiwa kuwa fedha za mauzo ya shirika hilo ziliingizwa katika akaunti yake binafsi kinyume cha uuzaji wa mashirika ya umma.

Akionesha kukerwa na ubadhirifu huo mkubwa, Mrema alisema suala hilo
litafikishwa katika kikao cha Bunge lijalo kwa kuwashirikisha Waziri Mkuu na Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

"Nashangaa wanaotuhumiwa na wizi huu ni viongozi wa siku nyingi na wengine wanatuhumiwa katika sakata la Shirika la Usafiri Dar es Salaam, lakini wanaendelea kudunda bila kuchukuliwa hatua kali za kisheria," alisema Mrema.

Alisema kamati yake inaangalia namna ya kuchukua hatua kali ikiwamo kuagiza kukamatwa kwa wahusika na kufikishwa katika vyombo vya dola kwa hatua za uchunguzi na kisha kuwafikisha mahakamani wale wote watakaobainika kuhusika moja kwa moja na ubadhirifu huo.

Katika hatua nyingine, kamati hiyo ya Bunge imeubana vikali uongozi wa Manispaa ya Kinondoni kwa kuingia katika mkataba wenye utata na Oysterbay Villa ambao wamemilikishwa milele kinyume cha sheria za nchi.

Makamu Mwenyekiti wa LAAC, Idd Azzan, alisema kuwa waliohusika na mkataba wa aina hiyo na mingine isiyo na masilahi kwa taifa lazima wachukuliwe hatua za kisheria.

Kesho nitaitisha kikao cha wazee wa Dar es salaam na tuwe na agenda moja tu: kumvua Idd Simba uenyekiti wa wazee wa Dar es salaam ili apate muda wa kujisafisha dhidi ya tuhuma zinazomzunguka. Sisi wazee ndio wa kuombwa ushauri juu ya matatizo mbalimbali sasa kama mwenzetu huyu ana tuhuma nzito kiasi hicho atatukosesha moral authority ya kushauri ama kukemea uozo. Atupishe
 
Kule Ujerumani alizaliwa mtoto hana miguu akawekewa ya bandia na sasa ni mkimbiaji hodari wa pararampiki,nako China alizaliwa mtoto hana mikono akawekewa ya bandia na sasa ni mcheza karate maarufu mwenye mkanda mweusi,hizi zote ni kazi za Madaktari mabingwa wa nchi hizo.Na huko BAGAMOYO nako alizaliwa mtoto hana Kichwa akawekewa NAZI Na sasa ni RAIS wa JOmhari,kwa nini hayo ya akina Iddy yasitokee kwa kufuata huu mtirirko? na kweli wanadunda tu mtaani
 
Ajabu ni kwamba Rais bado anaweza kuendelea kumteua kuwa Mwenyekiti wa Bodi au Mjumbe wa Bodi kwenye mashirika mengine huku akiwa na rekodi mbaya ya utendaji iliyozungukwa na ubadhilifu kila mahali alikopita.
 
Na Chalila Kibuda

KAMPUNI ya East African Meat ambayo mwenyekiti wake wa bodi alikuwa Waziri wa zamani wa Viwanda na Biashara, Idd Simba, inatuhumiwa kuchota na kutumia vibaya mabilioni ya shilingi zilizokuwa zitumike kwa ajili ya ujenzi wa machinjio ya kisasa jijini Dar es Salaam.

Ubadhirifu huo wa kutisha umegunduliwa jana na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) ilipokutana na uongozi wa Manispaa ya Kinondoni, ambapo hata matumizi ya kiwanja kilichokuwa kijengwe machinjio hayo yamebadilishwa.

Mwenyekiti wne Lyatonga Mrema, alisema fedha hizo zilitolewa na Manispaa ya Ilala sh mil. 364, Kinondoni sh mil. 223, Temeke sh mil. 224 huku Halmashauri ya Jiji ikichangia zaidi ya sh bilioni moja.

Mrema alisema kuwa watu wanaotuhumiwa kuchota fedha hizo ni viongozi makini ambao pia wanatajwa kuwamo katika sakata la Shirika la Usafiri Mkoa wa Dar es Salaam (UDA).

Mrema alisema fedha hizi ni nyingi, na zingeweza kufanya kazi nyingine kwa ajili ya kuwahudumia wananchi lakini matokeo yake zimekwenda kwa wajanja wachache.

Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Dk. Didas Masaburi, alikiri kutoweka kwa fedha hizo na kudai kuwa zilikusanywa chini ya Idd Simba, ambaye alikuwa mwenyekiti wa bodi ya kampuni hiyo.

Hata hivyo, Masaburi alisema kampuni ambayo ilitatakiwa kuendesha machinjio hayo ilikwisha kufilisika kabla ya kuanza ujenzi huo na wanaotakiwa kuhojiwa ni waliokuwa watendaji na wajumbe wa bodi ya kampuni hiyo.

Waziri huyo wa zamani anatuhumiwa pia kuhusika na sakata ya uuzaji wenye utata wa Shirika la Usafiri la UDA ambapo inadaiwa kuwa fedha za mauzo ya shirika hilo ziliingizwa katika akaunti yake binafsi kinyume cha uuzaji wa mashirika ya umma.

Akionesha kukerwa na ubadhirifu huo mkubwa, Mrema alisema suala hilo
litafikishwa katika kikao cha Bunge lijalo kwa kuwashirikisha Waziri Mkuu na Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

“Nashangaa wanaotuhumiwa na wizi huu ni viongozi wa siku nyingi na wengine wanatuhumiwa katika sakata la Shirika la Usafiri Dar es Salaam, lakini wanaendelea kudunda bila kuchukuliwa hatua kali za kisheria,” alisema Mrema.

Alisema kamati yake inaangalia namna ya kuchukua hatua kali ikiwamo kuagiza kukamatwa kwa wahusika na kufikishwa katika vyombo vya dola kwa hatua za uchunguzi na kisha kuwafikisha mahakamani wale wote watakaobainika kuhusika moja kwa moja na ubadhirifu huo.

Katika hatua nyingine, kamati hiyo ya Bunge imeubana vikali uongozi wa Manispaa ya Kinondoni kwa kuingia katika mkataba wenye utata na Oysterbay Villa ambao wamemilikishwa milele kinyume cha sheria za nchi.

Makamu Mwenyekiti wa LAAC, Idd Azzan, alisema kuwa waliohusika na mkataba wa aina hiyo na mingine isiyo na masilahi kwa taifa lazima wachukuliwe hatua za kisheria.

Yaani Idd Simba kelele zote zile za kupigania wazawa ndo ulikuwa unamaanisha haya sukari+uda+machinjio...nakutakia maisha marefu ili siku magamba wakitolewa madarakani,ushitakiwe na ufungwe!
 
Huyu mrundi mwizi!! kila sehemu anadokoa tu. Watu kama hawa ni bora kupata historia zao wakati wa utoto, huenda lilikuwa toto dokozi. Yaani kila baada miezi mitatu lazima usikie uizi wa Iddi Simba, ingekuwa China angeshapigwa risasi zamani sana huyu babu
 
Lengo la mfanyabiashara yeyote yule awe mtanzania au la ni kupata faida kubwa kadri inavyowezekana. CDM hapo inabidi waangalie policies zao. Huwa wanapenda sana kushabikia wafanyabiashara wazawa kana kwamba ndiyo wenye uchungu na nchi.
 
Kumbe!

Iddi-Simba.jpg

Idd Simba,
Mwenyekiti wa Wazee Dar es Salaam
Kada wa Chama cha Mapinduzi
Fisadi wa UDA.
 
Kule Ujerumani alizaliwa mtoto hana miguu akawekewa ya bandia na sasa ni mkimbiaji hodari wa pararampiki,nako China alizaliwa mtoto hana mikono akawekewa ya bandia na sasa ni mcheza karate maarufu mwenye mkanda mweusi,hizi zote ni kazi za Madaktari mabingwa wa nchi hizo.Na huko BAGAMOYO nako alizaliwa mtoto hana Kichwa akawekewa NAZI Na sasa ni RAIS wa JOmhari,kwa nini hayo ya akina Iddy yasitokee kwa kufuata huu mtirirko? na kweli wanadunda tu mtaani

Kwani Huyo wa bagamoyo ndiye aliyemtuma Idd aibe? Simba amewwahi kutuhumiwa zamani kabla hata ya utawala huu, je hatua gani alichukuliwa? Au na hao waliomuacha mda huo walikuwa na vichwa vya nazi? Au hujui historia ya huyo mzee? Au yy ndiyo mahakama? Acha kuropoka kwa IDs za JF, kama ww mpambanaji yaseme haya kwa jina lako!
 
Lengo la mfanyabiashara yeyote yule awe mtanzania au la ni kupata faida kubwa kadri inavyowezekana. CDM hapo inabidi waangalie policies zao. Huwa wanapenda sana kushabikia wafanyabiashara wazawa kana kwamba ndiyo wenye uchungu na nchi.
Kwa hiyo unataka kusema kwamba wafanyabiashara wazawa hawana uchungu na nchi hii? Kwamba wao wanataka tu kupata faida?
Kama usemayo ni kweli basi mimi naogopa.
 
Back
Top Bottom