Idd Simba ahusishwa na ufujaji wa mabilioni

Kwani Huyo wa bagamoyo ndiye aliyemtuma Idd aibe? Simba amewwahi kutuhumiwa zamani kabla hata ya utawala huu, je hatua gani alichukuliwa? Au na hao waliomuacha mda huo walikuwa na vichwa vya nazi? Au hujui historia ya huyo mzee? Au yy ndiyo mahakama? Acha kuropoka kwa IDs za JF, kama ww mpambanaji yaseme haya kwa jina lako!

so utawala huu umuache?
 
Ajabu ni kwamba Rais bado anaweza kuendelea kumteua kuwa Mwenyekiti wa Bodi au Mjumbe wa Bodi kwenye mashirika mengine huku akiwa na rekodi mbaya ya utendaji iliyozungukwa na ubadhilifu kila mahali alikopita.
Kwenye lile sakata la UDA, JK (kupitia mwanae) alihusihwa na Simon Group. Sasa kama habari zile zilikuwa za kweli na haya yanayotokea sasa, pamoja nayo bado anateuliwa kushika nafasi zingine...naona ni suala la kuunganisha dots tu. 'Mrema amesema ni mtandao unaohusisha vigogo!
 
Nape zungumzia juu ya huyu kada wenu!watanzania tumemchoka sukari,uda,machinjio,shamba rukwa,NICOL vyote ni mabilioni
 
na chalila kibuda

kampuni ya east african meat ambayo mwenyekiti wake wa bodi alikuwa waziri wa zamani wa viwanda na biashara, idd simba, inatuhumiwa kuchota na kutumia vibaya mabilioni ya shilingi zilizokuwa zitumike kwa ajili ya ujenzi wa machinjio ya kisasa jijini dar es salaam.

ubadhirifu huo wa kutisha umegunduliwa jana na kamati ya bunge ya hesabu za serikali za mitaa (laac) ilipokutana na uongozi wa manispaa ya kinondoni, ambapo hata matumizi ya kiwanja kilichokuwa kijengwe machinjio hayo yamebadilishwa.

mwenyekiti wa laac, augustine lyatonga mrema, alisema fedha hizo zilitolewa na manispaa ya ilala sh mil. 364, kinondoni sh mil. 223, temeke sh mil. 224 huku halmashauri ya jiji ikichangia zaidi ya sh bilioni moja.


mrema alisema kuwa watu wanaotuhumiwa kuchota fedha hizo ni viongozi makini ambao pia wanatajwa kuwamo katika sakata la shirika la usafiri mkoa wa dar es salaam (uda).


mrema alisema fedha hizi ni nyingi, na zingeweza kufanya kazi nyingine kwa ajili ya kuwahudumia wananchi lakini matokeo yake zimekwenda kwa wajanja wachache.

meya wa jiji la dar es salaam, dk. Didas masaburi, alikiri kutoweka kwa fedha hizo na kudai kuwa zilikusanywa chini ya idd simba, ambaye alikuwa mwenyekiti wa bodi ya kampuni hiyo.

hata hivyo, masaburi alisema kampuni ambayo ilitatakiwa kuendesha machinjio hayo ilikwisha kufilisika kabla ya kuanza ujenzi huo na wanaotakiwa kuhojiwa ni waliokuwa watendaji na wajumbe wa bodi ya kampuni hiyo.


waziri huyo wa zamani anatuhumiwa pia kuhusika na sakata ya uuzaji wenye utata wa shirika la usafiri la uda ambapo inadaiwa kuwa fedha za mauzo ya shirika hilo ziliingizwa katika akaunti yake binafsi kinyume cha uuzaji wa mashirika ya umma.


akionesha kukerwa na ubadhirifu huo mkubwa, mrema alisema suala hilo
litafikishwa katika kikao cha bunge lijalo kwa kuwashirikisha waziri mkuu na waziri ofisi ya waziri mkuu, tawala za mikoa na serikali za mitaa (tamisemi).


“nashangaa wanaotuhumiwa na wizi huu ni viongozi wa siku nyingi na wengine wanatuhumiwa katika sakata la shirika la usafiri dar es salaam, lakini wanaendelea kudunda bila kuchukuliwa hatua kali za kisheria,” alisema mrema.


alisema kamati yake inaangalia namna ya kuchukua hatua kali ikiwamo kuagiza kukamatwa kwa wahusika na kufikishwa katika vyombo vya dola kwa hatua za uchunguzi na kisha kuwafikisha mahakamani wale wote watakaobainika kuhusika moja kwa moja na ubadhirifu huo.


katika hatua nyingine, kamati hiyo ya bunge imeubana vikali uongozi wa manispaa ya kinondoni kwa kuingia katika mkataba wenye utata na oysterbay villa ambao wamemilikishwa milele kinyume cha sheria za nchi.


makamu mwenyekiti wa laac, idd azzan, alisema kuwa waliohusika na mkataba wa aina hiyo na mingine isiyo na masilahi kwa taifa lazima wachukuliwe hatua za kisheria.





mzee iddi simba ana bahati sana ya kuishi hapa tanzania. Angekuwa china basi mpaka sasa angekuwa amashasaulika siku nyingi sana.
 
Huyu mrundi mwizi!! kila sehemu anadokoa tu. Watu kama hawa ni bora kupata historia zao wakati wa utoto, huenda lilikuwa toto dokozi. Yaani kila baada miezi mitatu lazima usikie uizi wa Iddi Simba, ingekuwa China angeshapigwa risasi zamani sana huyu babu

Ndo aliyeanzisha soko huria la uwakala na makapuni ya meli bila kulinda shirika kubwa lilokuwa na amali nyingi na mtaji mkubwa NASACO kufa kifo kitakatifu huku akifumbiwa macho hivihivi.
 
This guy stinks corruption! Mhhh! Kila kashfa lazima atie mkono wake??????
 
Nchi ishauzwa hii tokea zamani, wajanja ndio haooo wanachukua vyao kiulaiiiini kabisa. Nyie kalagheni bao maisha bora kwa kila mdanganyika yanawezeka chukua hatua.
 
Na Chalila Kibuda

KAMPUNI ya East African Meat ambayo mwenyekiti wake wa bodi alikuwa Waziri wa zamani wa Viwanda na Biashara, Idd Simba, inatuhumiwa kuchota na kutumia vibaya mabilioni ya shilingi zilizokuwa zitumike kwa ajili ya ujenzi wa machinjio ya kisasa jijini Dar es Salaam.


Ubadhirifu huo wa kutisha umegunduliwa jana na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) ilipokutana na uongozi wa Manispaa ya Kinondoni, ambapo hata matumizi ya kiwanja kilichokuwa kijengwe machinjio hayo yamebadilishwa.

Mwenyekiti wa LAAC, Augustine Lyatonga Mrema, alisema fedha hizo zilitolewa na Manispaa ya Ilala sh mil. 364, Kinondoni sh mil. 223, Temeke sh mil. 224 huku Halmashauri ya Jiji ikichangia zaidi ya sh bilioni moja.

Mrema alisema kuwa watu wanaotuhumiwa kuchota fedha hizo ni viongozi makini ambao pia wanatajwa kuwamo katika sakata la Shirika la Usafiri Mkoa wa Dar es Salaam (UDA).

Mrema alisema fedha hizi ni nyingi, na zingeweza kufanya kazi nyingine kwa ajili ya kuwahudumia wananchi lakini matokeo yake zimekwenda kwa wajanja wachache.
Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Dk. Didas Masaburi, alikiri kutoweka kwa fedha hizo na kudai kuwa zilikusanywa chini ya Idd Simba, ambaye alikuwa mwenyekiti wa bodi ya kampuni hiyo.

Hata hivyo, Masaburi alisema kampuni ambayo ilitatakiwa kuendesha machinjio hayo ilikwisha kufilisika kabla ya kuanza ujenzi huo na wanaotakiwa kuhojiwa ni waliokuwa watendaji na wajumbe wa bodi ya kampuni hiyo.

Waziri huyo wa zamani anatuhumiwa pia kuhusika na sakata ya uuzaji wenye utata wa Shirika la Usafiri la UDA ambapo inadaiwa kuwa fedha za mauzo ya shirika hilo ziliingizwa katika akaunti yake binafsi kinyume cha uuzaji wa mashirika ya umma.

Akionesha kukerwa na ubadhirifu huo mkubwa, Mrema alisema suala hilo
litafikishwa katika kikao cha Bunge lijalo kwa kuwashirikisha Waziri Mkuu na Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

"Nashangaa wanaotuhumiwa na wizi huu ni viongozi wa siku nyingi na wengine wanatuhumiwa katika sakata la Shirika la Usafiri Dar es Salaam, lakini wanaendelea kudunda bila kuchukuliwa hatua kali za kisheria," alisema Mrema.

Alisema kamati yake inaangalia namna ya kuchukua hatua kali ikiwamo kuagiza kukamatwa kwa wahusika na kufikishwa katika vyombo vya dola kwa hatua za uchunguzi na kisha kuwafikisha mahakamani wale wote watakaobainika kuhusika moja kwa moja na ubadhirifu huo.

Katika hatua nyingine, kamati hiyo ya Bunge imeubana vikali uongozi wa Manispaa ya Kinondoni kwa kuingia katika mkataba wenye utata na Oysterbay Villa ambao wamemilikishwa milele kinyume cha sheria za nchi.
ADMIN
MOD
WASITIRINI MAREHEMU NA NYIE.NJIA.MOJA.KAMA.MNAONA.POST ZINAONGELEA.MTU ASIEWEZA KYJIBU ASITIRIWE PLS NA AHESHIMIWE
OV
Makamu Mwenyekiti wa LAAC, Idd Azzan, alisema kuwa waliohusika na mkataba wa aina hiyo na mingine isiyo na masilahi kwa taifa lazima wachukuliwe hatua za kisheria.
 
Back
Top Bottom