A
Anonymous
Guest
Kumekuwa na changamoto kwa watumishi wa idara ya afya Korogwe kulipwa fedha za on-call allowances; huu ni mwezi wa nane tangu February wakiuliza wanagombezwa na viongozi (ofisi ya mganga mkuu wilaya ya Korogwe) hasa watumishi kituo cha afya Mombo.
Pili, kumekuwa na changamoto ya kuwalipisha malipo wajawazito wakati wa kufanya vipimo kwenye Kliniki za ujauzito na wakati wa upasuaji wa uzazi kama mama atatakiwa kujifungua kwa upasuaji anaambiwa alipie vifaa zaidi ya elfu 60 na kuendelea; wakiuliza wanaambiwa ni utaratibu wa Wilaya wakati ni kinyume na maagizo ya Serikali kwenye kituo cha afya Mombo.
Tatu, mganga mfawidhi katika kituo hicho ni mkorofi, hana ushirikiano na watumishi wenzake hasa kwenye kutatua changamoto za mahitaji ya watumishi hao kufanyia kazi jambo linaloshusha ari ya kufanya kazi kwa kuwa wanafanya kazi kwenye mazingira magumu ya kutolipwa madai yao ya muda wa ziada.
Nne, labor ward vitoto vichanga vinakufa Vingi kwa sababu ya huduma mbovu ya uzazi; hakuna vifaa vya kuzalishia, utakasaji wa vifaa haufuatwi kiasi cha sisi tunaopata huduma tunaogopa kuambukizwa magonjwa wakati wa kujifungua kwenye kituo hicho.
Labor ward na theatre kuna rushwa tunaombwa fedha wakati wa kupata huduma , mimi mwenyewe wakati wa upasuaji wa kujifungua nilitoa fedha kama elfu 65 nikaambiwa na madaktari wa theatre ni za vifaa vya dharura.
Mdogo wangu mwenyewe huko labor ward pamoja na mtoto kufariki kwa sababu ya uzembe wao wa kutokuwa na vifaa salama bado tuliombwa fedha 20000 ya kujifungua eti masona.

- Hospitali vitanda na magodoro vina kunguni na wana magodoro mapya hawabadilishi.
- Nyakati za usiku duka la dawa wanafunga na hivyo huduma ya dawa tunalazimika kwenda kununua nje ya hospitali na ni mbali. Hii imekuwa changamoto ya siku nyingi tumeulizia kwenye mikutano ya kijamii mganga mfawidhi anatujibu wanashughulikia lakini tunasikia ametumia fedha nyingi kukarabati duka la nje kwa ubadhirifu kwa hiyo lipo ni chumba tu. Sisi tunapata shida usiku tukija kupata huduma.