Idara husika na ajira Serikalini acheni ubaguzi wa kuhitaji GPA. TCU pia jirekebisheni utendaji wenu

Zygot

JF-Expert Member
Apr 14, 2016
2,251
2,875
Kuna kilio kikubwa sana toka kwa watu ambao hawakusoma vyuo vya Tanzania yetu. Ajira za serikalini zinazoelekezwa katika vyuo vya elimu ya juu vinahitaji uwe na kiwango fulani cha GPA, nadhani iwe 3.8 kwenda juu. Hili ni hitaji sahihi lakini kuna tatizo la kukariri neno GPA hata kwa watu wasiohusika. Vyuo vingi vya nje ya Tanzania, havitumii ufaulu huo wa GPA.

Matokeo yake waliosoma nje ya Tanzania hawapati ajira ktk sehemu hizo kwa kisingizioa cha kutokuwa na GPA kwenye vyeti vyao. TCU wanachofanya ni kutapeli watu pesa zao kwa kisingizio cha kuidhinisha vyeti vyao, lakini huwa hawawezi kuvitafutia hiyo GPA ili viendane na mahitaji ya Tanzania.

Muhimu ni kwenu Tume ya ajira serikalini, rekebisheni mahitaji yenu ya ajira na kuelewa kwamba GPA siyo kipimo cha dunia yote ktk elimu. TCU pia acheni kuchota pesa za watu kwa kisingizio cha kuthibitisha vyeti vya watu, wakati hakuna lolote linalofanyika ktk ofisi zenu.
 
Ajira haiangalii cheti, but uwezo wa kujieleza ukaeleweka.
Boss, utajieleza kwa nani? Barabarani? Muwe munasoma kinachojadiliwa na kuelewa. Mimi nimeelewa na ninafahamu kwamba kuna matangazo megi yanayolazimisha uwe na GPA ya kiwango fulani. Wakati huo kuna watu wana vyetu visivyoonesha GPA. walikosoma hakuna mtindo huo.

Swali, kwa nini Watu wa ajira wanangángána na GPA wakati siyo jambo la lazima ktk Dunia hii? Yaani hawajui dunia hii inakwenda wapi?
 
Huu ujinga wa kuanzisha mambo bila kuwa na watu wanaoielewa dunia ni hatari sana. Itachukua muda kabla hao watu wa utumishi hawajagundua kosa lao. Halafu nimesikia kuna vijana wanaojiita wa IT ndo wanaamua kufunga mtandao au kufungulia mtu fulani. ni udhaifu tupu!! Vijana munaotafuta kazi serikalini jitahidini san kupiga kelele.
 
Nimeangalia badfo wanatoa m,atangazo yakihitaji GPA bhla! bhla! Hawa watu wana elimu gani huko serikalini?????
 
Back
Top Bottom