Idadi ya ndoa za wasagaji na mashoga

Mbonea

JF-Expert Member
Jul 14, 2009
640
20
Idadi ya ndoa za wasagaji na mashoga nchini Marekani zimeongezeka maradufu kiasi cha kwamba mwaka jana kulikuwa na ndoa laki moja na nusu za watu wa jinsia moja.

Jumla ya ndoa 150,000 za watu wa jinsia moja (mashoga na wasagaji) zilifungwa mwaka jana nchini Marekani ikiwa ni idadi kubwa sana kulinganisha na idadi ambayo serikali ya Marekani ilikuwa ikitambua, taarifa ya awali ya sensa ya ndoa za jinsia moja iliyofanyika nchini Marekani ilionyesha.

Asilimia 27 ya mashoga 564,743 waliopo nchini Marekani walisema kuwa wanaishi kama mume na mke, taarifa iliyotolewa na kitengo cha sensa cha Marekani ilisema.

Kitengo hicho cha sensa kilisema kuwa pea 100,000 za watu wa jinsia moja walifunga ndoa kisheria mwaka jana huku wengi wakiamua kuishi wenyewe kama mume na mke bila kufunga ndoa.

Utafiti ulionyesha kwamba idadi ya ndoa hizo ingekuwa kubwa zaidi iwapo kama sheria ya kuruhusu ndoa ya jinsia moja ingekuwa inatumika kwenye majimbo yote ya Marekani.

Utafiti huo ulionyesha zaidi kuwa mashoga wengi na wasagaji nchini Marekani wangependa kufunga ndoa lakini sheria zinazokataza ndoa za jinsia moja katika majimbo wanayoishi zimewabana na kuwafanya washindwe kufanya hivyo.

Hadi mwaka jana ni majimbo manne tu ya Marekani, California, Massachusetts, Iowa na Connecticut ambayo yalikuwa yakiruhusu kisheria ndoa za jinsia.

Inakadiriwa kuwa mfumuko wa ndoa hizo utajitokeza zaidi kwenye sensa ya mwaka 2010.

Katika ndoa 149,956 za jinsia moja zilizofungwa nchini Marekani mwaka jana asilimia 56 ya ndoa hizo ni za wanawake wanaosagana.

Ingawa sensa hiyo ilionyesha kuongezeka kwa ndoa hizo, kulikuwa hakuna takwimu zilizotolewa kuonyesha idadi ya ndoa za jinsia moja zilizovunjika.

Bwana Curtis Chin, 41, na bwana Jeff Kim, 43, wa Los Angeles, ni miongoni mwa mashoga ambao wanampango wa kujiandikisha kwenye sensa hiyo wakijitambulisha kuwa na wao ni mke na mume.

Wawili hao walipanga kufunga ndoa na kufanya sherehe kubwa mwaka huu lakini baada ya kusikia kuwa wakazi wa California walikuwa na mpango wa kupiga kura kupiga marufuku ndoa za jinsia moja waliamua kufunga ndoa ya bomani mwaka jana ili ndoa yao itambulike kisheria.

Chin alisema kuwa yeye na Kim hawatajihisi kuwa wamefunga ndoa mpaka watakapofanya sherehe kubwa itakayohudhuriwa na familia zao pamoja na marafiki zao.
 
Back
Top Bottom