Huyu Pastor Dominic (kiboko ya wachawi) ni mkweli?

Papaa Gx

JF-Expert Member
Oct 10, 2016
10,098
15,685
Kuna huyo pastor anajiita Dominic (kiboko ya wachawi) nadhani kuna wanao mfahamu mi nauliza tu ni mkweli ama tapeli kama wengine?

Kuna siku natafuta channel ya kusikiliza kwenye radio mara nikasikia mahubiri yake, nikaona ngoja nitege sikio. Jamaa mahubiri yake yamelenga kuwakomesha wachawi, kipindi anaendelea kutoa hayo mahubiri yake aliruhusu watu kupiga simu.

Katika kupiga simu anakuuliza majina yako kisha jamaa anakwambia shida yako mpaka wabaya wako walio kuletea hayo mabalaa. Anaenda mbali mpaka anakutajia mazingira ya nyumbani kwako mpaka namna ilivyo. Kifupi huyo jamaa kila anacho kisema kwako unabaki unashangaa amejua vipi, maana wale walio piga simu walikuwa wanakubali tu kila wanacho ambiwa na kusema ni kweli kabisa.

Kuna dada alipiga simu, shida yake ilikuwa mama yake akisumbuliwa na saratani ya mapafu huyo mama yake kwa maelezo yake alikuwa hawezi kupumia. Basi pastor Dominic akamwambia hilo tatizo amelipata kutokana na ushirikina alio fanyiwa na mdogo wake. Akamwambia aandae mafuta ya kupikia ili ayaombee kisha ampake mwilini, dada akafanya hivyo kisha jamaa akapiga maombi hapo baada ya kumaliza akamwambia ampake hayo mafuta kichwani, kifuan, miguuni na sehemu nyingine. Kipindi anapaka hayo mafuta jamaa anapiga maombi, mara yule mama akaanza kupumua dada akawa haamini anacho kiona akabaki analia tu sijui ndio furaha. Pastor akamwambia ashike miguu ya mama, yakapigwa maombi hapo mara mama akasimama kwa maelezo dada alie kuwa karibu na mama yake. Hizo drama mimi ziliniacha hoi

Ukafika wakati wa shuhuda toka nimesikia hizo shuhuda ni wadada tu sikusikia shuhuda yoyote ya mwanaume. Ata kwenye kupiga simu ni wadada tu nilibaki najiuliza Sana hiyo kitu.

Huyu jamaa kama ni mkweli kwanini alikuwa anajipigia promo ya kutafutwa sana na kusihii kuonana nae pale kanisani kwake maana ilikuwa haipiti dakika moja lazima ataje namba zake. Najua hapa jukwaani kuna raia kibao na huenda kuna baadhi wanamfahamu, huyo jamaa ni mkweli ama ni tapeli tu kama wale wengine?

Karibu.
 
Enyi wajinga ni nani aliyewaroga?
Je, una uhakika kuwa hao waliopiga simu kuwa si miongoni mwa cabinet yake?
Siku moja tapeli mmoja ana sauti ya kukoroma huwa unampigia simu anakutabiria. Nikamwambia wife ngoja nimpigie huyu tapeli uone jinsi anavyotabiri uongo.
Hawa Jamaa wanatumia saikolojia simple sana kukuhadaa. As you talk to them wanapata mpenyo wa kuhisi hali yako ya maisha.
Akaniamba nahangahika kutafuta kazi pasi na mafanikio nimerogwa. Huku maishani mwangu sikuwahi kusotea kazi. Nimeajiriwa tangu tu namaliza skuli.
 
Taja kwanza ni radio gani na ni mda gani ili nimsikilize na wewe ulisikiliza lini ndani ya week.

Huyo nmeambiwa kwenda private kumuona ni 200k akutajie hao wachawi sasa kama huna wachawi sijui atakwambia nini.

Tuzidi kulijua neno la Mungu ili kuepuka haya.
 
Kuna huyo pastor anajiita Dominic (kiboko ya wachawi) nadhani kuna wanao mfahamu mi nauliza tu ni mkweli ama tapeli kama wengine?

Kuna siku natafuta channel ya kusikiliza kwenye radio mara nikasikia mahubiri yake, nikaona ngoja nitege sikio. Jamaa mahubiri yake yamelenga kuwakomesha wachawi, kipindi anaendelea kutoa hayo mahubiri yake aliruhusu watu kupiga simu.

Oyooo
Mbona hautaki apate wafuasi wengine!!! taja jinala redio na muda.
la ziada jijenge mwenyewe kiimani na kwa kusoma neno lake Mola.
 
Ukishaamini supernatural powers za huku kwanini usiamini za kule ? Binafsi takwambia ni uongo yule atakwambia ni ukweli na sababu Imani haiitaji Proof beyond reasonable doubt itabidi niseme..., To each their Own....
 
Kuna huyo pastor anajiita Dominic (kiboko ya wachawi) nadhani kuna wanao mfahamu mi nauliza tu ni mkweli ama tapeli kama wengine?

Kuna siku natafuta channel ya kusikiliza kwenye radio mara nikasikia mahubiri yake, nikaona ngoja nitege sikio. Jamaa mahubiri yake yamelenga kuwakomesha wachawi, kipindi anaendelea kutoa hayo mahubiri yake aliruhusu watu kupiga simu.

Katika kupiga simu anakuuliza majina yako kisha jamaa anakwambia shida yako mpaka wabaya wako walio kuletea hayo mabalaa. Anaenda mbali mpaka anakutajia mazingira ya nyumbani kwako mpaka namna ilivyo. Kifupi huyo jamaa kila anacho kisema kwako unabaki unashangaa amejua vipi, maana wale walio piga simu walikuwa wanakubali tu kila wanacho ambiwa na kusema ni kweli kabisa.

Kuna dada alipiga simu, shida yake ilikuwa mama yake akisumbuliwa na saratani ya mapafu huyo mama yake kwa maelezo yake alikuwa hawezi kupumia. Basi pastor Dominic akamwambia hilo tatizo amelipata kutokana na ushirikina alio fanyiwa na mdogo wake. Akamwambia aandae mafuta ya kupikia ili ayaombee kisha ampake mwilini, dada akafanya hivyo kisha jamaa akapiga maombi hapo baada ya kumaliza akamwambia ampake hayo mafuta kichwani, kifuan, miguuni na sehemu nyingine. Kipindi anapaka hayo mafuta jamaa anapiga maombi, mara yule mama akaanza kupumua dada akawa haamini anacho kiona akabaki analia tu sijui ndio furaha. Pastor akamwambia ashike miguu ya mama, yakapigwa maombi hapo mara mama akasimama kwa maelezo dada alie kuwa karibu na mama yake. Hizo drama mimi ziliniacha hoi

Ukafika wakati wa shuhuda toka nimesikia hizo shuhuda ni wadada tu sikusikia shuhuda yoyote ya mwanaume. Ata kwenye kupiga simu ni wadada tu nilibaki najiuliza Sana hiyo kitu.

Huyu jamaa kama ni mkweli kwanini alikuwa anajipigia promo ya kutafutwa sana na kusihii kuonana nae pale kanisani kwake maana ilikuwa haipiti dakika moja lazima ataje namba zake. Najua hapa jukwaani kuna raia kibao na huenda kuna baadhi wanamfahamu, huyo jamaa ni mkweli ama ni tapeli tu kama wale wengine?

Karibu.
Vya wajinga ndio viliwavyo!
bado tuna safari ndefu kufuta ujinga, umasikini na maradhi.
 
Back
Top Bottom