FaizaFoxy
Platinum Member
- Apr 13, 2011
- 92,926
- 109,317
We tutakuuliza Waarabu wa K'koo wabulushi wa Mbeya niachie mimi.
Hao ni shemeji zangu tena damu damu, unanchekesha.
We tutakuuliza Waarabu wa K'koo wabulushi wa Mbeya niachie mimi.
wewe si ulijidai mjuaji unamfahamu kwa undani huyu mulla?umesema ana biashara 'nyingi' ana vibali na leseni za hizo biashara 'nyingi' sasa tuwekee hivyo vibali au leseni tuvione!
Niende wizarani wakati wewe upo?
Mulla apora Kiwanda cha Chai, Lupembe
MUVYULU ni Muungano wa Vyama vya Msingi toka katika vijiji 9 vya Tarafa ya Lupembe.MUVYULU kilianzishwa mwaka 1998, kimesajiliwa kisheria , na kinaongozwa na Bodi ya Wakurugenzi, wakiwakilisha vyama vya msingi vilivyounda MUVYULU.
MUVYULU, kama chama kinamiliki hekta 215 za mashamba ya Chai na kina hisa katika Kiwanda cha Kusindika chai cha Lupembe. Kuna jumla ya wakulima 6036 wanaomiliki mashamba binafsi ya chai yenye jumla ya hekta 4200, nje ya shamba la ushirika. Mashamba haya yana uwezo wa kuzalisha tani zaidi ya 10,000 za majani mabichi kwa mwaka , ambayo yanapouzwa huwapaia wakulima waastani wa shilingi bilioni 1.3. Baada ya kuisindika chai huliingizia taifa dola milioni 3.3 za Kimarekani kwa mwaka.
Kabla ya Ubinafsishaji, Kiwanda cha Kusindika chai cha Lupembe kilimilikiwa kwa ubia kati ya Serikali na MUVYULU ambapo serikali ilimiliki asilimia 25.76% na MUVYULU kilimiliki asilimia 74.24% ya hisa zote.. Tarehe 19/03/2004 MUVYULU na PSRC walisaini mkataba wa kuuza hisa asilimia 70% kwa kampuni ya Dhow Mercantile(EA) Ltd kwa lengo la kuboresha uzalishaji na usindikaji. MUVYULU kilibakia na asilimia 30% za hisa katika ubia huo. Makubaliano yalikuwa kwamba kampuni ya Dhow Merchantile ilipe asilimia 10% mara moja baada ya kusaini makubaliano, asilimia 40% baada ya kusaini mkataba wa mauzo na asilimia 50% ndani ya kipindi cha miezi 12 tangu kusaini mkataba .
Hadi sasa ni mwaka wa saba unakwisha tangu Dhow Merchantile wachukuwe kiwanda na hawajalipa malipo ya asilimia 50% kama makubaliano ya mkataba yalivyo walitakiwa wawe wamelipa ndani ya miezi 12.. Kwa maana nyingine, Dhow Merchantile wamevunja mkataba . Cha kusikitisha zaidi, Dhow Merchantile wameteka nyara mamlaka yote ya Kiwanda kwa kukataa kuishirikisha MUVYULU kwenye uongozi na udhibiti wa mapato na matumizi ya kiwanda kama mkataba unavyoelekeza. Jitihada zote za PSRC na MUVYULU za kuwataka Dhow Merchantile kutimiza masharti ya mkataba na kuwashirikia MUVYULU katika uendeshaji wa kiwanda zimegonga mwamba.
Katika jitihada za kuendelea kutafuta suluhu kabla ya kutumia kifungu cha mkataba kinachowezesha kuvunja mkataba kama wanachama hawanufaiki na uendeshaji wa kiwanda,. Bodi ya MUVYULU ilimwita Mwenyekiti wa Kampuni ya Dhow Merchantile,Ndugu Yusuf Mulla tarehe 19/12/2007 ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Mbeya ili kuzungumza na kutatua matatizo hasa ya kumalizia malipo ya mauzo ya 50% na kushirikishwa katika uendeshaji wa kiwanda.
Kwa masikitiko makubwa Ndugu Mulla aliijibu Bodi kwamba, nanukuu " siwezi kuzungumza na mbwa bali nazungumza na mwenye mbwa!" na kwamba "hamwezi kufanya chochote kwa kuwa IKULU ni sebuleni kwangu".Mwisho wa kunukuu .
Kwa kuona dharau, kiburi na majigambo ya Ndugu Mulla, tarehe 24/07/2008 MUVYULU ilisitisha mkataba wa ubia wa kumiliki kiwanda cha Lupembe na Dhow Mercantile(EA) Ltd kwa kutumia taratibu na sheria za makubaliano ya awali. Dhow Merchantile walipewa siku saba(7) na Consolidated Holding Corporation (mrithi wa PSRC) kukabidhi kiwanda. Hata hivyo, Dhow Merchantile walikaidi amri hiyo. Wanachama wa MUVYULU walikifunga kiwanda ili kunusuru mali na rasilimali zake.
Hadi sasa kiwanda kimeendelea kufungwa kwa kuwa Dhow Merchantile wamefungua kesi mahakamani inayohusu migogoro ya umiliki kati yao wenyewe na kuihusisha MUVYULU. Madhara ya kufunga kiwanda ni mengi na makubwa. Wananchi na wanachama wa MUVYULU wameendelea kuathirika kiuchumi, chai inaharibikia mashambani, kwa wale wanaouza kwenye viwanda vingine wanauza kwa bei ya chini sana, mara nyingine chai inaharibika kabla ya kufikishwa kiwandani kwa sababu ya umbali na serikali inaendelea kupoteza fedha za kigeni ambazo ni muhimu sana kwa ustawi wa uchumi wetu..Aidha uuzaji holela wa majani mabichi ya chai umesababisha kushuka kwa ubora wa chai ya Lupembe kwenye soko la dunia.
Wananchi na wanachama wa MUVYULU hawana kesi na Dhow Merchantile. Wao ndiyo waliovunja mkataba kwa ujeuri na kiburi chao. Wakulima wa chai wanasikitika jinsi wanavyoteseka na kuathirika kiuchumi na kimaendeleo kwa sababu ya kiburi cha mtu mmoja.Upo usemi unaosema "mwenye pesa si mwenzio". Pengine ni kwa sababu ya unyonge wa wakulima ndiyo maana hawajapata haki licha ya kuwa wabia wa kiwanda cha Lupembe.
VITENDO VYA HUJUMA
Kesi aliyofungua Mulla mahakama kuu imekuwa ikihairishwa kila mara bila ya kusikilizwa, ambapo alipata hati batili ya mahakama ikionyesha kuwa ameshinda kesi ambayo anawaita wakulima kuwa ni wavamizi wa kiwanda chake. Baada ya kupata hati hiyo aliomba msaada wa kampuni ya Yono Action Mart tawi la Iringa wapeleke mabaunsa wao Lupembe kuondoa uongozi wa MUVYULU ndani ya kiwanda.
Yono kwa makubaliano na Mulla alitafuta mabaunsa wengi mjini Iringa na siku waliyokubaliana walipelekwa Lupembe kuondoa uongozi na kufungua kiwanda cha chai. Wakulima walipata habari za mpango mzima wa kuvamiwa kwa kiwanda chao. Wakulima nao walijipanga sawasawa kivita kukabiliana na mtu yeyote atakayeingia kwenye eneo la kiwanda.
Mabaunsa wa Yono walifika kiwandani majira ya asubuhi askari wa mlangoni wa kiwanda akawafungulia lango kuu nao wakaingia ndani, walipofika karibu na ofisi, wakajitokeza kundi ndogo la wakulima na wakaanza kuwahoji, madhumuni ya ujio wao, wale mabaunsa waliwadharau sana wale Wabena kwa ufupi wao, na wakawa wanalazimisha kuingia ofisini kwa nguvu kuwaondoa watumishi waliokuwepo, mara lilijitokeza kundi kubwa ajabu la Wabena waliokuwa wamelala chini ya miti ya chai, na mapambano yakaanza, mabausa walizidiwa na hawakuweza kufanya lolote, ikabidi wasalimu amri.
Lupembe ni nchi ya baridi sana hasa nyakati za asubuhi, wale mabausa walivuliwa nguo, wakabaki na chupi peke yake, waliamriwa kurudi walikotoka wakirushwa kichura na kuchapwa bakora za nguvu hadi walipofikishwa nje kabisa ya kiwanda.
Mkuu wa kituo kidogo cha Polisi cha Lupembe alipelekewa taarifa na Mwenyekiti wa serikali ya kijiji ambao wote walikuwa upande wa Mulla, wakiwa bado wapo kituoni Wabena wakafika na watuhumiwa, mkuu wa kituo cha polisi alichukua funguo za jela ya mahabusu, wakaingia yeye na mwenyekiti wa kijiji na kujifungia, kwa sababu wanajua vita ya Wabena ilivyo, wakati huo wakawa wanaomba msaada wa kikosi cha polisi kutoka wilayani Njombe, lakini walijibiwa hakuna askari yeyote kituoni. Yupo mama mmoja aliona hali ilivyo mbaya, kwa ushawishi wake aliwasihi wananchi watulie, akawa anafanya mazungumzo na mkuu wa polisi aliyejifungia selo.
Wananchi walitulizwa kwa kununulia bia na soda na wakawachia watuhumiwa, kisha wakatafutiwa gari lililowapeleka Njombe wakiwa mahututi kwa kipigo.
JARIBIO LA PILI
Mulla alifanya majadiliano na baadhi ya wakulima baada ya kuwapa vijisenti, kuwa atandaa maandamano na wakulima watabeba mabango, yanayolaani uongozi wa MUVYULU kwa kufunga kiwanda, kunakosababisha chai yao ikose sehemu ya kusindikia.
Aliwachukuwa wahandishi wa habari wa channel 10 ambao wangechukua picha na taarifa zote za tukio. Wabena walipata taarifa zote za mpango huo. Siku ya tukio Wabena wakaanza ndoria ya ulinzi tangu usiku, asubuhi zikafika gari mbili toka Njombe, na ndani walikuwepo waandishi wa habari wa channel 10. Walipofika eneo linaloitwa kibaoni magari yalisimamishwa na wananchi, na wakaanza kuhojiwa, walijitetea wamekuja kuchukua taarifa za matatizo ya wakulima baada ya kiwanda kufungwa. Walilazimishwa kufungua sehemu ya nyuma ya gari sehemu ya kuweka mizigo, na walipofungua yalikuwapo mabango mengi sana, yakiwalaumu viongozi wao.
Hali ilibadilika ghafula, kijana mmoja subira ilimshinda, mkononi alikuwa ameshika mnyororo unaozungusha gurudumu la baiskeli, aliurusha kichwani mwa kijana mmoja aliyekuwa na kamera, mnyororo ulijizungusha kichwani mwake kisha akauvuta, ulimchana kichwa vibaya sana, walianza kukimbia kuelekea ndani ya kanisa lililokuwa karibu, huku wananchi wakitoa kipigo cha nguvu. Alikuwepo msamaria mwema na gari yake, aliendesha hadi karibu na kanisa wale vijana wakaingia haraka na kuondoka kwa speed kubwa hadi kituo kidogo cha polisi. Kufika pale wakakuta polisi wamefunga kituo na kutokomea kusikoeleweka.
Mulla ameingia makubaliano na Tanesco na ameshavuna miti ipatayo 1,000,000 kutoka ndani ya shamba la miti la kijiji yenye thamani ya shilingi bilioni nane (8,000,000,000/=)
nionyeshe ni wapi nilipomtuhumu mulla kama mulla??!!!!Wewe si ndie unamtuhumu? tuoneshe wewe ni wapi kafanya kosa. Atakuwa na kapuni ya kusafirisha wanyama, tena holding area iko wazi kabisa, ukitoka KIA tu kuelekea Arusha unaiona waziwazi na kila mtu anaijuwa ni ya Mulla halafu unauliza leseni? kweli tuna ma great thinkers JF. Ulitaka kama namjuwa basi vibali vyake nikae navyo mimi? unanchekesha! halafu ubishani wako unaonesha ni mtoto mdogo wa shule, nenda kalele saa hizi, wachana na haya majukwaa hayakufai.
Uongo wa kupanga na majungu yasiyo na mpango.
PSRC hawauzi shirika lolote la umma lenye faida. Walishindwa kuliendesha Mulaa kanunua linaingiza faida wanalitamani. Mengine yote ya matusi na nini ni pumba tupu za kuwatia watu chuki. Nyie ndio wanga wenyewe, huwa mnauchungu wenzenu wanapoweza mliposhindwa nyinyi na ndio maana mpaka leo hamuendelei na kwa roho kama hiyo hamtaendelea maisha, wataoendelea ni wale tu wataobadilika na kustaarabika ki ukweli.
Nambie kuna shamba lipi la umma au shirika lipi la umma lenye faida inayostahili likauzwa? Wacha Uongo.
Hivi NMB ilikuwa ikiendeshwa kwa hasara??????? just curious!
nionyeshe ni wapi nilipomtuhumu mulla kama??!!!!
Kwa hiyo kuwa na kampuni(biashara) na holding area inayoonekana kiurahisi yatosha kusema biashara hiyo ni halali!!kweli wewe ndio great thinker!
Umeonyesha unamjua ki-undani sasa kwa nini iwe shida kuwa na vibali vyake?kama humjui we sema tu usijisikie aibu.
Nakusihi;kwa kuwa unalingana na bibi yangu kapumzike japo kidogo usije kuanguka msikitini, kesho iddi!
Kila kitu unakijua wewe. Hongera sana, Zawadi yako nitakuchinjia yule mwanakondoo wa maajabu mwenye baka leupe ubavuni special kwa ajili IDD.Sana tu, ilisha filisika! Lakini kwa sasa ni mlipa kodi wa hali ya juu Tanzania (Katika top ten).
Ama kweli KIRUSI aina ya FaizaFoxy kimeingia kwenye Jamii Forum. Hiki ni Kirusi pandikizi cha ccm. Ni cha hatari kama kimeta na ukimwi!!Sana tu, ilisha filisika! Lakini kwa sasa ni mlipa kodi wa hali ya juu Tanzania (Katika top ten).
Sana tu, ilisha filisika! Lakini kwa sasa ni mlipa kodi wa hali ya juu Tanzania (Katika top ten).
Now, the government is selling 49% of shares in the National Microfinance Bank, the largest bank in Tanzania, in November of this year. Currently PSRC (Presidential Sector Reform Commission), the Tanzanian Government's privatisation agency, is evaluating the pre-qualifications that were submitted by interested investors in September. Due to the size, power, asset value, and profitability of this bank, along with the good will that the bank will continue to soar in the next five to ten years, the government is taking extra steps in this process to ensure it gets what it deserves to benefit the country for the 49% stake of the bank. One method is an extra heavy price tag of close to Tshs. 20 billion (about $20 million USD). Additionally, there are strict terms and conditions set to the investors who submitted the bids. One of the key conditions is the consortium must include Tanzanian investors – and have solid Tanzanian influence. Secondly, the investor must be able to come up with the funding or have proof of the funding, to prove that they would in fact be able to handle the takeover. The other required qualifications are - experience in a number of privatisations of financial institutes (preferably in developing countries), knowledge of micro-finance business, financial and business anaylsis and merchant banking experience. - Source Bofya hapa
naona umeshachoka nakushauri ukapumzike!Onesha ni wapi haina uhalali?
unadhani ni binti huyu?Acha uongo binti!!!!!!
hii ni principle au fact?Uongo wa kupanga na majungu yasiyo na mpango.
PSRC hawauzi shirika lolote la umma lenye faida
.
Kila kitu unakijua wewe. Hongera sana, Zawadi yako nitakuchinjia yule mwanakondoo wa maajabu mwenye baka leupe ubavuni special kwa ajili IDD.
naona umeshachoka nakushauri ukapumzike!
unadhani ni binti huyu?