Huyu ni mtumishi wa umma, alipaswa aondolewe na ubunge si kutenguliwa uwaziri tu

Nyamesocho

JF-Expert Member
May 5, 2023
476
1,244
Nchi hii inahitaji marekebisho makubwa sana ya katiba kuhusu ukiukwaji wa maadili wa viongozi wa umma, hasa eneo la wabunge inapobainika wamevunja maadili ya utumishi wa umma.

Paulina Gekuli alipaswa avuliwe ubunge moja kwa moja, haiwezekani mwakilishi wa mwananchi ndiye mnyanyasaji wa mwananchi, halafu aendelee kuwakilisha wananchi.

Nchi zilizoendelea kwa kitendo hiki Paulina Gekuli alipaswa aondolewe awe raia wa kawaida na mashitaka yafuate.

Tunahitaji marekebisho ya katiba kuhusu eneo hili.
 
Tuache kutoa hukumu sisi sio Mahakama, Hatujaskiliza upande wa pili lkn tayari tumehalalisha kosa. Tuache kuendeshwa wa hisia na chuki.

Siasa siyo VITA,imekuwepo Kasumba CHADEMA mwanachama wao akihamia CCM anaombewa Njaa mpaka atakoma. Acheni hii tabia ya UCHAWI na dalili ya UMASKINI.
 
Mtu akitenguliwa na Rais ujue kuna asilimia 98 ya ukweli wa mambo kwa sababu Rais ni taasisi yenye vyombo vya juu vya uchunguzi
 
Tuache kutoa hukumu sisi sio Mahakama, Hatujaskiliza upande wa pili lkn tayari tumehalalisha kosa. Tuache kuendeshwa wa hisia na chuki.
Siasa siyo VITA,imekuwepo Kasumba CHADEMA mwanachama wao akihamia CCM anaombewa Njaa mpaka atakoma. Acheni hii tabia ya UCHAWI na dalili ya UMASKINI.
basi tuombe uchunguzi huru, ikibainika afukuzwe na kufunguliwa mashtaka
 
Nchi hii inahitaji marekebisho makubwa sana ya katiba kuhusu ukiukwaji wa maadili wa viongozi wa umma, hasa eneo la wabunge inapobainika wamevunja maadili ya utumishi wa umma.

Paulina Gekuli alipaswa avuliwe ubunge moja kwa moja, haiwezekani mwakilishi wa mwananchi ndiye mnyanyasaji wa mwananchi, halafu aendelee kuwakilisha wananchi.

Nchi zilizoendelea kwa kitendo hiki Paulina Gekuli alipaswa aondolewe awe raia wa kawaida na mashitaka yafuate.

Tunahitaji marekebisho ya katiba kuhusu eneo hili.
Nafikiri kila kitu kipo wazi kikatiba. Ili avuliwe ubunge, kama si wa kuteuliwa ni budi avuliwe uanachama wake kwenye chama kilichomsimamisha ugombea then automatic anakosa sifa ya kuwa mbunge.
 
Kwa hiyo ni suala la muda kwa kuwa kumvua uanachama kuna process zake.
 
Enough is enough acheni kumsakama Mama wa watu hata km alikosea Sasa imetosha wewe una mabaya mangapi ambayo unayafanya Gizani?

Mnakera sana au mmetumwa kumuandama akisema mnatumia nuksi na kumroga kila uchwao mtakataa yaan ngozi nyeusi hususani watanzania ni bure kabisa,

Yes kakosea Sasa ndio kila siku mnashinda mitandaoni kumsagia kunguni?

Mmeambiwa kesi ipo polisi inaelekea Mahakamani acheni Mahakama ifanye kazi yake itoe uamuzi ni nani mwenye haki, yaweza ikawa ni script tu km yaliyomkuta yule jamaa alikua sijui Mkuu wa Wilaya sijui Mkuu wa Mkoa huko Shinyanga Bwana Simalenga kuna binti wa kike alimuandama kwamba alimpiga akiwa uwanjani akaweka na bonge la bandeji limefunika jicho km katolewa jicho Dkt. Gwajima D akalivalia njuga suala lile baadae kilichotokea watu wakaumbuka

Na lilipokuja kutolewa bandeji hakuna kupasuliwa jicho hakuna nini ni drama tu kwa hio acheni mihemko tulieni msilalie upande kila upande una haki ya kusikilizwa nyie mmeishia kusikiliza upande mmoja tu na kutoa maamuzi yenu ya ajabu tulieni sikilizeni na upande wa Pili una lipi la kusema, hili sio suala la kukurupukia na kuanza kusema maneno ya ajabu ajabu
 
Nchi hii inahitaji marekebisho makubwa sana ya katiba kuhusu ukiukwaji wa maadili wa viongozi wa umma, hasa eneo la wabunge inapobainika wamevunja maadili ya utumishi wa umma.

Paulina Gekuli alipaswa avuliwe ubunge moja kwa moja, haiwezekani mwakilishi wa mwananchi ndiye mnyanyasaji wa mwananchi, halafu aendelee kuwakilisha wananchi.

Nchi zilizoendelea kwa kitendo hiki Paulina Gekuli alipaswa aondolewe awe raia wa kawaida na mashitaka yafuate.

Tunahitaji marekebisho ya katiba kuhusu eneo hili.
Kuna mdau mmoja aliwahi kusema, "wapinzani ni wabaya kama ccm, ukiwapa madaraka"
Huyu gekul, alikuwa chadema, akaenda ccm, kwa upepo wa Maghu, sasa angalia alichokifanya, akiwa waziri tu!
 
Enough is enough acheni kumsakama Mama wa watu hata km alikosea Sasa imetosha wewe una mabaya mangapi ambayo unayafanya Gizani?

Mnakera sana au mmetumwa kumuandama akisema mnatumia nuksi na kumroga kila uchwao mtakataa yaan ngozi nyeusi hususani watanzania ni bure kabisa,

Yes kakosea Sasa ndio kila siku mnashinda mitandaoni kumsagia kunguni?

Mmeambiwa kesi ipo polisi inaelekea Mahakamani acheni Mahakama ifanye kazi yake itoe uamuzi ni nani mwenye haki, yaweza ikawa ni script tu km yaliyomkuta yule jamaa alikua sijui Mkuu wa Wilaya sijui Mkuu wa Mkoa huko Shinyanga Bwana Simalenga kuna binti wa kike alimuandama kwamba alimpiga akiwa uwanjani akaweka na bonge la bandeji limefunika jicho km katolewa jicho Dkt. Gwajima D akalivalia njuga suala lile baadae kilichotokea watu wakaumbuka

Na lilipokuja kutolewa bandeji hakuna kupasuliwa jicho hakuna nini ni drama tu kwa hio acheni mihemko tulieni msilalie upande kila upande una haki ya kusikilizwa nyie mmeishia kusikiliza upande mmoja tu na kutoa maamuzi yenu ya ajabu tulieni sikilizeni na upande wa Pili una lipi la kusema, hili sio suala la kukurupukia na kuanza kusema maneno ya ajabu ajabu
Ngoja mwanao afanyiwe hivo vitendo nyuma kwakwe af uje urudie haya maneno.
 
Ninajua maumivu anayopitia mzazi Ila kuna vyombo vya dola sio kukaa kusikiliza upande mmoja je upande unaoshutumiwa umesemaje? Achana na Mambo ya script za kuchora na kuchafua watu hata wewe unaweza ukachafuliwa vile vile, leo kwake kesho kwako usiishi kwa kujisahau sana kesho wewe unaweza ukabambikwa kesi ya kulawiti mtoto ambae haujamlawiti na ukasakamwa vile vile
 
Nafikiri kila kitu kipo wazi kikatiba. Ili avuliwe ubunge, kama si wa kuteuliwa ni budi avuliwe uanachama wake kwenye chama kilichomsimamisha ugombea then automatic anakosa sifa ya kuwa mbunge.
Ndo maana tunataka katiba iwe wazi kwa watu wenye tabia kama hii badala ya kusubiri chama cha siasa kumvua uanachama
 
Back
Top Bottom