Huyu ndiyo Bruce Lee

Hata jina Bruce ni la kimarekani.

Mchina anaezaliwa china hawezi pewa jina la bruce.
Bruce Lee ni mchina wa Hong Kong. Hong Kong walitawaliwa muda mrefu na waingereza. Hivyo majina yao yamechanganyika na kizungu. Mfano kama kama Jack(Jack Chen), Donnie(Donnie Yen) n.k

Ijapokuwa si wote ila wengi wao wenye majina ya kizungu na kichina ni wa Hong Kong.
 
Kung fu ni mchezo ambao umechelewa kusambaa ukilinganisha na michezo mingine ya mapigano. Sababu kubwa ndiyo hiyo uliyoitaja wachina waliofanya ni tamaduni yao ni siri yao hivyo haifai kurithishwa kwa mtu yeyote isipokuwa ni China pekee.

Unachosema ni kweli Bruce Lee alikataa hii kitu yeye aliona kung fu ni kama zawadi ya dunia hivyo si vyema kuifungia ibaki kwa wachina pekee yake bali kila mtu ana haki.

Matokeo yake aliingia mgogoro na ma-masta wengi wa kichina. Wengine walikuwa wanasafiri kabisa kutoka China mpaka Marekani kumpa onyo!

Ila Bruce alikuwa kiburi wa namna yake! Aliwaambia ma-masta yeyote atakayenipiga nitaacha kuufundisha huu mchezo!

Kwa bahati mbaya ma-masta walishindwa kumpiga walikuwa wanachezeshewa kichapo wao.

Ila mwamba Bruce Lee kiuhalisia anapiga! Yupo vizuri! Kuna mambo anafanya ya ajabu sana!
Uongo.
 
Bruce alikuwa mmarekani mwenye asili ya china because USA KWAKE NI COUNTRY OF BIRTH NA CHINA NI COUNTRY OF HIS ORIGIN MKE WAKE LINDA LEE NI MZUNGU MWANAE WA KIUME ALIKUFA BRANDON LEE WA THE CROW KWAIYO KABAKI BINTI YAKE NA MKE WAKE TU
Mmh wLiamua kupoteza kizazi chake!
Mtt wa kiume kwann alikufa?
 
Angalieni documentary ya Bruce Lee ipo Netflix. Utaelewa vizuri maisha na falsafa yake jamaa.
 
Sijawahi kuzipenda wala kuzielewa muvi za huyu jamaa

Ni kwel kabx bro ila sabbu wakati anaigiza bado movie zilikuwa Bado low budget quality pia kwa ufupi 1970s movie zilikuwa azina ubora San ila uwezo wa martial arts alikuwa nao mkubwa
 
Bruce Lee aliweka rekodi ya dunia baada ya kupiga 'push up' 200 kwa kutumia vidole viwili vya mkono moja na kurusha punje ya mchele hewani na kuidaka kwa kutumia kijiti chembamba cha kulia chakula (chop stick).

Bruce Lee alizaliwa tarehe 27 november 1940 California, Marekani na alifariki tarehe 20 July 1973 Hong Kong akiwa na miaka 32.

Bruce Lee nguvu ya ngumi yake (punching force) ilikuwa na kilo 158 sawa na Mohammed Ali, lakini maajabu Bruce Lee alikuwa na kilo 58 na Mohammed ali kilo 117.

Bruce Lee alikuwa na uwezo wa kupiga ngumi tisa kwa sekunde moja, na ngumi yake ya inchi moja (one inch punch) ilikuwa na uwezo wa kumrudisha nyuma mita 5-6 mwanaume mwenye kilo 68.

Alikuwa na uwezo wa kupiga mateke tisa kwa sekunde moja, alipiga teke kiroba cha mchanga chenye kilo 135 na kuruka urefu wa futi tano kwenda juu. Alikuwa na uwezo wa kufungua kizibo cha soda kwa kutumia vidole viwili.

Aliweka rekodi ya dunia kwa kupiga 'push up' 1500 kwa mikono miwili bila kupumzika, 'push up' 400 kwa mkono moja, 'push up' 200 kwa kutumia vidole viwili vya mkono moja, na 'push up' 100 kwa kidole gumba cha mkono moja.

Bruce Lee alikuwa mchina wa kwanza kurekodi filamu Hollywood Marekani katika sanaa ya kupigana (martial arts). Bruce Lee pekee ndiye alievunja rekodi ya dunia mara kumi ndani ya miaka 2 tu.




View: https://www.youtube.com/watch?v=HaN8U8vuj-U
 
Back
Top Bottom