Huyu ndiye Padri Privatus Mutekanga Karugendo (1956-2021)

Rest in Peace Mr. Karugendo.

Ukishajua Mungu hayupo na hizi dini ni biashara za watu tu, huwezi kusumbuliwa na hii migogoro.

Yani watu wanakufa kwa UKIMWI, wanashindwa kujizuia kuacha ngono, kanisa linakataza condom!
 
Na Mungu alipowaambia wana wa Israel wakatubu kwa makuhani, alikuwa analeta mfumo wa ajabu?
Usikosoe anachofanya mwenzio, fanya unachoona kinafaa( kwenye masuala ya imani), maana anafuata maandiko
Baada ya Yesu kufa msalabani everything is clear hakuna maombi yanayopokelewa na MUNGU mbinguni pasipo kutumia jina la Yesu christo,tatizo lenu ndg zangu waroma mnamuamini sana Papa na Padri kuliko Yesu anaesamehe dhambi,unaenda kumhadithia Padri dhambi zako eti nimezini na mtu Fulani hui ni ujinga
 
Baada ya Yesu kufa msalabani everything is clear hakuna maombi yanayopokelewa na MUNGU mbinguni pasipo kutumia jina la Yesu christo,tatizo lenu ndg zangu waroma mnamuamini sana Papa na Padri kuliko Yesu anaesamehe dhambi,unaenda kumhadithia Padri dhambi zako eti nimezini na mtu Fulani hui ni ujinga
So hatutakiwi kabisa kufuata Agano la kale?
 
Sijui aliwaza nini huyu aliyekuwa Mtumishi wa Mungu kutumia jina la jinsia nyingine.
Mambo ya utawala tuu, unajua serikali zetu za kina magofool wao walikuwa wanakesha huku kuwakamata wanaoandika ukweli, kwaiyo bila ku hide ID hutokuwa salama na kamata kamata ya mwendesha mashtaka
 
Nilichojifunza hapa ni kwamba, Askofu Niguwemizi roho yake inaendeshwa na shetani himself and yet anavaa joho la Uaskofu.
Ni ajabu kama kwa haraka hivi umeshajifunza, tena kwa kusikia hoja za upande mmoja! Genius!
 
roho yake inaendeshwa na shetani himself and yet anavaa joho la Uaskofu
Ni busara kuhukumu baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili. Tofauti na hapo unadhihirisha jinsi unavyoongozwa na hisia zaidi ya akili.

Pia nimejifunza kwamba Kanisa Katoliki halimtumaini Mungu wa KWELI bali binadamu anayeitwa Papa.
Wakatoliki tunamuamini na kumtumikia Mungu mmoja aliyejidhihirisha kwetu kupitia nafsi tatu:
• Mungu Baba
• Mungu Mwana
• Mungu Roho Mtakatifu

Kanisa Katoliki lina asili kutokea kwa mitume ambao waliongozwa na Petro baada ya kuchaguliwa na Yesu Kristu mwenyewe (Mathayo 16:18). Mtume Petro ndiyo Papa wa kwanza na huyu wa sasa, Francis, ni wa 265.

Papa ni kiongozi wa dunia wa Kanisa lililoanzishwa na Yesu Kristu mwenyewe. Kanisa Katoliki linamtumainia kiongozi wake, lakini hatujawahi kumuabudu wala imani yetu haipo kwa Papa bali Mungu.

Tatu nimegundua kwamba Kanisa Katoliki hujivika joho la demokrasia nchi mbalimbali wakati ndani ya Kanisa hilo hawaitambui
Kanisa Katoliki linaamini katika Theocracy (uongozi wa Kimungu), Mungu ndiyo kiongozi wetu na kila kitu. Tunaamini kiasi fulani katika Demokrasia (uongozi wa mwanadamu) lakini ni ile isiyopingana na mafundisho ya Kimungu.

Nne. Hawa watoto wa mapadri tunaoishi nao mitaani hatima yao ipoje kupitia misimamo ya kipagani ya Kanisa?
Kanisa halijawahi kuwa na misimamo ya kipagani. Unless uthibitishe hizi tuhuma zako.
 
Tangu mwaka 1990 nilipokuwa kidato cha tatu katika Seminari ya Katoke (Biharamulo) hadi leo nimemfahamu Hayati Privatus Mutekanga Karugendo (65) kama mwanateolojia, mwanafalsafa, mchambuzi wa masuala mtambuka, mtafiti, mwandishi, mume na mzazi.

Naandika tanzia hii kuonyesha mafanikio na changamoto zake ninazozifahamu ili viwe somo kwa waombolezaji tuliobaki hai.

Privatus amefariki dunia jioni ya 24 Juni 2021, katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam, kutokana na changamoto ya upumuaji aliyokutana nayo ndani ya masaa 12.

Changamoto hii ilitanguliwa na homa ya siku tatu ikiambatana na kushuka ghafla kwa kiwango cha sukari mwilini. Kwa kuwa hati ya kifo bado haijatoka hatujui chanzo cha changamoto hii. Ameacha mke mmoja, Dk. Rose Katesigwa, na mtoto mmoja, Yesigwe.

Kwa mujibu wa mkewe, Dk. Rose Katesigwa, niliyeongea naye leo, mazishi ya Privatus yatafanyika Jumatatu ya 28 Juni 2021, katika Makaburi ya Kinondoni, Dar es Salaam. Kwa sasa msiba uko nyumbani kwake, eneo la Tabata, Dar es Salaam.

Kuzaliwa

Kwa mujibu wa maandiko yake mwenyewe, Privatus ni mmoja wa watoto wa kiume sita katika familia ya Karugendo. Wengine ni Primus, Pacificus, Pascrates, Princhipius, na Prudence. Tayari Princhipius na Prudence wametangulia katika haki.

Privatus alizaliwa 14 Januari 1956, katika Jimbo la Bukoba. Lakini maisha yake yote ya upadre yamekuwa ni Jimboni Rulenge, kwenye wilaya za Ngara, Biharamulo, Karagwe na Kyerwa.

Elimu ya juu na utumishi wa kikuhani (1975-2000)

Alianza masomo ya seminari kuu mwaka 1975, kupadirishwa, na kufanya kazi ya utumishi wa kutoa huduma za kikanisa hadi mwaka 2000. Hivyo, amekuwa sehemu ya Kanisa Katoliki kwa kipindi cha miaka ipatayo 25.

Alisoma Diploma ya Filosofia katika Seminari ya Ntungamo huko Bukoba (1975-76); na Stashahada ya Teolojia katika Seminari ya Kipalapala huko Tabora (1977-81). Amefanya kazi kama Paroko Msaidizi katika Parokia ya Ntungamo huko Ngara (1982); na kama Mmisionari katika Parokia ya Munchen huko Ujerumani (1982-84).

Alipata Elimu ya Kilimo katika Chuo cha Kilimo Uyole huko Mbeya (1985-87); na kurudi kufanya kazi kama Paroko Msaidizi katika Parokia ya Bushangaro huko Karagwe (1987-97). Pia amehudumu kama Paroko katika Parokia ya Bushangaro huko Karagwe (1998).

Kisha alikwenda kusoma Diploma ya Haki za Binadamu Katika Chuo cha Copenhagen huko Denmark (1999); na kurudi kufanya kazi kama Paroko Msaidizi katika Parokia ya Buziku huko Biharamulo (1999-2000).

Mgogoro wa Privatus na Askofu Niwemugizi

Mwaka 2000 ulizuka mgogoro kati ya Padre Privatus na mkubwa wake wa kazi, Askofu Severine Niwemugizi. Kutokana na mgogoro huu, Privatus alisimamishwa kutoa huduma na kuamuliwa kuondoka jimboni Rulenge na kwenda kuishi nyumbani kwa wazazi wake Bukoba alikozaliwa.

Wakati huo alikuwa ametumikia kanisa kwa miaka ipatayo 20, na wazazi wake wote walishakufa. Pia, mfumo wa utawala wa Kanisa Katoliki haitoi kiinua mgongo kwa padre au sista anayeachishwa kazi. Aidha, hakuna utaratibu wa kuchangia mifuko ya pensheni ya Taifa kwa ajili ya padre au mtawa aliyeachishwa au kuacha kazi.

Hivyo, pamoja na kulitumikia kanisa kwa miaka ipatayo 20, ghafla Privatus alijikuta ni sawa na mwanafunzi aliyemaliza Chuo ambaye hubeba begi lake kurudi nyumbani. Alijikuta njia panda.

Alimua kumwomba rafiki yake mmoja, Askofu Benson Bagonza, wa KKKT Dayosisi ya Karagwe, ampangishie nyumba ya kuishi kwa muda. Akawa anatafakari afanye nini kama njia ya kupata mkate wa kila siku katika mazingira haya mapya. Askofu Bagonza alikubali kumsaidia.

Lakini, baadaye, Privatus aliamua kuondoka Karagwe na kwenda kuishi nje ya Jimbo la Rulenge. Alihamia huko wilaya ya Magu, mkoani Mwanza. Huko alipokelewa kwa ukarimu na Kaya ya Kisukuma, familia ya Mwalimu Mkina. Siku zikasonga mbele akiwa hapo anatafakari jinsi ya kupata mkate wake wa kila siku. Yalikuwa ni majira ya majaribu makubwa kwake.

Wakati akitafakari hayo, Askofu Niwemugizi aliamua kufungua kesi dhidi yake katika mahakama ya Kanisa akimtuhumu kwa makosa kadhaa. Kwa mujibu wa nakala ya barua aliyonionyesha kulikuwepo na tuhuma kama sita hivi. Nakumbuka tuhuma mbili.

Kwanza ni tuhuma ya kuvunja kiapo cha mapdre kuhusu maisha ya useja. Na pili, ni tuhuma kuhusu tabia ya kuhimiza watu kutumia kondomu kama kingamimba na kingamagonjwa kinyume cha mafundisho rasmi ya Kanisa Katoliki.

Kwa mujibu wa sheria za Kanisa Katoliki, Askofu anapofanya maamuzi ya kisheria lazima ashauriane na mwanasheria mwingine mmoja. Niwemugizi aliamua kushauriana na mwanasheria mwenzake, Padre Charles Kitima.

Hatimaye, Askofu Niwemugizi alimtafuta Askofu Mkuu wa Metropolitani ya Kanda ya Ziwa Viktoria na wakakubaliana kuunda Mahakama ya Kanisa ya Kanda (Metropolitan Church Tribunal) iliyojumuisha Majimbo ya Rulenge, Bukoba na Mwanza, yaani hadi Magu alikukuwa anaishi Privatus.

Kwa mujibu wa Sheria za Kanisa, mara nyingi, Mahakama ya Kikanda ni mahakama ya rufaa (second instance court). Kwa mfano, inaweza kutumika kama mahakama ya mwanzo pale jimbo linapokuwa linashitakiwa.

Kwa mujibu wa maelezo ya Privatus, mahakama hii ya Kikanda ilipokea mashitaka dhidi yake kutoka kwa Askofu Niwemugizi wa Jimbo la Rulenge, bila mashtaka hayo kuanzia kwenye Mahakama ya Mwanzo (first instance court) iliyopaswa kuanzishwa jimboni Rulenge .

Hatimaye mahakama ya Kanda ilipokea utetezi wa maandishi kutoka kw Privatusi wenye mapingamizi ya awali yaliyoeleza dosari hizi za kisheria. Lakini bado, mahakama hii iliamua kuendeleza kusikiliza kesi dhidi ya Privatus. Kwa mujibu wa maelezo ya Privatus hakupewa wito wenye hadhi ya kisheria ili aweze kufika na kujitetea katika mahakama hiyo.

Hatimaye, bila yeye kuwepo, mahakama hiyo iliamua kusiliza kesi upande mmoja na kumtia hatiani Privatus. Hukumu hii ilipelekwa kwa Papa. Kwa mujibu wa gazeti la Kiongozi, toleo namba moja la mwaka 2009, Papa Yohanne Paulo II alikubaliana na hukumu hiyo.

Hatimaye Papa alifanya uamuzi wa kumondoa Privatus kutoka katika daraja la upadre tarehe 14 Septemba 2008, kwa kutumia hati ya Kipapa yenye kumbukumbu namba 4182/08. Baadaye kidogo, uongozi wa Kanisa ulipeleka hati ya Papa kwenye televisheni ya Taifa, kuisoma na kuionyesha wazi kwa umma wote.

Mnamo 26 Aprili 2017, miaka tisa baada ya kuvuliwa upadri, Privatus alifunga ndoa na Rose Birusya. Ndoa hiyo ilifungwa katika Kanisa la Mtakatifu Petro, jijini Dar es Salaam, katika misa iliyoongozwa na Padri Stefano Kaombe.

Kusudi aweze kufunga ndoa hiyo ilibidi kwanza aombe kuondolewa katika daraja la upadre. Kwa mujibu wa taratibu za Kanisa mchakato huo huanza baada ya mhusika kuandika barua kwa Papa kupitia kwa Balozi wa Papa.

“Kabla sijaandika barua hiyo, niliambiwa na Paroko kwamba tayari Balozi wa Papa anayo barua ya Padre Privatus aliyemwandikia Papa ili kuomba kibali cha kuoa tangu siku zile nilipoondolewa kwenye rosta ya upadre,” aliwahi kutamka Privatus.

Hivyo, Privatus aliamua kuitumia barua hiyo kukamilisha azima yake ya kufunga ndoa, na paroko alikubaliana naye. Privatus amekufa anaamini kwamba barua hiyo iliandikwa na Askofu Niwemugizi.

Mgogoro huu kati ya Padre Privatus na Askofu Niwemugizi unaweza kueleweka kama ukiwekwa ndani ya mraba unaounganisha Mtaguso wa II wa Laterani (1139), Mtaguso wa Trent (1545-63), Toleo Jipya la Sheria za Kanisa Katoliki (1983), na Waraka wa Papa Paul VI uitwao “Humanae Vitae (1968).”

Mwaka 1139 Papa Innocent II alitunga kanuni iliyopiga marufuku mapadre kufunga ndoa. Mwaka 1563 Papa Pius IV, kupitia Mtaguso wa Trent (1545-63), ulitunga kanuni iliyopiga marufuku walei kupadirishwa. Waraka wa “Humanae Vitae (1968)” ulipiga marufuku matumizi ya kingamimba kama vile kondomu, vidonge na kitanzi.

Na mwaka 1983 Sheria za Kanisa (CIC 290-293) ziliweka utaratibu wa kisheria wa kumwondoa mtu katika daraja la makleri na kumweka katika daraja la walei. Hadi leo kuna ukuta unaotenganisha sakramenti ya makleri (upadirisho) na sakramenti ya walei (ndoa).

Lakini, kwa mujibu wa sheria za Kanisa, ukuta huu una mlango unaofunguka kuelekea upande mmoja wa walei, na hivyo kuwaruhusu makleri kugeuka walei. Lakini bado walei waliofunga ndoa hawaruhusiwi kugeuka makleri.

Privatus alisema na ameandika sana kwamba, ni kweli kwamba aliwahi kuteleza na hivyo kukiuka kiapo cha useja. Lakini aliendelea kusema kwamba tayari alikwisha kutubu, tena kwa Askofu Niwemugizi.

Lakini, “Askofu Niwemugizi alitumia siri zangu alizizipata kupitia zoezi la kuendesha sakramenti ya kitubio kunitia hatiani, jambo ambalo ni kinyume na sheria za kanisa,” alilalamika Privatus kupitia maandiko yake kadhaa. Fungu la 983(1) la sheria za kanisa Katoliki (1983) lahusika.

Kuhusu marufuku dhidi ya matumizi ya kinga mimba, Privatus alikuwa anakosoa kwa hoja fundisho lifuatalo:

“This particular doctrine [that ‘each and every marital act must of necessity retain its intrinsic relationship to the procreation of human life’] … is based on the inseparable connection, … which man on his own initiative may not break, between the unitive significance and the procreative significance which are both inherent to the marriage act.” (Pope Paul VI, 1968: Humanae Vitae, No. 12).

Privatus alipenda kusema kuwa hoja ifuatayo haina ukweli wowote: “the unitive significance and the procreative significance … are both inherent to [every instance of] the marriage act”; thus, “each and every marital act must of necessity retain its intrinsic relationship to the procreation of human life”.

Kwa maoni ya Privatus, hoja hii inachanganya maembe na machungwa, kwa kuanzia kwenye dokezo linaongelea maumbile kwenda kwenye hitimisho linalongelea maadili.

Yaani, ni hoja inayopingana na kanuni ya kimantiki iitwayo “no ought from is principle,” yaani “NOFI principle.” Amekufa akiwa ameushikilia msimamo huu kwa uthabiti.

Kwa mtazamo wake, “contraception is extrinsically evil.” Yaani, uharamu wa kitendo cha kutumia kingamimba unategemea aina ya kingamimba iliyotumika na mazingira husika.

Maisha ya utafiti (2003-2018)

Kwa kipindi cha miaka 20 Privatus amekuwa anatafuta mkate wake wa kila siku kwa fanya kazi kama mtafiti asiyeajiriwa, yaani “daiwaka.” Kupitia utafiti huu ameandika au kushiriki katika uandishi wa ripoti zaidi ya 20, zinazohusu masuala ya kisiasa, kiuchumi na kijamii hapa Tanzania.

Kazi za uandishi na makala

Mbali na kutafiti na kuandaa ripoti za kitafiti, Privatus alikuwa mwandishi wa vitabu na makala zaidi ya 1000 kwa lugha za Kiswahili, Kiingereza na Kijerumani.

Makala za Kijerumani zilichapishwa na gazeti liitwalo “Gemainde Heuite,” la Ujerumani. Makala za Kiswahili zilichapishwa kupitia magazeti ya Rai, Raia Mwema Tanzania Daima, na Uwazi.

Vitabu alivyoandika na kuchapisha ni pamoja na: Maisha yangu Wito wangu; Ubikira; Pambazuko gizani; Maswali 40, majibu 40 ya January Makamba; Maisha yangu Baada ya Miaka 70.

Pia kuna vitabu ambavyo ameandika lakini ameaga dunia kabla havijachapishwa. Vitabu hivyo ni: wasifu wenye jina “Mawazo, Matendo na Matunda ya Askofu Christopher Mwoleka” pamoja na riwaya iitwayo “Sista Kobulongo Maria Mtawa wa Karonga.”

Wakati wa uhai wake, Privatus alinambia kuwa anataka wasifu wa Mwoleka uchapwe na Pius Ngeze, wakati alitaka riwaya ya Mtawa wa karonga ichapwe na Elieshi Lema.

Kazi za ustawi wa jamii

Askofu Niwemugizi
Mbali na kazi za utafiti, Privatus alifanya kazi za kustawisha jamii, akiwa kama mshauri, au mjumbe wa Bodi au mwanachama wa taasisi mbalimbali zipatazo 15.
Taasisi hizo ni pamoja na: Edmin Education Centre; PESENET; SODT; KADENVO; DAC; European Community; USAD; KDCU; TGNP; SNV; HakiElimu, GEMSAT na Mkamilishano.

Hoja zake tutaendelea kuzichunguza sisi tuliobaki hai. Apumzike kwa amani Privatus.
Huyu askofu Askofu Niwemugizi si ndie anajifanya mwanademokrasia ,kutwa yupo mitandaoni na kudai sijui haki kwa Watanzania kumbe yale anayohubiri ni tofauti na yale anayoyatenda, kelele zote ni za kutaka umaarufu tu kumbe anaroho mbaya kama ya paka shume.
 
Huyu askofu Askofu Niwemugizi si ndie anajifanya mwanademokrasia ,kutwa yupo mitandaoni na kudai sijui haki kwa Watanzania kumbe yale anayohubiri ni tofauti na yale anayoyatenda, kelele zote ni za kutaka umaarufu tu kumbe anaroho mbaya kama ya paka shume.
Mkuu, na wewe unahukumu kwa kusikiliza upande mmoja? Hayo ni matumizi ya hisia badala akili.
 
Kwanza, hatupaswi kuhukumu kwa kusikiliza upande mmoja. Kanisa Katoliki lina sheria na taratibu ambalo kwazo linajiongoza.

Padre (Askofu pia ni padre) anapotoa siri za boksi la maungamo anakuwa ananajisi Saramenti Takatifu ya Kitubio na hivyo anakuwa amejitenga (excommunicated) na Kanisa moja kwa moja bila kujali ushawishi wala nguvu zake na Kanisa humuwajibisha bila kumtazama machoni. Nitakupa mfano.

Mnamo mwaka 1534, mfalme wa Uingereza Henry VIII aliinajisi Sakramenti Takatifu ya ndoa na hivyo akajitenga moja kwa moja na Kanisa. Halikujali nguvu au umaarufu wake kama Mfalme wa taifa kubwa la Uingereza.

Kama Kanisa liliweza kumwajibisha mtu mkubwa kama Mfalme Henry VIII; kwanini lishindwe kwa Askofu Niwemugizi?

Note: Tunaungama moja kwa moja kwa Mungu kupitia Padre. Ni sawa na mtu atoke Dodoma kwenda Dar es Salaam moja kwa moja ila atapitia Morogoro.
Huu ulikuwa mwanzo wa kuanzishwa Kanisa la Anglikana (The Anglican Church au The Church Of England).
 
Back
Top Bottom