Huyu ndiye mtoto wa kwanza wa baba wa Taifa Mwalimu Nyerere

inatusaidia nini kuwajua hawa ? je kuwafahamu kwa mtiririko kunamwondoleaje ukali wa maisha mtanzania.so far bado wanatumia rambirambi walizopewa
Ww una wivu wa kike.Usitamani nafasi ambayo c rahis ukaipata maishani mwako na hata katika familia yako

Mwalimu ni marehemu aliyehai,hivyo usitegemee akaacha kuzungumziwa ktk taifa hili mpaka dunia inakwisha,sasa ww usiyeona umhm wa hili bora ukakaa kimya kuwapa nafasi wenye mawazo kwenye thread hii.
 
Watu na matukio,tusiwe wajinga na majuha ,malofa,mwalimu Nyerere hakuwa Mungu wala Nabii,alikuwa binadamu tu kama sisi wooote,ukitaka kutathmini kumbuka maisha yake kabla ya uhuru,yaani alikuwa hana chochote cha kipekee,sasa huu u special unatoka wapi?,na kama alikuwa na makarama au maajabu basi angezuia njaa na maisha magumu yaliojitokeza wakati wa utawala wake.

Kwa hiyo wewe ni wise boy au boya boy?,sasa hao askari wa Uganda ndio walikuhadithia kwamba walipopiga picha Butiama picha yake haikuonekana?,kwa hiyo shida yao ilikuwa picha?,na pia katika vita hao waganda waliona Butiama au picha ya Butiama muhimu ili iweje?,au waliandika hiyo habari kwenya gazeti lako la Uhuru na Mzalendo?,naona aibu kama vile mimi ndie nimeandika umbumbu huo.

Na utaendelea kusikia upupu kila siku,sababu unasikiliza wajinga na malofa.

Wewe Mamdenyi,nilifikiri kuwa ni mtu mwelewa kumbe mbururula.

Kumbe na wewe ni pumba kali.

Mkuu heshima kwako,kama wanajamii forum wote wangekuwa kama wewe,basi leo hii Tanzania ingekuwa kama Japan.
Kumchukia marehemu ni shughuli pevu.
 
Ndugu yangu, mimi si wa ukoo huo, lakini nimekuwa karibu nao kwa sababu napenda sana kuyajua mengi kuhusu ukoo wa Nyerere Burito.
Naomba utueleze zaidi kuhusu watoto wa Chief Burito. Inasemekana Julius Kambarage, Joseph Kisurira na John Kiboko ni watoto wa mama mmoja. Ila baba yao alikuwa na wake wengi. Jee alikuwa na wake wangapi?. Jee ndugu wengine wa Nyerere kwa baba mmoja ni wangapi na wanaitwa kina nani ukiondoa hao ndugu wa tumbo moja wanaotumia majina ya JK Nyerere?.
Chifu Nyerere Burito ambaye ni babake Mwalimu, alikuwa na wake 26. Mamake Mwalimu aliitwa Mgaya Nyang'ombe. Huyu alikuwa mke wa tano. Mwalimu alikuwa na ndugu zengine kwa babake, baadhi yao ni Justine Nyerere, Wisigana, Joseph Muhunda,Jackton, Wanzagi, Mukami, Tagazi, Nyasisenye, Daniel, na wengine wengi sana. Fikiria wanawake 26 si mchezo!!
Mkuu Mwitongo kwanza asante kwa taarifa hii. Taarifa nyingi za maandishi zinataja idadi ya wake wa Chifu Burito ni 22, wewe hii idadi ya wake 26 umeitoa wapi? !.
Pasco
 
Mkuu Mwitongo asante sana, kwa nini wanaotumia jina la Nyerere ni wale watoto wa Mugaya tuu?. Kuhusu Jacton mwanawe, Manyerere alinieleza kuwa ni ukoo huo lakini mpaka leo hakuna data halisi watoto wa baba mmoja na Nyerere ni kina nani?, kuna hoja iliwahi kujengwa kuwa Chifu Edward Wanzangi ni kaka yake, hata Joseph Butiku na Joseph Warioba pia walielezwa hivyo hivyo!. Hili la Baba wa Nyerere kuwa na wake 26 ndio nalisikia kwako leo!, ila samahani nina mashaka na baadhi ya taarifa zako!.

Pasco kuna Museum House pale Butiama ya Mwalimu Nyerere, Ukifika pale Historia yote ipo pale Na Bibi yetu Maria Nyerere kama atakuwa Butiama utapata wasaa wa kuongea nae fanya maandalizi lakini, na sio Mwitongo akuelezee halafu tena humwamini anachokifahamu yeye.
 
Ukimwangalia Mwalimu, ana features za Kitutsi. Light soft skinned, long face, na dental formular ya Wahima!, Jee ni kweli sifa ya nani anakuwa Chifu wa Wazanaki ni yule mwenye ng'ombe wengi?. Jee ni kweli asili halisi ya Chifu Burito ni mtoto wa mchunga ngombe wa Kitutsi alichunga vizuri ng'ombe wa chifu halisi wakazaliana kwa vingi ila ikatokea huyo chifu hakubahatika kupata mtoto wa kiume hivyo akamteua Burito ambaye ni mtoto wa mchunga ng'ombe wake wa Kitutsi aliyezaliwa boma yake, akamtwaa na kumlea kama mwanae na alipofariki, akaukwaa uchifu?. Hali kama hiyo pia imemtokwa rais Kabila wa DRC, imekutikana kumbe sio mtoto wa Kabila bali ni Mtutsi. Museveni pia ni Mtutsi, inasemekana hata Uhuru Kenyatta sio mtoto wa Jomo Kenyatta bali ni damu ya Kitutsi!.

NB- haya ni mapokeo tuu, yaani vitu vinavyosemwa, inawezekana vipo au ni hadithi tuu kama ilivyo kwa Ben, jina la Mkapa ni la kikeni!, kiumeni ni nchumbiji!.
Hima-tutsi Empire
 
mkuu mwitongo
mbona umesepa?

kwa nini J W BUTIKU ambae baba yake wiliam ni mtoto wa nje tu wa mzee burito amekuwa na sauti kubwa katika ukoo huu il hali watoto alowazaa Burito kwa halali kama Muhunda, wesigana, Nyerere wa mugalla, Jacton Nyambereka na wengineo wamefunikwa na hata pale Nyerere Foundation Kajaza wazinzi wenzie tuu
Aisee!
 
Mimi niliwahi kumsikia Nyerere kupitia video yake wakati wa uhai wake, akisema "mama" yake kufariki na miaka takriban mia moja, yeye haoni sababu kwanini asifikishe miaka hiyo.

Nilimshangaa sana kwa kauli hiyo. Baada ya mwaka, nadhani alipokwishagundua kuwa ana ugonjwa wenye chance ndogo sana ya kupona, nilimsikia tena akibadili kauli yake hiyo na kunukuu vifungu vya Biblia vya makumi sita.

Mungu amuweke anapostahiki.
Sheikh Sharif Majini angekuwa hai angempaka mafuta ya BUHURI EL SHAMDI angepona
 
Chifu Nyerere Burito ambaye ni babake Mwalimu, alikuwa na wake 26. Mamake Mwalimu aliitwa Mgaya Nyang'ombe. Huyu alikuwa mke wa tano. Mwalimu alikuwa na ndugu zengine kwa babake, baadhi yao ni Justine Nyerere, Wisigana, Joseph Muhunda,Jackton, Wanzagi, Mukami, Tagazi, Nyasisenye, Daniel, na wengine wengi sana. Fikiria wanawake 26 si mchezo!!
good
 
Kwa kweli watoto wa Mwalimu wapo na kila mmoja ana shughuli zake. Andrew na John wapo Msasani. Emil, Madaraka, Makongoro na Rosemary wapo Butiama. Anna Watiku yupo Tarime. Wana shughuli za kawaida kama watanzania waungwana wengine.

Mwalimu akiwa hai alizuia bonde lote kuanzia pale kwake pasijengwe. Hoja yake ilikuwa kwamba kukibaki na uhalisia wake, kutasaidia kuchuja hewa na kuweka mandhari katika uhalisia wake. Pia aliamini kuwa bonde lile ni mkondo bahari ambao unakuwa na maana sana wakati wa majanga kama ya tsunami na mengine. Pia kulikuwa na viwanja vya ndugu zetu wamakonde kukutana kila wikendi na kuburudika kwa ngoma.

Kuhusu wane wananchi waliokuwa katika kijiji cha butiama-Msasani, wengi waliponzwa na tamaa ya fedha. Mwalimu waliwatetea kwa kuzuia kina KItwana Kondo kuwapoka maeneo yao, lakini kwa njaa zao, baada ya mwalimu kufariki dunia wakauza kwa bei ya kutupa. Wengi wamekufa kwa kihoro, maana wapo waliouza kiwanja hadi kwa sh milioni mbili. Walitapeliwa sana na yule Rwegarisa (Silent Inn) ambaye sasa anajifanya mtu wa Mungu.

Kama kuna swali, lete
Dah asante kwa elimu hii

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rwegasira huyu wanae sema kafulia?
 
Hakuna mtoto wa mwalimu aliyefariki katika ajali ya ndege wakati wa vita. Andrew alikuwa Fighter pilot kama alivyokuwa mdogo wake, John. Makongoro alikuwa mtaalamu wa mizinga. Wakati wa vita Makongoro alipigana mstari wa mbele. Kwa kifupi niseme hakuna mtoto wa mwalimu aliyekwishafariki, iwe vitani au kwa namna nyingine. Wote wakingali hai. Mwalimu alikuwa mvuta sigara, na aliacha baada ya Uhuru. Hakuna kumbukumbu za yeye kuvuta siga kubwa! Kuhusu hilo la katiba ya Tanu ni kweli, lakini aliandika katika pango kule Ikizu.

Nawasilisha
Kwa taarifa hii, naona kama watoto wa Nyerere hawajatendewa haki katika Taifa hili kwa uzalendo wa baba yao na wao wenyewe kwa Taifa letu. Viongozi wa Sasa sidhani kama wanaweza kupeleka watoto wao, yaani familia nzima vitani Frontline. Walitakiwa kupewa heshima na nafasi kubwa za upendeleo katika uongozi wa Taifa. Tunasikia baadhi ni wamekuwa walevi, pengine ni frustration za vita na kutengwa.
 
Ndugu zangu,

Nimeona mjadala mkali unaomhusu Andrew Nyerere. Wapo wanaomkejeli kwa jina lake, na wengine wanamzushia tu mambo.

Nimeona nieleze haya machache...

Andrew Nyerere ndiye first born wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Burito. Jina lake la kuzaliwa ni Burito.

Burito ni babu yake Mwalimu Julius Nyerere.

Andrew ana wadogo zake. Mtiririko wao wa kuzaliwa ni Anna Watiku, Emil Magige, John-Guido Nyerere, Charles Makongoro, Godfrey Madaraka, Rosemary na Pauleta.

Nimeona nitoe elimu hii fupi nikiamini kuwa katika JF suala la kuelimishana limepewa umuhimu mkubwa.

Kama lipo swali, nawakaribisha.

Asanteni sana.
Nini kimetokea hata Andrew aanze kutajwa SASA?
 
Ndugu yangu, mimi si wa ukoo huo, lakini nimekuwa karibu nao kwa sababu napenda sana kuyajua mengi kuhusu ukoo wa Nyerere Burito.
Good: nitonye kwanini familia ya Nyerere haijaonekana kwenye shughuli ya Lupaso
 
Mwalimu kaacha taifa maskini duniani licha ya uwepo wake wa miaka 24 kwenye uongozi. Yakamshinda akang'atuka. Alipokabidhiwa hii nchi ilikuwa ya kwanza katika Afrika kusafirisha bidhaa za kilimo katika Afrika, alipong'atuka kaiacha ni maskini wa mwisho duniani.
Ila ameacha Nchi yenye amani kubwa na kuongea lugha moja . Duniani kote. Hao matajili hawana amani
 
Kwa kweli watoto wa Mwalimu wapo na kila mmoja ana shughuli zake. Andrew na John wapo Msasani. Emil, Madaraka, Makongoro na Rosemary wapo Butiama. Anna Watiku yupo Tarime. Wana shughuli za kawaida kama watanzania waungwana wengine.

Mwalimu akiwa hai alizuia bonde lote kuanzia pale kwake pasijengwe. Hoja yake ilikuwa kwamba kukibaki na uhalisia wake, kutasaidia kuchuja hewa na kuweka mandhari katika uhalisia wake. Pia aliamini kuwa bonde lile ni mkondo bahari ambao unakuwa na maana sana wakati wa majanga kama ya tsunami na mengine. Pia kulikuwa na viwanja vya ndugu zetu wamakonde kukutana kila wikendi na kuburudika kwa ngoma.

Kuhusu wane wananchi waliokuwa katika kijiji cha butiama-Msasani, wengi waliponzwa na tamaa ya fedha. Mwalimu waliwatetea kwa kuzuia kina KItwana Kondo kuwapoka maeneo yao, lakini kwa njaa zao, baada ya mwalimu kufariki dunia wakauza kwa bei ya kutupa. Wengi wamekufa kwa kihoro, maana wapo waliouza kiwanja hadi kwa sh milioni mbili. Walitapeliwa sana na yule Rwegarisa (Silent Inn) ambaye sasa anajifanya mtu wa Mungu.

Kama kuna swali, lete
Dah
 
Back
Top Bottom