Huyu mwanangu wa ujanani nimfanye nini ili awe kama wenzie?

mulwanaka

JF-Expert Member
Feb 19, 2017
5,262
12,837
Ndgu zanguni habari za jmosi, nina first born wangu nilio zaa wakati wa ujana wangu na mwana chuo mwenzangu.

Ndoa ilishindikana tukaamua kulea mtoto wetu, mtoto amekaa na mama ake hadi 8yrs nilimchukua na kuanza kumlea mwenyewe paka sasa ana 16yrs.

Mtoto wangu nampenda sana ila amekua tofauti na wadogo zake, ana tabia mbaya ya udokozi nyumbani na tabia ya wizi inaanza kukua.

Kwa kweli ina tukera kama familia, aliuza CPU zote nyumbani na pia kachukua laptop yangu kaiuza, kachukua simu ya mama ake mlezi nk, hi tabia yake imekua sugu ni metumia psychological approach ya kuwa karibu naye na kumshauri kumpa pocket money ya kutosha ila naona imeshindikana.

Alipofika form two nilimpeleka shule ya mbali kijijini ili aweze kufikilia na kuacha hiyo tabia, nilidhani amebadilika alivo ingia f4 sasa jana mama ake amempa atm card atoe pesa amlipie ada yake ya shule na mahitaji ya shule mpya, kampiga pesa katoa 50k zaidi ambao hakumwabia hivi vi pesa vidogo

Jamani huyu mtoto atakuja kubadilika au ndo hivo kasha kuwa mwizi wa kudumu? Ushauri tafadhari
 
Duh pole sana..
Ngoja waje wazoefu, ila tabia ikiendelea ataanza kuwaibia watu wengine, huko watampiga watamuua.

Kipindi nakua mtaani kwetu kulikuwa na mtoto wa jiran ana tabia kama za mwanao, cha ajabu kwao walikuwa wanajiweza ila mtoto kutwa ni wizi tena mpka kwa majirani. Sasa sijui huwa ni tabia au tamaa tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ongea na maaskari wamlaze ndani siku tatu hiyo Sero iwe ni chafu sana na ina watu vichwa ngumu.Mtegee alfu 50 ingine aibe afu mtie ndani.

Sent from my SM-G920F using JamiiForums mobile app
Lockup itamfanya awe sugu zaidi, kuna kipindi aligoma kuenda shule paka apewa pocket money 70k tukaleta sungusungu mgambo ili amtishe wala hakushituka aliendelea na msimamo wake......
 
Dah pole mkuu Kuna watoto ni changamoto, umejaribu kukaa nae kumuuliza kwa nini anaiba?? Labda Kuna mambo anafanya huko nje yanayohitaji pesa ndio maana anaiba jaribu kumchunguza na marafiki anaoshirikiana nao pia maana makundi mabaya nayo yanachangia.Kingine huwa unafanyaje ukimkamata ameiba?? Mimi mdogo wangu wa kiume alikua na hiyo tabia tulivyochunguza tukagundua anaiba hela anaenda kucheza pool table fimbo zilitembea Sana mpaka akaacha wizi na alikua mdogo Sana just 10yrs,wewe simama Kama baba muulize hela huwa anapeleka wapi mcharaze mikanda hapo mpaka aseme ukweli na mwambie asiposema unampeleka polisi wakamshughulikie, maana akizoea ipo siku ataiba huko nje na jamii haitamuacha salama.Pole Sana malezi Karne hii ni magumu sana
 
Kweli mkuu nilishamchapa kwelikweli alivo iba laptop yangu nimeshampiga mara nyingi ila mtokeo bado na ni mkimya sana
 
Duh pole sana..
Ngoja waje wazoefu, ila tabia ikiendelea ataanza kuwaibia watu wengine, huko watampiga watamuua.

Kipindi nakua mtaani kwetu kulikuwa na mtoto wa jiran ana tabia kama za mwanao, cha ajabu kwao walikuwa wanajiweza ila mtoto kutwa ni wizi tena mpka kwa majirani. Sasa sijui huwa ni tabia au tamaa tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Tabia ni km ngozi.Huoni mtu unaweza kuwa na mke tena mzuri tu,lkn kwasababu ya Ukiboro dinda,unajikuta unatoka nje ya Ndoa.
 
Kweli mkuu nilishamchapa kwelikweli alivo iba laptop yangu nimeshampiga mara nyingi ila mtokeo bado na ni mkimya sana
Basi jaribu na upande wa saikolojia labda Kuna vitu anapitia anashindwa kukuambia wewe moja kwa moja akipata mtaalamu mzuri wa saikolojia ya watoto anaweza kuongea nae mkajua nini shida, na mama yake anasemaje?? Labda amemshirikisha mama mzazi.
 
Lockup itamfanya awe sugu zaidi, kuna kipindi aligoma kuenda shule paka apewa pocket money 70k tukaleta sungusungu mgambo ili amtishe wala hakushituka aliendelea na msimamo wake......
Ameshawasoma ameona nyie Wazazi wake ni mdebwedo tu,huyo inatakiwa anapewa stiki za maana na zoezi la kufa mtu, hiyo siku lazima ajinyee, Mbona atanyooka tu.Sema mmechelewa kwasababu miaka 16,inachanganyikana tabia zake mbovu na Adolescence,lkn bado haujachelewa, mkabidhi kwa makamanda wamtikite kisawasawa atajuta kuzaliwa.
 
Vumilia miaka miwili atakuwa 18. Mtimue home akahangaikie huko akafunzwe na ulimwengu. Trust me pyscholohical approach does not work to african kids. Viboko vingesaidia sana kumnyoosha
Tatizo mtoto kulelewa na Mama pekee kuna vitu ame vikosa kutoka kwa Baba kwenye makuzi yake tatizo single mother malez ya mtoto wanacho jua ni kununua nguo Kula vizur bas hawajui kuna Malez ya Baba Yana takiwa wenyewe wanacho taka Baba utume hela tu
 
Back
Top Bottom