Huyu Muhishimiwa Dkt. Mohammed Gharib Bilal anacho fanya ni sahihi?

Bob_Dash

Member
Nov 1, 2010
90
13
​Nimefuatilia sana safari za huyu Muhishimiwa Makamu wa kwanza wa Rais Dr. Mohammed Gharib Bilal anapokuwa kwenye safari za kikazi hapa nchini ama nchi za nje kila wakati lazima aambatane na eitha mke ama wake zake wote, ninajua wazi lazima gharama zote zitakuwa zinagharimiwa na kodi za wananchi, je hii ni sahihi? kuna ulazima gani kuambatana na wake zake kila mahala anapokuwa kazini? mbona hata viongozi wa mataifa tajiri huwa hawafanyi hivi, hii kitu huwa inanikera sana, mara nyingi kila ukiona picha za huyo muhishimiwa lazima utaona na picha za mke ama wake zake wote pia, narudia kuuliza, HII NI SAHIHI WAUNGWANA?
 
mke anaetambulika kiserikali ni mmoja so gharama za mke mwingine ni juu yake maana hajawekewa fungu, hata hivyo mimi sioni ubaya yeye kuambatana na wake zake ilimradi tu atimize wajibu wake kwa serikali na kwa wananchi
 
he he he wazee wa siku hizi engine moto,bora huyo anasafiri na wake kuliko wale wanaotembea na madada zetu wa vyuoni
 
mke anaetambulika kiserikali ni mmoja so gharama za mke mwingine ni juu yake maana hajawekewa fungu, hata hivyo mimi sioni ubaya yeye kuambatana na wake zake ilimradi tu atimize wajibu wake kwa serikali na kwa wananchi

Lakini hata hivyo, kuna ulazima gani kila safari lazima aambane na mke wake? mbona hatuoni viongozi wengine wakifanya hivyo?
 
​Nimefuatilia sana safari za huyu Muhishimiwa Makamu wa kwanza wa Rais Dr. Mohammed Gharib Bilal anapokuwa kwenye safari za kikazi hapa nchini ama nchi za nje kila wakati lazima aambatane na eitha mke ama wake zake wote, ninajua wazi lazima gharama zote zitakuwa zinagharimiwa na kodi za wananchi, je hii ni sahihi? kuna ulazima gani kuambatana na wake zake kila mahala anapokuwa kazini? mbona hata viongozi wa mataifa tajiri huwa hawafanyi hivi, hii kitu huwa inanikera sana, mara nyingi kila ukiona picha za huyo muhishimiwa lazima utaona na picha za mke ama wake zake wote pia, narudia kuuliza, HII NI SAHIHI WAUNGWANA?

Shhiiiiiiiiiiiii !!! usiwaamshe wadanganyika, zanzibar ni nchi inayotoa maexpert wa urais tanganyika
 
Ahhh yaani mzee huyu mimi ananiboa sana hana kazi yoyote kutwa kuzunguka na wake zake akifungua shule za kata na upuuzi wowote...na huko kote kazi kuwaweka mbele wake zake aaahh kiongozi gani wa hovyo hivi..nafikiri kwenye mapendekezo ya katiba hiki cheo kifutwe hakina tija kwa mtanzania ni ulaji tuu wa pesa za walipa kodi.
 
Labda tatizo lipo kwa hao wake zake hawaaminiani kila mmoja anataka kukaba penati
 
Lakini hata hivyo, kuna ulazima gani kila safari lazima aambane na mke wake? mbona hatuoni viongozi wengine wakifanya hivyo?
Anaogopa mitihani ya duniaaaa.Bora yeye kuliko kuwaacha nyumbani halafu alale na vimada. Wahudumu mzee kajadhatiti wafateni haohao!!!!!!!!!
 
Ahhh yaani mzee huyu mimi ananiboa sana hana kazi yoyote kutwa kuzunguka na wake zake akifungua shule za kata na upuuzi wowote...na huko kote kazi kuwaweka mbele wake zake aaahh kiongozi gani wa hovyo hivi..nafikiri kwenye mapendekezo ya katiba hiki cheo kifutwe hakina tija kwa mtanzania ni ulaji tuu wa pesa za walipa kodi.
Acha chuki binafsi. Kaacheni kazee ka watu kale nchi. Kwani nchi nafasi gani inaumuhimu wote wizi mtupu.
 
Dah!nafuatilia hili maana kama mtu anakuwa na wake wanne na wote ndan ya msafara mbona hatufiki mbali,mi nadhani huu umasikini unasabishwa na mambo ya kipuuz puuz tu.mke au wake kila pahala hyo haifai.nadhan mke mmoja siyo mbaya na hasa kwa safari ya siku 3 nakuendelea vngnevyo ni ufujaji wa mali ya wavuja jasho.
 
Jamani ebu wacheni donge roho mbaya na choyo,asingee wachukua hata mmoja mngesema kawachukua mnasema,
Mbona hamuwasemi wanao kula pesa za EPA mnamsema babu wawatu, mwacheni ale raha na wakezake hamjui anapenini mpaka akawachukua wote kila mmoja anasifa zake,au unataka amuwache kwako mmoja akirudi safari ampitie..
 
Nimefuatilia sana safari za huyu Muhishimiwa Makamu wa kwanza wa Rais Dr. Mohammed Gharib Bilal anapokuwa kwenye safari za kikazi hapa nchini ama nchi za nje kila wakati lazima aambatane na eitha mke ama wake zake wote, ninajua wazi lazima gharama zote zitakuwa zinagharimiwa na kodi za wananchi, je hii ni sahihi? kuna ulazima gani kuambatana na wake zake kila mahala anapokuwa kazini? mbona hata viongozi wa mataifa tajiri huwa hawafanyi hivi, hii kitu huwa inanikera sana, mara nyingi kila ukiona picha za huyo muhishimiwa lazima utaona na picha za mke ama wake zake wote pia, narudia kuuliza, HII NI SAHIHI WAUNGWANA?

Mkuu usikurupuke tu kuandika thread bila kwanza kufanya utafiti, kwanza umeipata wapi hiyo kuwa gharama zote zinalipwa na serikali una uhakika?

Serikali inamtambua mke mmoja tu ndio inagharamia, halafu umetoa mfano mbona mataifa makubwa viongozi wake hawafanyi hivyo.

Jacobo Zuma, Rais wa Afrika Kusini wakati mwingine anatembea na wake zake wote wanne. Na hakuna tatizo
 
Wewe una undugu naye nini? kwangu mimi naona huo ni upuuzi tu, umetolea mfano Jacob Zuma, siyo kweli kila safari zake anaonekana kuambatana na hao wake zake bana, mimi sina tatizo kwamba ana wake wangapi, ila nataka kufahamu kunaulazima gani unapokuwa katika safari za kikazi kila mara kuongozana na mkewe? huo ni mzigo usio wa lazima kwa Serikali. download (46).jpg
Si mnaona wenyewe hapo? hiyo ilikuwa safari ya siku kadhaa mkoani Tanga na kabla ya hapo alikuwa Lindi pia na hizo "MBAVU ZAKE"
 
Ulitaka akuchukue wewe, utamsaidia shughuli za usiku??

Acha kufikiri matope

Nachojiuliza mimi ni hivi, huo usiku ukifika, analala na yupi?

Mambo haya nilifikiri ni ya kibada tu, kumbe na watu na elimu zao bado wanaishi kama jogoo!

Haya bwana mtaalam, niambie usiku inakuwa vipi, anawaweka vyumba vitatu tofauti hlf analala kwa zamu au anawarundika kwa pamoja? (Watumishi wa hotel wanajionea mambo makoridoni bila shaka)
 
Back
Top Bottom