Huyu mama atakuwa ananitaka ki-mapenzi au shida yake nini?

ushauri wangu ni huu ufuatao:
1. piga hesabu pesa zote alizowahi kukupa tangu uvamiwe na majambawazi uwe nazo tayari akizihitaji pindi utakapo kataa usiliwe kiboga na mumewe.
au
2. ukubali kula na kuliwa....
3. mke wa mtu sumu, uache hayo mazoea ya kupokea zawadi...
Mkuu nashukuru kwa ushauri wako,lkn hana mume. Mume alifariki mwaka 2010 kwa ajali.
 
Usipende kupokea cos one day lazima utoe chochote na wewe
Una ndoa kuwa na tabia njema linda ndoa yako

Huyo anakutaka kataa pesa zake na mazoea yake
Michepuko sio dili.mpende mkeo
Ushauri wako nauzingatia kiongozi.
 
Nenda naye taratibu tu kiongozi mpaka uuone mwisho wake.
Tena kwa kuwa ni mjane I thought ni mke wa mtu.
 
unashindwa kumuuliza zawadi kwa misingi ipi?afteral laki 7 kwa wengine ni hela ndogo sikatai ila think big.

HIV is very easily transmitted
 
hivi visa ni ving kumbe mjini hapa. Hv wamama mnatutakia nin vijana si mtuache tule ujana na vijana wenzetu?
 
Ulisham-entertain tangu mwanzo kaka,mtu wa jinsia tofaut na yako anapofanya vitu ambavyo hata ww huvielewi na huna mazoea nae..unatakiwa kumpiga stop hapo hapo. Kwanini akuzidishie fedha tena mara kwa mara na wakat mwingine anakupa tu fedha...?? Kuna jambo....nothing goes go for free indeed....!! Ila nina imani ushamuelewa sema tu hutaki kukubali ukweli.
 
Usipokee kitu hujui kusudio lake, na pia hakuna kitu cha bure duniani. Usipokee, au tunza hizo pesa kisha uje umrudishie (ingawa ni ngumu ila huna jinsi) Pia kitu cha busara ni wewe kukaa nae na kumuuliza ni kwa nini anafanya hivyo! Kama wadai hana mme, basi mueleze kuwa wewe una mke na usingependa kuiingiza ndoa yenu matatizoni. Pia natumai wajua mme wake alifariki kwa chanzo gani.
 
Nakushauri hiyo 200,000 + 700,000 = 900,000 umrudishie kwa utaratibu huohuo uliozipokea. Itakuepusha na mengi. Dunia ishaharibika hii!
 
Hivi hapa mwenye shida ni huyo mwanamke au wewe unayepokea hela zake!!!

Hivi angekuwa anakuletea kinyesi kwenye bahasha ungekipokea wewe?

Ila kwa kuwa ni fedha basi umezipokea na kibindoni umezitia halafu waanza kubwata kuwa hujua dhamira yake.

Watu wengine banaa hamnazo kabisa
 
Sasa unataka nikushauri nn wakat mmeshafikia hatua yakuambiana umri wenu?ila poa acha tu nikushauri kuwa inabidi uridhike na unachokipata hapo ofisin kwako,so akikupa pesa usizipokee coz hatima yake ni mbaya kwa ndoa yako lol!.
Ndugu wana-MMU! Naombeni msaada,me npo wilaya temeke hapa Dar,biashara yangu ni M-PESA,Tigopesa na Airtelmoney. Kuna mmama ni Mteja wangu sana toka nilipofungua hapa mwaka 2011. Lkn kuna matendo sielewi dhamira yake ni nini! Ilianza mwaka Jana nilivamiwa hapa na majambazi yenye silaha na kufanikiwa kunipora kiasi kidogo cha pesa na simu zangu zote.

Usiku uleule nikiwa police natoa Maelezo nae alikuwepo. Hakufanya chochote(nadhani kwa vile nilikuwa na mke wangu). Kesho yake asubuhi wakati naondoka kwenda mjini kushughulikia kurudisha simcard zangu nilimkuta stendi nae akisubiri gari,tulijikuta gari moja na siti moja.

Tuliongea mengi juu ya kuibiwa kwangu,alinilipia nauli na wakati tunataka kushuka kariakoo,akanishikisha noti nyekundu ambazo sikujua idadi yake wakati huo na kuniambia hiyo pole yangu.Nilipokuja kuzihesabu zilikuwa laki 2. Nilishangaaa saana!

Toka wakati huo nimekuwa nikipata zawadi za fedha mara nyingi bila kumuomba. Leo amenipigia simu akaniambia km Nina Salio kwenye tigopesa nimuwekee kwenye simu yake laki 5 then anatuma mtoto aniletee,kwa vile nilikuwa na salio nikamuwekea,muda mfupi baadae kaja binti yake kuniletea,amenipa zikiwa kwenye bahasha nimefungua nizihesabu nimezikuta zipo milioni moja na laki 2.

Nilipompigia simu kumwambia zimezidi,akaniambia ameamua kunipa hizi laki 7 km zawadi yangu. Bado sijaelewa dhamira ya huyu mama,ni mama mwenye miaka km 42 hv,ana nizidi km miaka 10,hajawahi kunitamkia chochote zaidi ya kuniachia hela kila akija kutoa hela hapa.

Hebu nipeni ushauri ana nia gani huyu mama!? Maana anajua me nna make tena mzuri tu. Ushauri Tafadhali.
 
Kuna mmama mmoja namfahamu ni muathirika na mumewe pia alikuwa ni muathirika walikuwa wanaishi temeke ila nakumbuka mumewe alikufa kwa ajili pia!chunga usije ukafanya watoto walaumu kama baba angekuwepo tusingekuwa ivi!


Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom