Huyu bwana anafanya dawa zake kwenye kiwanja changu ikiwemo kuwaogeshea dawa wateja zake

Unforgettable

JF-Expert Member
Aug 1, 2019
5,277
11,775
Habarini za asubuhi wakuu,

Napata ukakasi wa nini chakufanya linapokuja kwenye swala hili,kwenye harakati za maisha nimebahatika kuwa na kiwanja changu maeneo flani hivi hapa dar,umepita mda kidogo sijakiendeleza zaidi ya kwenda kukifanyia usafi tu jirani yangu tuliekua tumepakana akaamua kuuza kipande chake na alienunua ni mganga wa kienyeji.

Sasa suala langu linakuja hapa huyu bwana anafanya dawa zake kwenye kiwanja changu ikiwemo kuwaogeshea dawa wateja zake na kurusha/kuvunja mavitu nisiyoyaelewa kwenye kiwanja changu, majirani zangu wananiambia hata mbuzi/kuku huchinjiwa hapo kusema kweli hili limeniogopesha ukitegemea me na haya mambo ni mbalimbali sasa nikaamua kukiuza kiwanja cha ajabu ni mteja napata anakuja mpaka kwenye kiwanja kukiona na tunakubaliana kabisa bei ila siku tunayopanga kuja kulipana mteja hatokei na hili limenitokea kwa mteja zaidi ya wanne ndomana nimeshtuka kuwa hiki si kitu cha kawaida..

Je, nifanyeje?
View attachment 2794250
 
Ushasema wewe na hayo mambo mbali mbali sasa kwann yanakukosexha amani,? Imani yako umeielekeza wap huko ambako hakuna msaada!?
 
Mfate yeye mwenyewe mwambie akutafutie mteja unataka kukiuza kwa changamoto kadhaa zinazokukabili, anaweza akanunua au akawaambia wateja zake, unavyozidi kujiweka mbali nae ndio unajikosesha amani mwenyewe usikute yeye hana hili wala lile juu yako.
Fuata wazo la mkuu, pengine huwa anamuona akija bila hata salamu akaona ngoja akuoneshe umwamba
 
Mfate yeye mwenyewe mwambie akutafutie mteja unataka kukiuza kwa changamoto kadhaa zinazokukabili, anaweza akanunua au akawaambia wateja zake, unavyozidi kujiweka mbali nae ndio unajikosesha amani mwenyewe usikute yeye hana hili wala lile juu yako.
Shida sio kua na hili wa lile juu yangu,kinachonikwaza ni mwanini afanyie dawa zake kwenye eneo langu
 
Ushasema wewe na hayo mambo mbali mbali sasa kwann yanakukosexha amani,? Imani yako umeielekeza wap huko ambako hakuna msaada!?
Unapoenda kwenye eneo lako ukakuta vyungu na madawadawa vinakukosesha amani,naogopa hata kukanyaga kwenye kiwanja
 
Habarini za asubuhi wakuu,

Napata ukakasi wa nini chakufanya linapokuja kwenye swala hili,kwenye harakati za maisha nimebahatika kuwa na kiwanja changu maeneo flani hivi hapa dar,umepita mda kidogo sijakiendeleza zaidi ya kwenda kukifanyia usafi tu jirani yangu tuliekua tumepakana akaamua kuuza kipande chake na alienunua ni mganga wa kienyeji.

Sasa suala langu linakuja hapa huyu bwana anafanya dawa zake kwenye kiwanja changu ikiwemo kuwaogeshea dawa wateja zake na kurusha/kuvunja mavitu nisiyoyaelewa kwenye kiwanja changu, majirani zangu wananiambia hata mbuzi/kuku huchinjiwa hapo kusema kweli hili limeniogopesha ukitegemea me na haya mambo ni mbalimbali sasa nikaamua kukiuza kiwanja cha ajabu ni mteja napata anakuja mpaka kwenye kiwanja kukiona na tunakubaliana kabisa bei ila siku tunayopanga kuja kulipana mteja hatokei na hili limenitokea kwa mteja zaidi ya wanne ndomana nimeshtuka kuwa hiki si kitu cha kawaida..

Je, nifanyeje?
Kiendeleze kwa ukuta, (fence)
 
Back
Top Bottom