Huyu anaishi Tanzania ipi?

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,015
Posted Date::10/9/2007
Waziri ashangazwa miundombinu finyu Lindi
Na Said Hassani, Lindi
Mwananchi

NAIBU WAZIRI wa Kilimo Chakula na Ushirika, Dk David Mathayo, ameshangazwa na miundo mbinu finyu katika Wilaya ya Liwale mkoani Lindi.

Hatua hiyo imekuja baada ya kubaini kuwa, miundombinu hiyo, imesababisha kukosekana usafiri wa uhakika kutoka katika wilaya hiyo kwenda wilaya jirani za Nachingwea na Kilwa.

Liwale ni miongoni mwa wilaya zilizopo pembezoni mwa nchi, ambayo inahitaji juhudi za makusudi katika kusaidia wakazi wake kuondokana na umasikini wa kipato.

Mapema akifafanua bajeti ya serikai kwa mwaka 2007/08, Dk Mathayo alisema kuwa wilaya hiyo imepewa Sh2bilioni kati ya Sh40.5bilioni zilizotengwa kwa Mkoa wa Lindi kwa maendeleo.

vipaumbele vikiwa vimeelekezwa katika miradi ya maendeleo, kama vile elimu, afya, kilimo, maji na miundombinu.

"Serikali imetenga kiasi kikubwa kama hicho katika miradi ya maendeleo, ikiwa ni moja ya njia ya kupunguza bajeti tegemezi kutoka kwa wahisani," alisema Dk Mathayo wakati akizungumza na watumishi wa taasisi za umma, katika Ukumbi wa Rainer uliopo mjini Liwale.

Aliwagiza Mkuu wa Wilaya hiyo, Anna Magowa kumwajibisha mtendaji atakavuruga juhudi za serikali kuwapelekea wananchi wake, maendeleo.
 
Aliwagiza Mkuu wa Wilaya hiyo, Anna Magowa kumwajibisha mtendaji atakavuruga juhudi za serikali kuwapelekea wananchi wake, maendeleo.

Tutafika kwa hii spidi.???
 
Back
Top Bottom