Tafakari_nami
JF-Expert Member
- Nov 4, 2016
- 783
- 1,551
Habarini wapendwa, bila kupoteza muda, naomba niende kwenye mada moja kwa moja. Mwaka jana mwezi wa 2, nilienda hospitali ya Regency sababu nilikuwa nina sumbuliwa sana na tumbo. Niliishiwa nguvu, mikono na miguu kufa ganzi, kuhisi kiwewe au kuchanganyikiwa, kichefuchefu, kuchoka sana, na kuhisi kutapika. Nilipima vipimo vingi, ikiwa ni pamoja na typhoid, malaria, H. pylori, lakini majibu yakatoka hasi. Hata hivyo, kipimo cha endoscopy kilionyesha kuwa nina Gastritis.
Tangu hapo, mpaka leo hii, sasa inakwenda mwaka mmoja tangu niende Regency Hospital, bado nina sumbuliwa sana na ugonjwa wa Gastritis. Walinipa dawa aina ya kupunguza acid au antacid, kama vile Pantonex 40mg, box 3 nitumie kwa miezi 3 mfululizo, na dawa nyingine kama maziwa, kama Relcer Gel.
Dawa hizi zinatuliza maumivu, lakini hazijaweza kumaliza tatizo kabisa mpaka sasa. Naomba msaada wenu ikiwa kuna dawa nyingine naweza kutumia kumaliza kabisa shida hii.
Kuhusu vyakula, nina jitahidi sana kutokula vyakula vyenye acid. Chakula changu kikubwa ni ugali mlenda au mchicha, na wali pia nakula japo mara moja moja.
Ninaomba pia kujua kutoka kwa wale ambao waliwahi kuugua ugonjwa huu na kupona, walitumia dawa gani au njia gani mpaka kupona. Nashindwa hata kutoka kutafuta kipato maana tumbo lauma sana, mithili ya kukwangua ndani tumboni. Siwezi lala kwa tumbo maana nikifanya hivyo ni kama nachokoza tumbo, nitashikwa na kuzunguzungu sana, na mikono na miguu kufa ganzi, pamoja na maumivu ya tumbo lenyewe.
Tafadhali, naombeni msaada ndugu zangu ili nami nipone. Ninapoandika haya, nahisi kutaka kulia, maana maumivu siyo poa, na ni kila siku.
Asanteni kwa kusoma ujumbe wangu.