Huu ni wizi wa mchana wa Fire

Edmond

JF-Expert Member
Oct 7, 2010
359
54
Ndugu wana jamii,
Juzi nilienda kulipia road licence ya gari langu, cha kushangaza nikaambiwa nilipie na fire extinguisher Tzs 35,000 cha ajabu nilipatiwa sticker pasipo kuwa na mtungi, kwanza mtungi wa fire ninao, na sidhani sticker pekee ni Tzs 35,000, je huu sio wa mchana?, kwanini serikali yetu inazidi kutulundikia mzigo mkubwa wananchi wake?, na je hii dhana ya maisha bora kwa kila mtanzania itafanikiwa kweli kwa mwendo huu?,

Wana bodi naomba kuwakilisha,
 
Ndugu wana jamii,
Juzi nilienda kulipia road licence ya gari langu, cha kushangaza nikaambiwa nilipie na fire extinguisher Tzs 35,000 cha ajabu nilipatiwa sticker pasipo kuwa na mtungi, kwanza mtungi wa fire ninao, na sidhani sticker pekee ni Tzs 35,000, je huu sio wa mchana?, kwanini serikali yetu inazidi kutulundikia mzigo mkubwa wananchi wake?, na je hii dhana ya maisha bora kwa kila mtanzania itafanikiwa kweli kwa mwendo huu?,

Wana bodi naomba kuwakilisha,

Kwa muda mrefu serikali imeendeshwa kwa
1. Pombe
2. Sigara
3. Kodi za wafanyakazi

Sasa mambo yamezidi kuwa magumu wanataka mteremko mwingine. Ndo akili ya Magamba ilipoishia.
 
Wana JF habari za mihangaiko na wenzangu poleni kwa mfungo,
Kuna taarifa ambayo ilitolewa na imetangazwa kwenye vyombo vya habari kuhusu ulipaji wa kodi ya FIRE na ROAD LICENCE,tangazo hilo linawataarifu wamiliki wote wa vyombo vya moto wanapokwenda kulipia kodi yao ya mwaka ya ROad Licence watakakiwa pia kulipia na kodi ya FIRE ambayo mwanzoni haikua inalipiwa hapo TRA na imepanda kwa karibu asilimia 1400% ,jamani hata kama ni wizi sasa serikali yetu imezidi,kodi ambayo zamani ulikua unatakiwa kulipia sh,3000-5000 kulinganana na ukubwa wa injili sasa angalia viwango hapa chini kutokana na taarifa ilivyotolewa:
KUANZIA JULY 2012 HUDUMA ZA FIRE ZITAKUWA ZINALIPIWA TRA WAKATI WA KU-RENEW NA BEI NI;
CC 1 - CC 500 10,000/=
CC 501 - CC 1500 20,000/=
CC 1501 - CC 2500 30,000/=
CC 2501 na kuendelea 40,000/=
Hii ni fair kweli?,kodi yote ya nini hii na inapelekwa wapi? Rafiki yangu alikwenda pale TRA Samora kurenew road licence yake na ndipo aliposhangazwa na hili,gari yake ni Toyota Starlet amechajiwa 40,000/= na bado ilimchukua kama siku 3 kupata hiyo stika ya fire na tena akaambiwa baada ya hapo anatakiwa apeleka gari kwenye kituo cha fire kwa ukaguzi,unalipia fedha zote hizo na bado tena usumbuliwe ,Nchi yetu tunaelekea wapi jamani,Hii ndio jinsi ambayo serikali yetu inajitafutia njia ya kujiongezea kodi.Swali langu kwa wadau na wale wanaojua kuhusu hili,hivi kodi ya fire si ipo pale unapolipia BIMA yako au inakuaje?,Maanake bado tena hapo unaenda kulipia Bima ya gari yako ambapo najua pia kuna bima ya moto.Kweli serikali yetu inawanyanyasa wananchi wake,Mara ya mafao ya NSSF na leo tena mambo ya TRA na kodi za FIRE,cha ajabu ni je wananchi wana taarifa kuhusu haya au ndio kama mwenzangu unafika pale na kukuta unatakiwa kulipa kiasi ambacho mfukoni kwako hata huna na maisha yenyewe ya $ 1 kwa siku ,tunaelekea wapi?
 
hii ni huduma au biashara!??
eh tanzania weeee kodi tunakatwa hadi basi ila hata huduma za dharura tunauziwa-dah!!
 
huu ni wizi na ufisadi uliopitiliza, yaani sh 40,000 ni stika tu? au wanakupa na fire extinguisher?
upuuzi kabisa huu
wizi wa hali ya juu
 
Afadhali baada ya kufanya hayo yote basi ungekuwa sticker pia unatoka nayo hapo na mtungi,mambo ya kwenda tena fire linakuja tatizo lile lile la kuzungushana kimsingi watz walio wengi wanapenda kulipa kodi tatizo ni mfumo unapokuwa wa kusumbuana kulazimika mtu kuacha shughuli za siku nzima kwa ajili ya jambo moja
 
hii ni huduma au biashara!??
eh tanzania weeee kodi tunakatwa hadi basi ila hata huduma za dharura tunauziwa-dah!!

Vumilia kwa miaka kama mitatu, kwenye bajeti ya mwaka 2015 hizi kodi zitaondolewa!
 
Haya malipo ni wizi na usumbufu tu. Fire sioni uhusiano wao na magari. Gari likiungua unapata fidia toka bima!! Hawa askari wa fire walikuwa wasumbufu sana pale BP/Bandari. Wanadai rushwa kama haki yao eti kwa kuwa hana sticker !! Hivi mtu gari lako likianza kuwaka watu wa fire watakuja kuzima moto? wameshazima mangapi ? hata majengo yanawashinda itakuwa magari !! Huu ni wezi. Naanza kuona serikali yetu haina habari na matatizo ya wananchi wao wanataka kukamua tu wananchi bila sababu ya kueleweka.
 
hii ni huduma au biashara!??
eh tanzania weeee kodi tunakatwa hadi basi ila hata huduma za dharura tunauziwa-dah!!

Mama D yaani hii ni zaidi ya biashara,Maisha yenyewe magumu then wanakuletea na mambo ya kodi ambazo nadhani hata huwezi kufaidika nazo,Kwa kweli hii sio sawa na tunakoelekea ipo siku utaambiwa ulipie kodi hata ya kutembea au kusimama.dah hii nchi kweli imeuzwa.watu wanajitafutia jinsi ya maslahi yao wenyewe bila kuwafikiria wale wa chini.
 
Vumilia kwa miaka kama mitatu, kwenye bajeti ya mwaka 2015 hizi kodi zitaondolewa!

Mtumpole unamkatisha mam d tamaa kabisa ya maisha,miaka3 mpaka iishe si mtu atakua anatembele mikono,dah maanake tunapoelekea ipo siku utakutwa umesimama mahali au unatembea unakamatwa na kuambiwa ukalipie kodi za kusimama na kutembea bila sababu.Hivi hii nchi ni yangu au imehamishiwa sehemu nyingine maanake kila kukicha yanatokea mapya.
 
Kweli itakuwa ni usumbufu kwa nanma hii. Huwezi kulipia Fire sticker kabla mtungi haujakaguliwa, ni wazi TRA hawana ujuzi wa kukagua mitungi ya extinguisher hivyo lazima uende kwanza ofisi za fire (utatolewa upepo kidogo) wakati huo huo hujapata road licence, halafu malipo yanatakiwa kufanyika benki, uende benki (foleni kwa masaa manne)halafu urudi TRA, ukishawasilisha copy ya pay in slip utatakiwa kuja siku nyingine kuchukua hiyo road licence, si ajabu na sticker itakuwa hivyohivyo.

Kimsingi sioni sababu ya kulipia TRA kwa kuwa inayolipiwa ni ada ya ukaguzi wa Fire extinguisher kwa nini asilipwe anayekagua alipwe TRA? This is non sense!!!

Nilitegemea kampuni za insurance ndio labda zingepewa jukumu hili maana ndio zitakazoathirika janga likitokea hivyo watakuwa makini kuhakikisha fire extinguisher ni nzima,

Nimeshuhudia sticker zikitolewa bila ukaguzi wo wote,fikiria tajiri ana magari 30, na yote yako barabarani mikoa mbalimbali na nje ya nchi, kinachotokea analipa anapewa sticker zake, mchezo umekwisha. Na kwa zangu wa TRA wanachotaka ni hela tu, sijui itakuwaje. Haya hii ndio serikali yetu.
 
Ubora wa kitu au kifaa, utautambua katika matumizi/kukitumia. kadri tunavyoendelea kuwa na serikali hii ya CCM ndo tunajua ubora na ubaya wake. kwa mambo yake mengi yanayoendelea, Sijui kama kuna M- CCM wa kawaida ambae hausiki katika maamuzi, anaweza kusema hii serikali ni bora!? kama yupo ... basi Tumsamehe bure!
 
Wabongo mnashangaza. Si ilitakiwa uhoji uhalali wa hayo malipo hapohapo ulipolipia. Huku kwenye mtandao utapata nini?
 
40,000 sticker pekee :A S-confused1:, Sticker kwanza halafu ndio upeleke gari likakaguliwe!!, sio gari imefanyiwa ukaguzi kwanza ndipo waridhike inafaa kuwekewa hiyo sticker ya moto. TRA walipaswa kukamilisha zoezi zima bila mmiliki wa chombo cha moto kwenda tena ofisi za fire kwa ukaguzi, mgonjwa anapatiwa dozi kwanza ndipo aende kwenye vipimo? kweli hii nchi inakoelekea sio kabisa
 
Sasa mbona starlet halifiki CC 2000 imekuwaje ulipe ela zote izo
Hii serikali iko bize na dagaa mapapa kama Barick ,Vodacom,Azam wanagwaya kwenda kukusanya kodi stahiki
 
Back
Top Bottom