Madumbikaya
JF-Expert Member
- Jun 6, 2018
- 638
- 1,902
Mamlaka ya ardhi ijitathimini na ichukue hatua kabla maafa hayajatokea mitaa ya kariakoo kwa maghorofa kuporomoka ghafla kama ilivyokuwa pale posta mtaa wa Indira ghandi kwa kukagua na kusimamia ubora wa majengo
Leo naangazia mtaa mmoja tu wa kariakoo
Livingstone street Kariakoo,
Huu ni moja ya mitaa mirefu zaidi kariakoo na maarufu sana kwa biashara za spare za magari na matairi ya magari
Ni mtaa unaoanzia maeneo ya Fire au Makutano ya msimbazi na Morogoro road
Livingstone street kariakoo ni mtaa ambao kwa sasa nyumba nyingi za kizamani zinabomolewa na kujengwa maghorofa ya makazi na biashara baada ya wenyeji kuamua kuuza nyumba zao za chini na za kizamani
Maghorofa mengi mtaa huu yanajengwa usiku na hayafuati sheria zozote za usalama kwa majirani na wapita njia kwa miguu au magari
Mbao zinaning'inia na misumari inagongwa bila jengo kuwekewa uzio kwa ajili ya kuzuia vipande vya tofali, mbao na misumari kuwadondokea raia wanaopita kwa miguu
Maghorofa yanajengwa ndani ya miezi mitano na kukamilika huku yakiwa na floor zaidi ya saba. Je, slub inamwagiliwa maji muda gani? Na vipi uimara wa jengo lenyewe?
Haya majengo ground floor ni kwa ajili ya biashara na top floor ni kwa ajili ya makazi
Ghorofa namba moja lenye mashaka lipo makutano ya mtaa wa livingstone street na Amani street. Eneo hili watu wanapita kwa roho ngumu tu.
Ghorofa limejengwa kwa kasi na mabati na mbao zimeegeshwa tu juu muda wowote mbao na bati zinaweza kuwadondokea raia
Limebandikwa ubao wa ujenzi lakini mafundi wanaotumika sio engineers ni watu local ambao hawajavaa kifaa chochote cha usalama wao wenyewe na maisha yao, Wajenzi hawajijali wao. Je, watawajali raia ambao wanapita chini ya majengo hayo
Ni vyema mamlaka wakapita mtaa huu wa livingstone na kujionea uhalisia wa mambo kwani ujenzi unafanyika usiku na mchana ni kimya
Na je slub na kingo za haya maghrofa ni imara kwa kujenga haraka ndani ya miezi mitatu au mitano