huu ni utapeli kwa wapigakura! bora uchaguzi uhairishwe hadi nipate haki yangu

araway

JF-Expert Member
Sep 26, 2007
534
144
wakati wanaanzisha daftari la kudumu la wapiga kura sikuzani kwamba sikumoja nitashindwa kumpigia kura Rais just kwasababu nipo nje ya kituo nilicho jiandikishia, nilizani kuwa kura ya raisi naweza kupiga popote ilimradi niwe na utambulisho ambao kwangu mimi ni hiyo kadi ya mpigakura.
najiuliza ni wapi tumeiga stahili hii ya daftari la kudumu la wapiga kura na sie tukashindwa kuliboresha ili kila raia aliyejiandikisha aweze kupiga kura japo ya rais wa nchi popote pale awapo Tanzania hii, ninini kinashindikana?? inakuwaje wenzetu waweze kupiga kura hata wakiwa nje ya mipaka ya nchi zao sie watanzania tushindwe kisa upo nje ya kata uliyojiandikishia?? huu ni upuuzi na ushenzi na madhara yake ndo haya kwanza wanavyuo kushindwa kutimiza haki yao ya kupiga kura kwasababu za kipuuzi kama hizi! najiuliza ni watu wangapi watashindwa kupiga kura sababu ya kutokuwa katika maeneo yao waliojiandikishia kwa sababu tofauti.

wito wangu kwa wenye wazo la nini kifanyike ili kila raia aliejiandikisha aweze kupata haki yakupiga kura hata kwakuahirisha uchaguzi! :doh:
 
Watu wengi sana hawatapiga kura kwa sababu hiyo!
Inatakiwa tuende na wakati, hivyo vitambulisho viwe vya kielectroniki-ili kuruhusu mtu kupiga kura sehemu yoyote na kura kuhesabiwa papo hapo na matokeo kuonekana kwenye display nje ya kituo cha kupigia kura. Mara zote watu wako kwenye mihangaiko, na safari zingine si za kuahirisha!:mmph:
 
Back
Top Bottom