mgen
JF-Expert Member
- Nov 18, 2010
- 22,631
- 8,417
Mkuu, Asante sana yaani ni fupi na ya kueleweka! Mimi hiyo hutba ya mtoa uzi nimeisoma hadi alipoanza kulaumu kiongozi wa kiroho hana haki kimwili! As if uongozi wa mwili aachiwe ibilisi bila yeye kufahamu mwili unapokuwa dhaifu na roho pia inadhoofika! Tumtie moyo Fr Mapunda!Huwezi kumwelewa Padre Mapunda mpaka usome hotuba ya Nyerere aliyoitoa kwa masista wa Maryknoll wa huko Marekani miaka ya 70. Alipomaliza hotuba ile masista wale walitoa machozi kwa sababu ilikuwa na ukweli wa kusikitisha. Nani anataka kusikia habari za Yesu wakati ulimwengu huu umejaa uonezi na dhuluma? Si afadhali kufa tu huku ukisimamia "ukweli" kama alivyofanya Yesu mwenyewe? Hotuba ya Nyerere iliyowaliza Maryknoll sisters inaitwa "Church and Society" au kwa kiswahili "Kanisa na Jamii". Kanisa liliitafsiri hotuba ile kwa liugha mbalimbali na kuitawanya kwenye makanisa yake duniani waisome na kuitafakari. Sisi tukae tu na kuimba uchochezi. Inapatikana kwenye moja ya mavitabu yake ya hotuba zake. Ni vizuri kuisoma hotuba kama hiyo utaelewa kwa nini Padre Mapunda anakemea mambo kama anavyofanya.