Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,890
- 6,898
Katika hatua nyingine inayoashiria kuzidi kuungwa mkono kwa CHADEMA na viongozi wake, jana Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe alikuwa kivutio katika sherehe ya Siku ya Sheria nchini iliyofanyika katika viwanja vya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ambayo rais Jakaya Kikwete alikuwa mgeni rasmi.
Mbowe alikuwa kivutio wakati akiinuka kwenye kiti alichokaa kuelekea kwenye ngazi za Mahakama Kuu kupiga picha na viongozi mbalimbali wa serikali na mahakama ambao ni watumishi wa mahakama, mawakili na wananchi mbalimbali waliohudhuria sherehe hiyo. Watumishi wa mahakama pamoja na wananchi hao walisikika wakimshangilia kwa sauti ya juu Mbowe Mbowe, Mbowe na kiongozi huyo kulazimika kuwapungia mkono na kutabasamu.
Source, Tanzania daima newspapers