Kig
JF-Expert Member
- Aug 13, 2012
- 1,076
- 456
Nimefuga kuku 180 wa mayai (kuku wa kisasa). Lakini naona hawatagi mayai ipasavyo. Niliwanunua kuku hawa mwezi wa april tar 15, 2012 wakiwa vifaranga kabisa. Nimehudumia tangu aprili hadi leo september. Nilitegemea niwe napata mayai 150 (tray 5) au zaidi kwa siku. Lakini hadi sasa kuku wanaotaga wapo 75 hadi 80 tu, na nakusanya mayai tray 2 na nusu tu na wameanza kutaga mwezi wa nane. Hii inaashiria kuwa takribani kuku 100 hawatagi. Naomba msaada nifanyaje ili wote wawe wanataga mayai kama nilivyotegemea?