Huu mradi unanichanganya akili; nisaidieni jamani

Kig

JF-Expert Member
Aug 13, 2012
1,076
456
Nimefuga kuku 180 wa mayai (kuku wa kisasa). Lakini naona hawatagi mayai ipasavyo. Niliwanunua kuku hawa mwezi wa april tar 15, 2012 wakiwa vifaranga kabisa. Nimehudumia tangu aprili hadi leo september. Nilitegemea niwe napata mayai 150 (tray 5) au zaidi kwa siku. Lakini hadi sasa kuku wanaotaga wapo 75 hadi 80 tu, na nakusanya mayai tray 2 na nusu tu na wameanza kutaga mwezi wa nane. Hii inaashiria kuwa takribani kuku 100 hawatagi. Naomba msaada nifanyaje ili wote wawe wanataga mayai kama nilivyotegemea?
 
mkuu Kig

nina wasiwasi na feeding management ... nikiwa nina maana ya kwamba inawezekana kuku (layers) hawakulishwa evenly .. yaani kuna kuku hawakupata chukula cha kutosha kulingana na feed program (grams of feed per day per each lay hen) ... hii inatokana na upungufu wa vyombo vya chakula bandani (feeders) na kupelekea kuku wengine kuwa na lishe isiyotosha (insufficient feed) .... hii inawafanya kuku waliokosa hii lishe pia kukosa virutubisho na wadini yatakayowafanya watage.... virutubisho hivi ni kama vile lycen na DCP ..... pia sababu nyingine inawezekana kabisa uliwabania chakula

hivyo basi cha kufanya ... chukua kuku anayetaga na wengine Unadhani hawatagi .... pima uzito wao na ulinganishe .... ukiona kuna tofauti ya uzito wa +/- 0.15 to 0.2kg.... hapo kuna tatizo la required weight to lay egg

nakushauri ufanye sorting ya kuku wasiotaga na uwauze wasiendelee kula na Kulala bure ili u-replace vifaranga vingine

all the best
 
Nimefuga kuku 180 wa mayai (kuku wa kisasa). Lakini naona hawatagi mayai ipasavyo. Niliwanunua kuku hawa mwezi wa april tar 15, 2012 wakiwa vifaranga kabisa. Nimehudumia tangu aprili hadi leo september. Nilitegemea niwe napata mayai 150 (tray 5) au zaidi kwa siku. Lakini hadi sasa kuku wanaotaga wapo 75 hadi 80 tu, na nakusanya mayai tray 2 na nusu tu na wameanza kutaga mwezi wa nane. Hii inaashiria kuwa takribani kuku 100 hawatagi. Naomba msaada nifanyaje ili wote wawe wanataga mayai kama nilivyotegemea?

Hizi biashara nyingine una risk tu....inakua kama kamali anytime unawin au unapoteza mazima....umetumia mtaji mkubwa alaf return yake ya kubahatisha....kwanini usifanye biashara iliyo na minimum risks at the same time return ni kubwa !! ona sasa pesa inavyopotea....mimi kuna biashara nafanya ina risk ndogo sana....na hata kama sijauza kitu....sina cha kupoteza na kama nikiuza faida napata tena kubwa tu...ila still mtaji niliouweka ni mdogo sana !! Cha muhimu ni kujituma kwako tu. Ni PM kwa habari zaidi....
 
Hiyo biashara yako iseme peupe, kama ni ya kificho basi hukuwa na haja ya kumsaidia huyu ndugu.
 
Mkubwa, hiyo attachment weka hapa watu tusome, kisha tukiona inalipa tutakufuata wenyewe mkuu. Usijali urefu, ww weka hapa, mbona wenzio wanaweka kila kilicho na manufaa kwa jamii hapa hapa jamvini?

Senior member hanijui wala simjui lakini naweza kuona hapa kuna dalili za utapeli

Au kama sio tapeli biashara atakayokutambulisha ni zile biashara za NETWORK MARKETING
 
Una weza ukawa sahihi kabisa. Ona sasa tumeharibu na thread ya mtu, jamani turudi ktk thread ya jamaa.
 
Pole ila sio kitu cha kukukatisha tamaa, nnavyojua kuna sababu nyingi
1. aidha uliuziwa broiler au jogoo, ni kawaida mayai kuanguliwa pia kwa vile bei zinatofauti kubwa sana kama sio wakala mwaminifu anaweza kuweka wengi ila kwa kila batch tegemea wawepo jogoo, cha kufanya sort out hao wasiotaga kama wana uzito mzuri uza kama mdogo walishe wanenepe kisha wauze
2. Chakula kama alivyoeleza mdau hapo juu, sijui kama inaweza kuwa reversible tafuta doctor akushauri, pia we mwenyewe chunguza chakula chako kama ni bora, badili kama unanunua kwa mifuko, ongezea vitu vingine kama "Layers kuku Bora" etc ili kuchochea utagaji unajua kama tulivyo binadamu kuku nao hutaofautiana fertility
3. Genetic, pengine ni aina wanachelewa kuanza kutaga usi panicky tafuta ushauri kwanza usije chinja kumbe wamechelewa tu
4. Kuna aina za magonjwa ambazo huwa zinadumaza ukuaji na utagaji wa kuku angalia na kumbuka historia ya uleaji kuku wako kama waliumwa ugonjwa gani na uliuzia effects zake kama reversible
5. Predators, juzi na mie kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na majaribio nimefuga hybrid wa malawi tayari wanataga na Cornish brown (courtesy of RETI) nilikuwa nashangaa mayai pungufu hadi kushtuka naambiwa panya anakunywa! na pia kumbe sijawakata mdomo, vile hukuti hata maganda huwezi jua nini kinaendelea, angalia security ya banda lako
Mwisho nakushauri ufugaji ni biashara lakini kama ilivyo kwa binadamu kuku ni viumbe hai, mengi yanaweza kuadhiri hii biashara hivyo unapohesabu faida weka 75% ya kuku chini ya hapo ndio ulizia ushauri, na hata kama unafanya hesabu zako za forecasting/cashflow weka hiyo na ununuapo vifaranga ukitaka idadi fulani watage ongeza hiyo risk ya 25%. Kaza buti umejitahidi hata hivi kufika hapo. Wataalamu watajazia hapa

Nimefuga kuku 180 wa mayai (kuku wa kisasa). Lakini naona hawatagi mayai ipasavyo. Niliwanunua kuku hawa mwezi wa april tar 15, 2012 wakiwa vifaranga kabisa. Nimehudumia tangu aprili hadi leo september. Nilitegemea niwe napata mayai 150 (tray 5) au zaidi kwa siku. Lakini hadi sasa kuku wanaotaga wapo 75 hadi 80 tu, na nakusanya mayai tray 2 na nusu tu na wameanza kutaga mwezi wa nane. Hii inaashiria kuwa takribani kuku 100 hawatagi. Naomba msaada nifanyaje ili wote wawe wanataga mayai kama nilivyotegemea?
 
Senior member hanijui wala simjui lakini naweza kuona hapa kuna dalili za utapeli

Au kama sio tapeli biashara atakayokutambulisha ni zile biashara za NETWORK MARKETING

inatakiwa aiweke hapa,ukiona wanaitana pembeni ujue kuna harufu ya utapeli ambayo anaogopa akiweka apa baaz ya wajanja watamshtukia
 
Pole ila sio kitu cha kukukatisha tamaa, nnavyojua kuna sababu nyingi
1. aidha uliuziwa broiler au jogoo, ni kawaida mayai kuanguliwa pia kwa vile bei zinatofauti kubwa sana kama sio wakala mwaminifu anaweza kuweka wengi ila kwa kila batch tegemea wawepo jogoo, cha kufanya sort out hao wasiotaga kama wana uzito mzuri uza kama mdogo walishe wanenepe kisha wauze
2. Chakula kama alivyoeleza mdau hapo juu, sijui kama inaweza kuwa reversible tafuta doctor akushauri, pia we mwenyewe chunguza chakula chako kama ni bora, badili kama unanunua kwa mifuko, ongezea vitu vingine kama "Layers kuku Bora" etc ili kuchochea utagaji unajua kama tulivyo binadamu kuku nao hutaofautiana fertility
3. Genetic, pengine ni aina wanachelewa kuanza kutaga usi panicky tafuta ushauri kwanza usije chinja kumbe wamechelewa tu
4. Kuna aina za magonjwa ambazo huwa zinadumaza ukuaji na utagaji wa kuku angalia na kumbuka historia ya uleaji kuku wako kama waliumwa ugonjwa gani na uliuzia effects zake kama reversible
5. Predators, juzi na mie kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na majaribio nimefuga hybrid wa malawi tayari wanataga na Cornish brown (courtesy of RETI) nilikuwa nashangaa mayai pungufu hadi kushtuka naambiwa panya anakunywa! na pia kumbe sijawakata mdomo, vile hukuti hata maganda huwezi jua nini kinaendelea, angalia security ya banda lako
Mwisho nakushauri ufugaji ni biashara lakini kama ilivyo kwa binadamu kuku ni viumbe hai, mengi yanaweza kuadhiri hii biashara hivyo unapohesabu faida weka 75% ya kuku chini ya hapo ndio ulizia ushauri, na hata kama unafanya hesabu zako za forecasting/cashflow weka hiyo na ununuapo vifaranga ukitaka idadi fulani watage ongeza hiyo risk ya 25%. Kaza buti umejitahidi hata hivi kufika hapo. Wataalamu watajazia hapa

Nashukuru sana Mama Joe na wengine kwa michango yenu nitaifanyia kazi. Ila kuna wengine humu ndani ni matapel tafadhali sana wadau muwe makini. Hao wanaodai niwaPM nimetawatumi PM, badala ya kunitumia hiyo attachment eti nwanadai niwatumie namba yangu ya simu na email address. Nikaona hawa mateja wamefuliaaaa tena bila sabuni.
 
Hizi biashara nyingine una risk tu....inakua kama kamali anytime unawin au unapoteza mazima....umetumia mtaji mkubwa alaf return yake ya kubahatisha....kwanini usifanye biashara iliyo na minimum risks at the same time return ni kubwa !! ona sasa pesa inavyopotea....mimi kuna biashara nafanya ina risk ndogo sana....na hata kama sijauza kitu....sina cha kupoteza na kama nikiuza faida napata tena kubwa tu...ila still mtaji niliouweka ni mdogo sana !! Cha muhimu ni kujituma kwako tu. Ni PM kwa habari zaidi....

Acha Utapeli tu unakusumbua. Mbona naku PM unanidai namba ya simu na email unataka za nini?
 
Kig,hayo ni mambo yua kawaida sana katika poultry business,usikate tamaa,usichukue maamuzi ya haraka,zingatia ushauri wa walionitangulia kucomment(except huyo tapeli) na zingatia kutafuta daktari wa mifugo,,,kama upo dar,nenda tanvet pale ubungo,kuna daktari mzuri,anaweza akakusaidia.zingatia sana ratio ya chakula(madini joto,damu,mifupa,chokaa,chumvi,mashudu etc),chunguza hali ya mwanga kwenye banda na hewa(ventilations),hakikisha kuna maranda ya kutosha na sehemu za kutagia mayai zinatosha,pia tafuta na ununue dawa ya kuchanganya kwenye maji ya kuku inaitwa Egg Booster..on top of that,anayehusika na kutoa mayai na kulisha awe specific,kwa mfano,kama ni mtoto,au mtu wa kazi,kwa kitendo cha kuwashtua shtua kuku au kuwapiga wakati akipita kinaweza kuchangia kuku wasitage pia...ukizingatia haya pamoja na wenzangu utafanikiwa tu.....narudia tena....BIASHARA HII INAHITAJI UVUMILIVU NA UFUATILIAJI WA KARIBU SANA.kila la kheri ndugu
 
Last edited by a moderator:

Nashukuru sana kwa ushauri wako. Mungu akubariki sana.
 
naomba kutoa feedback,,,kwa hisia za kawaida tu,huyu Senior Manager anajaribu kushawishi mambo yale yaleee,ya network marketing,,,kaka hapa umechemka,sijiungi ng'oo.hizo powerpoint ulizotengeneza ndugu ni za kucopy na kupaste kutoka TVi na Oriflame umebadilisha vitu vichache tu,,,bado unang'ang'ania namba yangu.....ushindwe na ulegee........ila nisikukatishe tamaa,fungua hata ka-website basi hata tuwe na viji-imani,sikuhizi matapeli ni wengi.....huwezi ku-invest hela yako kwenye kampuni ambao ni wabahili wa hadi kutengeneza kitu kidogo kama website.......nimeingilia mada ili usisumbue wengine.....Fungua thread yako abt hiyo business yako na ujaze nyama zaidi.....nawatahadharisha tu wengine kwamba huyu ni walewale wa network marketing.....
 
huwa iantokea mara kwa mara kama kuku ndo mara yao ya kwanza kuanza kutaga,pia n ngumu kwa kuku wote kutaga kwa wakati m1,arafu unaweza kukuta kuna matasa ndani yake japo n ngumu kuyagundua,kingine cheki na chakula unachowapa kinawezekana co kizuri kwao.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom