Hussein Bashe: Membe amuache Rais Magufuli afanye kazi

Mimi sielewi...ina maana mtu ukimkosoa Magufuli ndo hutaki afanye kazi yake?

Ukimkosoa ndo unamzuia kufanya kazi yake?

Huyo Magufuli yuko juu ya kila kitu hata kukosolewa/ kujadiliwa?
Huo ndio mtazamo wa wana ccm
 
Kiukweli CCM ni mchanganyiko wa vyama vingi tofauti ndani yake

kinachowaunganisha ni kuwa madarakani tu
siku wakitoka watabaki vipandevipande....

ndo maana kuna vision tele
kila mtu na yake.....na wafuasi nao kila mtu na kundi lake....
Umeonaeee...

Sawa na CHADEMA asili(inayopambana na ufisadi kikwelikweli ikiongozwa na Dr Slaa) na CHADEMA inayotetea na kusafisha mafisadi(ikiongozwa na mbowei).
 
Sio culture ya CCM kumkosoa Rais

Sababu hata Magufuli mwenyewe hakupatikana katika open contest

Sasa sababu wanajua ile mandate ya Magufuli sio genuine
kila anaemkosoa wanaona 'kuna hatari' ya kuinfluence uasi...

hilo ndo linalowasumbua.....na sio Magufuli tu
kina Kolimba walimkosoa Mkapa....Kambona alijaribu kumkosoa Nyerere
Mrema kumkosoa Mwinyi...the list is endless.....kukosoa sio culture ndani ya CCM

Ila kukosoa ni culture ya wapi? Ni wapi au nchi gani ambapo Viongozi hukosoa vyama vyao wenyewe kwenye vyombo vya Habari?
 
Ila kukosoa ni culture ya wapi? Ni wapi au nchi gani ambapo Viongozi hukosoa vyama vyao wenyewe kwenye vyombo vya Habari?

Nchi nyingi tu watu hukosoa vyama vyao hadharani
nchi karibu zote za demokrasia hilo ni kawaida....ni utamaduni watu kukosoana...hadharani bila kuogopa
 
Nchi nyingi tu watu hukosoa vyama vyao hadharani
nchi karibu zote za demokrasia hilo ni kawaida....ni utamaduni watu kukosoana...hadharani bila kuogopa

Kusema Nchi nyingi kila mtu anaweza kusema, nitajie nchi moja na mfano ambapo Kiongozi wa Chama na jina la hicho Chama na Cheo cha huyo Kiongozi kwenye hicho chama ambapo alienda kwenye vyombo vya Habari na kukosoa Chama chake bila kupitia kwanza kwenye vikao vya Chama chake!
( kwa hapa Membe ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM hivyo huyo kiongozi awe na wadhifa kama wa Membe au unaofanana kwenye hicho alichokosoa)
 
Kiukweli CCM ni mchanganyiko wa vyama vingi tofauti ndani yake

kinachowaunganisha ni kuwa madarakani tu
siku wakitoka watabaki vipandevipande....

ndo maana kuna vision tele
kila mtu na yake.....na wafuasi nao kila mtu na kundi lake....

Haswaa.....humo ndani Kuna chama cha wafanyabiashara na vision yao ni kukaa vizuri na wafanyabiashara wachache wenye nguvu kubwa ya pesa kwani Hao ndio kila kitu katika uendeshaji wa nchi, hawa pia hutoa uhuru wa habari na vyombo vya habari pasipo mipaka. Pia huko ndani Kuna chama chenye vision ya "wananchi", wale wa jembe na nyundo, hawa hawatoi uhuru wa kufuru wa habari na vyombo vya habari, maskini na tajiri wanawekwa fungu moja la wanachi, hamna privileges (Tajiri kumunukisha shombo la maskini inawaudhi sana wale wa Chama cha kwanza). Halafu Kuna vikundi vya kushangilia, kuzomea, kuponda, kusifia etc, vyote viko huko ndani. Basi unaposikia ccm ni taasisi kubwa ujue ni kubwa kwelikweli si mchezo...
 
Unakumbuka ticket ya ndege sh 600000 ,ofisi ya Membe walikua wanaandika sh 6000000????yaani wanaongeza sifuri.
Membe ni mtoa na mpokea rushwa.Pesa ya Gadafi kijenga kiwanda cha cement lindi kafanya ni mradi binafsi kupitia kwa mfanyabiashara feki
 
Unakumbuka ticket ya ndege sh 600000 ,ofisi ya Membe walikua wanaandika sh 6000000????yaani wanaongeza sifuri.
Membe ni mtoa na mpokea rushwa.Pesa ya Gadafi kujenga kiwanda cha cement lindi kafanya ni mradi binafsi kupitia kwa mfanyabiashara feki
 
Sio culture ya CCM kumkosoa Rais

Sababu hata Magufuli mwenyewe hakupatikana katika open contest

Sasa sababu wanajua ile mandate ya Magufuli sio genuine
kila anaemkosoa wanaona 'kuna hatari' ya kuinfluence uasi...

hilo ndo linalowasumbua.....na sio Magufuli tu
kina Kolimba walimkosoa Mkapa....Kambona alijaribu kumkosoa Nyerere
Mrema kumkosoa Mwinyi...the list is endless.....kukosoa sio culture ndani ya CCM

Kuongeza nyama kidogo, kukosoa sio utamaduni katika siasa za Tanzania, si unakumbuka ya Zitto na Chadema, ya Hamad na CUF, ya Kafulila na Nccr...the list goes on...
 
hongera bashe. kwa kueleza ukweli. daima ukweli na uwongo haukai pamoja. makufuli usikatishwe tamaa na membe ww fanya kazi . badili mfumo uliooza kwa manufaa ya watanzania walio wengi. maamuzi anayofanya makufuli ni kwa manufaa ya nnchi na sio manufaa yake. safari ya kutumbua majipu haitakua rahisi sana, lazima ikumbane na vikwazo vingi vya watu wanaofanana na kina membe . go makufuli don't look back.
 
Sasa hapa wafuasi wa CCM wako njia panda. Wakimsupport Bashe wataonekana wanamsuport EL. Wakimpinga Bashe wataonekana wanaungana na BCM kumpinga JPM
 
Ah membeeeee, mara tulipishana angani kama kwetu kunawaka moto, ghafla huwezi kutawala bila kutoka nje utake usitake utatoka tu!!!
 
Achana na kitu inaitwa pesa nchi ilikua mikononi mwa wafanyabiashara ,kurudisha umiliki wa uchumi kwa wananchi Magufuli anatakiwa awe na kichwa cha mwendawazimu sio kazi ndogo ,japo pia hilo la kurudisha uchumi kutoka kwa matajiri kumilikisha wananchi sijui kama litafanikiwa naskia dunia yote hii inaongozwa na familia 13 kina Rothschild ,Rockefeller na wenzake
 
Back
Top Bottom