Humphrey Polepole ni nani?

Mjomba Mkude

JF-Expert Member
Nov 21, 2013
287
110
Humphrey Polepole, mjumbe wa iliyokuwa Tume ya Katiba amekuwa mstari wa mbele kutoa maelezo, ufafanuzi na kukabiliana kwa hoja na Wapinzani wa rasimu katiba iliyowasilishwa.

Kipekee nampongeza sana kwani tume ilikuwa na wajumbe wengi lakini wengine wako kimya ila Bwana Polepole amekabiliana nao na anaendelea kukabiliana nao dhidi ya upotoshaji, kwangu mimi Bw Polepole anastahili tunzo ya heshima.

Nawakaribisha wadau kwa maoni.
 
Last edited by a moderator:
Huyu kwangu namwita kijana shujaa katikati ya wanyama wakali na mchukulia kama kijana wakuingwa ndani ya taifa letu Tanganyika aka Tanzania ni hazina kubwa sana hongera sana kijana Polepole.
 
Dr. Mvungi alikuwa kikwazo kwa haya wanayotaka CCM hii leo ili kuondoa udhia WAKAMUA ushahidi wa kuhusika huku kwa hawa jamaa ni ile movie ya KOVA kwenda kwenye vyombo vya habari na kuonyesha Bendera na Kofia zenye rangi za CDM kuwa ndio walizokamatwa nazo wahusika wa tukio lile lakini baadae tukasikia matamko kuwa Familia na wahusika wamesamehe mungu atawahukumu waliohusika na ndio ukawa mwisho wa ufuatiliaji wa tukio lile na hata wale tulioambiwa wamekamatwa sijawahi kusikia mwendelezo wa kesi ile.

Kwa hiki anachokifanya bwn polepole ni vema akajilinda na hawa wauaji kwani wanaweza kumziba mdomo kwa kumkatisha uhai wake ili waendelee na hizi sarakasi zao za kupindua maoni ya wananchi na hapa ndipo ninapoona uhalisia wa hili jina CHAMA CHA MAPINDUZI
 
Nchi ina watu wengi wenye weledi mkubwa sana ndugu zangu na huyu ni mmoja wao, ila mfumo hauruhusu kumea na kushamiri kwa watu wasio tegemezi na wenye fikra huru!!!!!

Wako vijana wengi sana wazuri kichwani na wako motivated sana ila hawataki kukuru kakara za uweledi kuingiliwa na siasa yaani ni kama wasomi wamesusia wanasiasa waendeshe nchi watakavyo liwalo na liwe sababu hata wakichangia wanaonekana kwenye mchakato lakini kwenye maamuzi au implememtation wanaachwa......mfano ndio huo wa tume...... kwa sasa wanaonekana wabaya, wamefanya kazi hovyo na kama hayo !!!!!!

Wakati tume ilitakiwa iwepo na huko bungeni wakae na kutoa ufafanuzi kila inapohitajika ila ndio kama hivyo sasa!!!!!!!
 
Tanganyika yetu itakaporudi yeye pamoja na Tume nzima ya Warioba watapewa Tuzo ya heshima ya juu sana Ya Tanganyika
 
Huyu mtu binafsi nimemwelewa sana japo yeye mwenyewe aliwahi kutamka wazi wazi yeye ni mwanachama wa CCM haswa lakini nimemuona amesimama kwenye ukweli zaidi kuliko kwenye siasa, ameitumia elimu yake ipasavyo na baadhi yetu wananchi tumemwelewa
 
Japo nilikuwa na haraka jana sikumsikiliza sana, ila alikuwa anajenga hoja vizuri on Star Tv - than Mwingulu, anyway mimi bado sijaona sababu ya UKAWA kususa, I thought - wangewatumia watu kama hawa akina Polepole "wakiwa nje ya bunge", and then wakati wa debate bungeni wawe wanatoa ufafanuzi wenye details kama hizi, badala ya njia waliyochukua, UKAWA wengi naona hawakujindaa kwa hoja instead walikimbilia mkenge wa mipasho na matokeo yake wamekimbilia hoja ya Intarahamwe eti CCM ni wengi, anyway tusubiri tuone movie
 
Sasa kwanini UKAWA wanashindwa kufanya hivyo na wanakimbilia mipasho badala ya hoja?
Huyu mtu binafsi nimemwelewa sana japo yeye mwenyewe aliwahi kutamka wazi wazi yeye ni mwanachama wa ccm haswa lakini nimemuona amesimama kwenye ukweli zaidi kuliko kwenye siasa ,ameitumia elimu yake ipasavyo na baadhi yetu wananchi tumemwelewa
 
Japo nilikuwa na haraka jana sikumsikiliza sana, ila alikuwa anajenga hoja vizuri on Star Tv - than Mwingulu, anyway mimi bado sijaona sababu ya UKAWA kususa, I thought - wangewatumia watu kama hawa akina polepole "wakiwa nje ya bunge", and then wakati wa debate bungeni wawe wanatoa ufafanuzi wenye details kama hizi, badala ya njia waliyochukua, UKAWA wengi naona hawakujindaa kwa hoja instead walikimbilia mkenge wa mipasho na matokeo yake wamekimbilia hoja ya Intarahamwe eti CCM ni wengi, anyway tusubiri tuone movie

Mjadala wa Katiba uko Bungeni, Maamuzi yote yako Bungeni. UKAWA wako sahihi kabisa na hasa kwa kuzingatia sheria ilivyo. Hawataendelea na kikao maana hawana tumaini la kutoa maamuzi bila UKAWA. Huwezi kuendelea kujadili na kundi la watu ambao hawako tayari kusikiliza. Wamejipanga kupinga makofi na vigelegele bila sababu.

Wanazomea bila sababu. Wanaingiza hayo ya ukabila kama yalivyotanjwa na Lipumba. Mbona UKAWA haijataja wasomali walioko CCM?
 
Back
Top Bottom