Humphrey Polepole: Jaji Ntemi alitufuata CCM akatuomba tumpelekee orodha ya Mawakili tunaotaka wafungiwe

chiembe

JF-Expert Member
May 16, 2015
12,009
20,683
Mbombo ngafu, Kwanini awafuate CCM? Sio TLP au Kituo Cha Sheria na Haki za Binadamu, au wakuu wa mikoa?

Humphrey Polepole Machi 6 2021, aliwahi kusema kuwa Jaji Ntemi aliwatafuta CCM akafungua milango kama kuna mawakili wanawasumbua watanzania basi wao(CCM) wapokee taarifa za Mawakili hao na wawapelekee wao (Kamati ya maadili ya Mawakili), na kama tuhuma zitathibitika basi mtuhumiwa atafutiwa Uwakili mara moja ili mtu huyo akafanye kazi nyingine.

 
Hii kauli ndio inathibitisha yanayotokea sasa, inasikitisha na kushangaza sana kuona majaji wameamua kugeuka majambazi wanaopora haki za wengine, ili kumfurahisha bosi anayewapandisha vyeo.

Samia lazima atuthibitishie uhai wa kauli zake anazotoa kila siku kuwataka majaji watende haki, atuoneshe yupo tayari kusimamia haki hata kama haki hiyo itayagusa maslahi yake kwa namna moja au nyingine.

Lakini kinyume na hapo, akiwaacha hao majaji waendelee kuwakandamiza wapinzani wake kwa maslahi yake, basi atambue zile kauli zake za kutaka haki itendeke kwenye idara ya mahakama zitabaki huko huko majukwaani tu.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
View attachment 2821695
 
Mbombo ngafu., Kwa nini awafuate CCM? Sio TLP au Kituo Cha Sheria na Haki za Binadamu, au wakuu wa mikoa?
View attachment 2821320
Nimemsikia!, kwanza Tanzania hatujawahi kuwa na Jaji Mtemi Ramadhani, Jaji ni Agustino Ramadhani. Mtemi Ramadhan ninayemjua mimi , ni aliyekuwa mchezaji wa Simba, kisha kiongozi wa Simba kisha kiongozi wa FAT.

Ila pia siwezi kushangaa, kwa hizi teuzi za majaji wa voda fasta, usikute Mtemi Ramadhan kawa Judge maana alikuja kusomea sheria OUT. Niliwahi kusema kitu kuhusu majaji wetu, Ukosekanaji wa Haki kwenye Mhimili wa Mahakama, kunaweza kuwa kunachangiwa na Majaji/Mahakimu wenye uwezo mdogo kubaini haki? usikute majaji wenyewe ndio hawa!.

P
 
Nimemsikia!, kwanza Tanzania hatujawahi kuwa na Jaji Mtemi Ramadhani, Jaji ni Agustino Ramadhani. Mtemi Ramadhan alikuwa mchezaji wa Simba, kisha kiongozi wa Simba kisha kiongozi wa FAT.
P
Mkuu, hii ifute kabla wateja wako wa uwakili hawajaiona, Judge Incharge Mahakama Kuu Masjala Ndogo Mwanza ni nani? Na pia alikuwa Jaji Incharge Mahakama Kuu Masjala NdogoBukoba akaacha madudu matupu huko.

Ingia google utakutana na mautumbo anayoandika katika hukumu. Anafuta mwenendo wote wa shauri wa mahakama ya chini, halafu anatumia mwenendo huo huo kutoa uamuzi na kutangaza mshindi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom