domokaya
JF-Expert Member
- Apr 22, 2010
- 3,545
- 1,722
Kuhubiri mabadiliko na kufanya mabadiliko ni vitu viwili tofauti.Tulihubiriwa Ccm mpya inakuja,Nilichoona mimi ni ccm ile ile kama wimbo wao ulivyo tu.Nini kimebadilika?
Pole pole na Rodrick Mpogolo unaweza kuiita ccm mpya?"Hapana"Ni ile ile.
Tuliambiwa wasaliti wataisoma namba,Msaliti namba moja wa chama alikuwa Nchimbi.Leo ni balozi"Ccm ni ile ile.Mnabisha?Kama unabisha nionyeshe hiyo ccm mpya.
Kwani wewe unataka nini? Waachie wenyewe CCM yao. Kama wewe huoni upya wao wenyewe wanauona. Inawezekana wewe upya uutakao ni watu, lakini wenyewe upya wao wanaotaka ni mabadiliko na upya katika fikra. Mtu anaweza kuwa yule yule akabadilika fikra na mtu aaweza kuwa mpya akawa na fikra kama yule aliyepita. Upya muda mwigine ni relative!