Nyahende Thomas
JF-Expert Member
- Nov 5, 2010
- 211
- 104
Katika taarifa ya habari Itv usiku huu, saa 2 wametangaza habari ya mwanamke mmoja aliyeporwa mtoto wake wa miezi minne na ndugu wa mume wake aliyepo nje ya nchi kwa sasa.
Uporaji wa mtoto huyo umefanywa na ndugu wa mume wa mwanamke huyo kupitia hukumu ya mahakama ya hakimu mkazi Kisutu kwa kile kinachodaiwa kwamba mama wa mtoto ni mgonjwa sana kiasi ambacho hawezi kumnyonyesha mwanae.
Kwa mujibu wa maelezo ya ndugu wa mke ni kwamba upande wa mume waliidanganya mahakama kwakuwa hawamtaki mke wa kijana wao.
Akihojiwa na Itv hakimu huyo amekiri kutoa amri hiyo lakini akadai kwamba ombi hilo lilipelekwa kwake chini ya hati ya dharura.
MY TAKE:
Kitendo cha hakimu kuwa mwepesi kumtenganisha na mama yake, mtoto mdogo kiasi kile bila kumuita mahakamani ama kuwa na uhakika wa hali ya afya ya mama yake kinaidhalilisha mahakama na kutia shaka weledi wa mahakimu wetu.