Hukumu ya Mwanamke aliyeporwa mtoto, Mahakama imejiaibisha...!!

Nyahende Thomas

JF-Expert Member
Nov 5, 2010
211
104
Katika taarifa ya habari Itv usiku huu, saa 2 wametangaza habari ya mwanamke mmoja aliyeporwa mtoto wake wa miezi minne na ndugu wa mume wake aliyepo nje ya nchi kwa sasa.
Uporaji wa mtoto huyo umefanywa na ndugu wa mume wa mwanamke huyo kupitia hukumu ya mahakama ya hakimu mkazi Kisutu kwa kile kinachodaiwa kwamba mama wa mtoto ni mgonjwa sana kiasi ambacho hawezi kumnyonyesha mwanae.
Kwa mujibu wa maelezo ya ndugu wa mke ni kwamba upande wa mume waliidanganya mahakama kwakuwa hawamtaki mke wa kijana wao.
Akihojiwa na Itv hakimu huyo amekiri kutoa amri hiyo lakini akadai kwamba ombi hilo lilipelekwa kwake chini ya hati ya dharura.

MY TAKE:
Kitendo cha hakimu kuwa mwepesi kumtenganisha na mama yake, mtoto mdogo kiasi kile bila kumuita mahakamani ama kuwa na uhakika wa hali ya afya ya mama yake kinaidhalilisha mahakama na kutia shaka weledi wa mahakimu wetu.
 
Ana miez 3 si mi 4, inaonekana hakimu kahongwa pesa mingi kiasi cha kuona ni haki kumtenganisha na mama yake kiumbe huyo anayehtaji mapenzi ya mama yake, ROHO MBAYA NA UKATILI WA HALI YA JUU
 
Wametumia SHERIA ZA KIISLAM,kuamua hiyo kesi mkuu!si unajua zilivyonamagumashi

Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu si mahakama ya kiislamu (mahakama ya kadhi) ndugu yangu, sasa hizo sheria za kiislamu zinatoka wapi?

Ndugu wa mume amedai kwamba anataka kuongea na mwanamme mwenzake hamtaki mama kwa kuwa yale ni mambo ya wanaume kwa mujibu wa sheria za kiislamu.
Sina uhakika kama sheria za kiislamu ndivyo zilivyo, kama kuna anayeifahamu vizuri sheria hiyo nitaomba afafanue hapa.
 
Ana miez 3 si mi 4, inaonekana hakimu kahongwa pesa mingi kiasi cha kuona ni haki kumtenganisha na mama yake kiumbe huyo anayehtaji mapenzi ya mama yake, ROHO MBAYA NA UKATILI WA HALI YA JUU

Kilichonisikitisha zaidi ni kwamba hakimu mwenyewe ni mwanamke lakini katika hili haonekani kutambua umuhimu wa maziwa ya mama kwa mtoto.
 
Huyo Jaji alijiridhisha kuwa mama wa mtoto kweli ni mgonjwa kiasi cha kutoweza kumlea mwanae?
Wabunge wa viti maalum wanawake -hasa wale wa UWT wanasemaji?
 
Huyo [blue=red]Jaji[/color] alijiridhisha kuwa mama wa mtoto kweli ni mgonjwa kiasi cha kutoweza kumlea mwanae?
Wabunge wa viti maalum wanawake -hasa wale wa UWT wanasemaji?

hapana si jaji huyo alotoa hukumu mdau,,,,,,,
 
Kilichonichosha zaidi hakim mwenyewe ni mwanamke mwenzake pia mtoto ni wa miezi miwili. Tz tumekwisha kwa sasa hakuna shm ya haki wala usalama!
 
Huyo Jaji alijiridhisha kuwa mama wa mtoto kweli ni mgonjwa kiasi cha kutoweza kumlea mwanae?
Wabunge wa viti maalum wanawake -hasa wale wa UWT wanasemaji?

Siyo Jaji ni hakimu ila kiukweli inauma maamuzi mengine kwani hati ya dharula ndio inamwongoza hakimu? hapa amekurupuka huyu hakimu
 
uislam unasemaje hapo mdau,,,,,kwani mahakama hiyo ni ya kiislam????

Kuna mbaba ndugu wa mwanaume alionekana akisema kwenye camera ya ITV kwamba kwa sheria ya kiislamu mwanamume ndio mwenye sauti katika jambo hilo, sasa nikajiuliza mbona hilo suala wamelipeleka kwa mahakama ya serikali (Kisutu)
 
Ndo mahakama za kadhi zijianza sijui itakuwaje kwa haki za wakina mama
 
Kuna mbaba ndugu wa mwanaume alionekana akisema kwenye camera ya ITV kwamba kwa sheria ya kiislamu mwanamume ndio mwenye sauti katika jambo hilo, sasa nikajiuliza mbona hilo suala wamelipeleka kwa mahakama ya serikali (Kisutu)

ngoja tuangalie gol la barotel
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom