SoC03 Hukumu ya kifo ikifanyiwa mabadiliko na kutumika vizuri inaweza kuleta mabadiliko makubwa nchini

Stories of Change - 2023 Competition

MAMESHO

JF-Expert Member
Jul 5, 2011
1,366
1,622
Hukumu ya kifo kwa makosa makubwa yaweza kuleta mabadiliko makubwa nchini


Najua umevutiwa na kichwa cha habari cha andiko hili. Najua Makala hii itapokelewa kwa hisia tofauti kutokana na maudhui itakayokuwa imeyabeba. Nikutahadharishe kabla huajendelea kuwa msingi wa Makala hii ni mawazo binafsi. Mimi sio mwanasheria, ni mwananchi wa kawaida ninayejua sheria kwa uchache wa sheria nilizoweza kuzielewa.

Hukumu ya kifo ni jambo ambalo limejadiliwa sana. Wengi wana maoni tofauti juu ya matumizi ya adhabu ya kifo. Ni adhabu ya juu kabisa kuweza kutolewa katika mahakama popote duniani. Japokuwa taasisi za haki za binadamu wanasema inakinzana na haki ya msingi inayosema kuwa kila mtu “ana haki ya kuishi” lakini bado tunaona adhabu hii inatumika maeneo mbali mbali duniani.

Kwa sheria ya nchi yetu Tanzania, hukumu ya kifo inaweza kutekelezwa kwa makosa ya aina mbili ambayo ni ya mauaji na uhaini

Makosa ya mauaji, kifungu cha 197 cha kanuni ya adhabu (sura ya 16) inatoa tafsiri kwamba, ikiwa utahusika na uuaji utahukumiwa kifo kwa kunyongwa. Utekelezaji wa hukumu hii utaacha wale ambao ni wajawazito au ambao ni chini ya miaka 18 kwa maelekezo maalumu kutoka kwa raisi au waziri wa sheria. Adhabu mbadala kwa walitoenda kosa ambao ni wajawazito au chini ya miaka 18 watahukumiwa kifungo cha maisha.

Kwa makosa ya uhani vifungu vinaelekeza kwamba adhabu yake ni hukumu ya kifo. Mahakama inatamka kwamba hiyo ni adhabu ya juu kabisa kutolewa kwa makosa hayo. Uhaini ni pale mtu au kikundi cha watu wanapofanya uhalifu dhidi ya nchi yake kwa mfano kupindua uongozi, usaliti, kutoa siri za nchi kwa maadui na makosa yanayofanana na hayo.

Kabla ya uhuru wakati wa ukoloni ni dhahiri kuwa adhabu hizo zilikuwa zinatekelezwa hata kwa makosa madogo. Ni vigumu kuwa na takwimu sahihi lakini adhabu hizo zilipungua baada ya kupata uhuru. Inafahamika kwamba baada ya uhuru hata sasa muda mrefu utekelezaji wa adhabu hiyo umeendelea kupungua.

Ikiwa watu waliotawaliwa walikuwa wameshazoea mfumo fulani wa sheria, kuwaondoa moja kwa moja kwenye mfumo waliokuwa wamezoea kunaweza kuleta athari sana kwenye jamii. Ni vyema utafiti ukafanyika kuchunguza na kujua mabadiliko hayo yameathiri kwa kiasi gani jamii husika.

Jambo muhimu la kwanza kabisa kufanya ni kubadilisha sheria hii iweze kuwa na wigo mpana kwa makosa ambayo yanatendeka mara kwa mara na ambayo yanapoteza rasilimali za taifa kwa kiwango kikukubwa. Kwa mfano wizi wa fedha za serikali au kusababisha hasara ya mabilioni ya fedha kwa lengo la kujinufaisha

La pili ni kuweza kutekeleza adhabu hizo baada ya kubadilisha sheria. Hali hii itapunguza wengi kutenda makosa kama hayo. Hivyo taifa litaweza kuwa na fedha za kutosha kutekeleza mipango yake ipasavyo na kuwa na maendeleo au kufikia lengo husika.

Mapendekezo haya yanaweza kuwa kwenye makosa makubwa kwa mfano, ugaidi, usambazaji wa dawa za kulevya, ubakaji, na uhalifu wa kiuchumi. Hili linaweza kuthibitika kwenye mataifa makubwa yaliyoendelea kama Marekani baadhi ya majimbo, China, Japani na nchi nyinginezo

Adhabu hii itazuia wahalifu waliokubuhu kuendelea kufanya makosa Zaidi lakini pia kuzuia wahalifu wasifanye makosa yaliyowekwa kwenye adhabu hii, vilevile itatoa haki kwa familia na watu waliothirika na vitendo vya uhalifu.

Kwa mfano mtu anaiba fedha za serikali. Je ni watu wangapi amaezua huduma ya afya isiende kwao? Amezuia barabara kiasi gani zisijengwe, amezuia shule ngapi zisijengwe, amezuia huduma ngapi zisifike kwa wanachi? Maji, umeme, na huduma nyinginezo? Unadhani kwa kufanya hayo atakuwa ameangamiza watu wangapi? Amewapa umaskini wangapi na ameua wangapi?

Pitia ripoti za ukaguzi wa fedha za serikali uone ni kiasi gani cha fedha na mali zimepotea. Ni dhahiri kwamba upotevu huu tukiwa na sheria kali utaweza kudhibitiwa, na ikiwa kweli itathibitika, mfumo wa utoaji haki ukafanya kazi yake vyema ili wahusika walipe na kuhukumiwa kwa haki.

Ni dhahiri kila siku kwenye vyombo vya habari tunasikia habari za ukatili wa hali ya juu, vitendo vya kinyama vikifanyika, ikiwa mabadiliko haya yatafanyika, vitendo hivyo vitaweza kupungua kwa kiwango kikubwa sana na hivyo kuleta ustawi katika jamii.

Je? Lipo jambo moja ambalo linaweza kufanyika kuleta mabadiliko hayo? jibu ni ndiyo, hakuna jambo ambalo halina ufumbuzi.

Ni jambo la kufurahisha sana ikiwa umesoma andiko hili mpaka kufikia hapa, kwa heshima kabisa ningependa kusikia kutoka kwako. Lakini ikiwa nimekukwaza nisamehe, nirekebishe, maana kujifunza ni pande mbili. Inawezekana kabisa kwa kukusanya mawazo ya wengi tukapata kilicho bora kabisa. Nizidi kukushukuru sana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom