Hukumu dhidi yangu: Shukrani kwa watanzania – Maxence Melo

Status
Not open for further replies.
Ramark,

Mkuu hongera kwa bandiko zuri. Ila una matatizo ya matumizi ya herufi H kwenye uandishi wako. Hata jana kwenye ule mjadala wetu niliona hilo kosa nikadhani ni spelling error, ila sasa nimejirisha kuwa una tatizo la wapi pa kuweka herufi H na wapi sio pa kuiweka.

Mfano hapo uliposema husitetereke, neno sahihi ni usitetereke. Hapo uliposema husijifungie ndani, neno sahihi ni usijifungie ndani. Nje au hapo una uwezo mzuri wa kujenga hoja. Jitahidi kurekebisha hilo ili watu makini wasikinai maoni yako
 
Sasa wenye akili za Zero IQ Mbadilike mtupe maada zenye maana. Mkuu anatupambania, nitakuja kuchapa mtu ban humu.
 
Hapana, hakimu amesema kuwa hakukuwa na ulazima wa kutoa data hizo ila akahitimisha kuwa niliwazungusha sana Polisi hivyo kuzuia upelelezi wao.
Kwanza poleni sana..! Mimi siyo mjuzi wa sheria lkn nadhani hakimu alikuwa sahihi. Hakimu kawaambia mliwachelewesha police, ungewaambia tu huna hizo taarifa badala ya kusubiri kujiridhisha kujua jinai ya wateja wenu. Kwa maoni yangu mlijichanganya wenyewe kuwapotezea muda police.
 
Kwanza poleni sana..! Mimi siyo mjuzi wa sheria lkn nadhani hakimu alikuwa sahihi. Hakimu kawaambia mliwachelewesha police, ungewaambia tu huna hizo taarifa badala ya kusubiri kujiridhisha kujua jinai ya wateja wenu. Kwa maoni yangu mlijichanganya wenyewe kuwapotezea muda police.

Wala kuchelewesha halikuwa tatizo, bali hiyo imechomekewa tu ili ionekane kulikuwa na kesi na sio nia ovu, ila lengo hasa ni kuitia woga jf ili iwe inamwaga taarifa za watu wasioofagilia serikali, ili wakafanyiwe kitu mbaya. Ufahamu kuna kesi nyingine ya kubumba hivyo hivyo, nayo haina shahidi mpaka leo! Lengo hasa ni kuzuia vitu vyenye ncha kali dhidi ya serikali humu jukwaani.
 
Simbaaaa atakaa kwenye vitabu vya historia ...
Kuna maisha baada ya ....., kuna upweke mkubwa unafuata muda huo.

Pole ndugu Maxence Melo
 
Pole Sana ndugu, tutavuka salama tu kwenye kesi zilizosalia, inshaallah!!
 
Naungana wengine kukupa pole na matatizo yote unayo na uliyopitia.
Kuna mstari wa utetezi wako unanipa mashaka kidogo, unaposema polisi wathibitishe jinai ya mteja ndio uwape taarifa. Una maana unataka polisi wawe mahakama au ianze kumuhukumu mtu bila kufanya uchunguzi? Polisi hawawezi kuthibitisha jinai zaidi ya mahakama kaka, so hapo ulikuwa wrong.

Vilevile unapima vipi ukweli wa taarifa zinazoletwa humu? hii itasaidia kuyokuingia kwenye matatizo otherwise utakuwa umejitwisha uwakili na umahakama kwa kuwahukumu wengine bila kusikilizwa? . je ni vii platform inakuwa sio bias?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom