Huko Makumira chuo cha Uchungaji hakufai/Hali ni tete..!

Nicksixyo

JF-Expert Member
Jan 11, 2011
944
263
Kwa habari nilizozipata muda sio mrefu kuanzia jana hadi leo pamekuwa na maandamano na vurugu za wanachuo baada ya mwenzao mmoja kugongwa na gari hapo nje ya geiti ya chuo.Wamekuwa wakiomba serikali isikie kilio chao cha kuweka bansi eneo hilo baada ya kuwepo kwa matukio mengi ya ajali,bila ya mafanikio.

Hatima na machungu yao imefikia ukingoni jana baada ya mwenzao mwingine kugongwa na kufia hapohapo njia. Wachungaji maaskofu na wote waliopo katika chuo hicho kwa masomo yao wameamua kutoka kudai haki yao ya kusikiliza na serikali kwa kuzuia magari yote yapitayo njia hiyo kuu ya Moshi - Arusha.

Waliopo maeneo hayo tunaomba mfuatilie tukio hili mtuletee habari zaidi kwani bado hali ni ya kuviziana kati ya polisi na wanachuo hao. Polisi wakifika hawaoni mtu lakin wakiondoka magari yanayopita hapo yanapigwa mawe na kuwekewa vizuizi barabarani. Nchi imekuwa mtafaruku...Nawakilisha.
 
HAbari yako si mbaya, ila heading ni ya Chokochoko!
Makumira si chuo cha Maaskofu na Wachungaji bali chuo conventional cha Elimu ya Juu kwa mtu yeyote eligible!
Tunapotoa habari ya kuijuza jamii tusiweke vitu vitakavyopoka uzito wa habari zetu na kuonekana vyenyewe ndiyo vya mvuto zaidi!
 
Msaada tafadhali ... Hii habari ni tofauti kiasi gani na ile ilipokuwepo hapa jana? Is there anything different...A new different event?
 
We hata ukisema ni cha kikatoliki hayo ni mapungufu yako na uwezo wako wa kufikiri ndipo ulipo ishia,wenzio wanakulu shavu na degree then maisha yanakua simple na wanakua global,itikadi yako ndio umaskini wako
 
HAbari yako si mbaya, ila heading ni ya Chokochoko!
Makumira si chuo cha Maaskofu na Wachungaji bali chuo conventional cha Elimu ya Juu kwa mtu yeyote eligible!
Tunapotoa habari ya kuijuza jamii tusiweke vitu vitakavyopoka uzito wa habari zetu na kuonekana vyenyewe ndiyo vya mvuto zaidi!
Weee..Pale wapo watu wanaenda kusafisha vyeti vyao wachungaji na maaskofu wapo wote wanabrash elimu yao ya thiologia..Tembele uone na ujue.Istoshe heading yangu haijaweka Neno "Maaskofu" soma kwa makini,ila nimesema waliopo walikuwa katika swala zima la kudai haki zao.SOMA VIZURI.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom