MSAGA SUMU
JF-Expert Member
- May 25, 2015
- 6,488
- 20,444
Juzi wakati nikitoka Kaliua kwenda Mpanda katika kuchimba madini tulikatiza mto Ugalla.
Wenyeji wa maeneo hayo walinipa taarifa kuhusu malkia wa Ugalla anayekaa ndani ya mto Ugalla.
Malkia akikasirika huwa anaujaza mto Ugalla maji mpaka unavunja kingo zake na kukata mawasiliano kabisa kati ya pande mbili za mto. Miaka michache ya nyuma alikasirika sana na kuamua kusomba reli yote na maji. Mainjinia kutoka pande zote za dunia na nchi kila walipojaribu kujaza mawe yote yalisombwa mpaka walipoamua kumrushia sarafu mtoni ndipo alipowalegezea na hatimaye kukamilika na usafiri kurudi kama kawaida.
Wachimbaji wote tunaolekea Mpanda kuchimba madini lazima tufike mtoni na kurusha sarafu ili kupata baraka na ruhusa. Kwa kila sarafu unayorusha basi utafanikiwa kupata kama nusu kilo ya madini.
Kwa bahati nzuri mimi nilikuwa na begi la sarafu kwa hiyo nategemea kupata kilo kadhaa za madini ambazo thamani yake itafikia bilioni kadhaa.
Asante sana malkia wa Ugalla kama utani hivi utajiri nje nje.
Karibuni sana hifadhi ya Ugalla wadau.