Huduma ya TIGO PESA isitishwe ili wajipange upya;

MC

JF-Expert Member
Oct 5, 2007
762
188
Kwanza kabisa niwapongeze TIGO kwa kuwa moja ya mitandao yenye wateja wengi mijini na vijijini, pia niwapongeze kwa kuona uwepo wao hapa JF. Pia napenda kutamka wazi kuwa kuna thread nyingi zimezungumzia kero za mitandao ya simu mbalimbali hapa Tanzania. Naomba ieleweke wazi kuwa Swala langu siyo TIGO kwa ujumla ila ni ‘TIGO PESA'
Nitaongea kwa kifupi bila maelezo marefu ni kwa nini TIGO isitishe huduma zake za TIGO PESA, na nitaongea kwa mifano halisi (Evidence based justifications)
1. Mimi ni Wakala wa Tigo pesa pamoja na mitandao mingine, lakini TIGO pesa inasua sua sana kiasi cha kusababisha mzozo kati ya mteja na Wakala.
1.1 Mfano, mtandao wa TIGO unaweza sema utaratibu wa kuhamisha pesa kati ya mteja na wakala umefeli, ila hali halisi inakuwa kinyume, kwamba mmoja kapata au kakatwa pesa bila kujua.
1.2 Upatikanaji wa Customer care na majibu yao; hapa ni kichekesho kikubwa, utaratibu wa pesa kwenye mitandao ya simu ni utaratibu wa kibenki, umakini mkubwa unahitajika kudhibiti wizi, ukoseaji wa bahati mbaya n.k. katika kutimiza hilo mitandao inatakiwa iwe na timu ya watu ambao wako ‘standby' kwa ajili ya kupokea taarifa na malalamiko mbalimbali ikiwa ni pamoja na kusitisha pesa iliyotumwa kimakosa kuchukuliwa na mtu ambaye si mlengwa. Tatizo kubwa ni Customer care ya Tigo Pesa ambao unaweza wapigia kwa masaa kadhaa kabla hujafanikiwa issue yako.

2. Umakini katika majina, wakati ni jambo la kawaida sasa kwa mitandao kukosea speling za majina ya watu, kwa upande wa TIGO Pesa Unaweza ukasajili namba, ukianza kutumia huduma jina likawa lingine kabisa tofauti na lako, lakini pesa inakuja na kutoka kwako. Mimi limenitokea hilo ‘live' na si kwamba nasimuliwa.

3. Mtandao kuwa chini mara kwa mara, Ukienda kwa mawakala wengi wa TIGO pesa, watakuambia wazi kuwa mtandao wa tigo pesa unabadilika badilika, unaweza kuwepo na kutoweka wakati wowote, leo nimeacha pesa yangu kwa wakala nilipoenda kutoa pesa huku niliko Arusha baada ya mimi kuonekana kuwa nimekatwa pesa ila yeye hajapokea message yeyote na wala balance yake haijabadilika. Kujaribu kuwapigia customer care ilikuwa kama kupoteza muda
Kuna mambo mengi sana ambayo TIGO PESA wanavulunda, nimeona niseme machache hayo na kutoa ushauri wa bure kwa TIGO pesa, isilazimishe isichokiweza, au wabadilike. Iko siku database yao itapoteza kumbukumbu na hapo ndio issue ya ' kama DECI' inapokuja.

MC.
 
  • Thanks
Reactions: aye
Hii ni kweli kabisa, mfano mimi jana niliingia hasara baada ya ku-transfer pesa mara mbili kwa Mzee wangu wakati ilishaniambia transfers zimefeli zote, hapa najifikiria jinsi ya kumwambia anirudishie nusu wakati alishaniambia ana shida!!!
Nimejaribu kuwapigia Tigo Customer Care toka jana ili wanirudishie kimyakimya but hawapokei!!
But Voda nao salama sana maana zina kawaida ya kurudi zilikotoka kimyakimya bila taarifa ambapo mara kwa mara hupelekea mabishano kati ya mtumaji Na mtumiwailji.
 
kwakweli mimi pia ni wakala wa tigo pesa hawa jamaa hawana msaada wowote kwetu wakala na pia mteja hasa kwene upande wa customer service. very very poor na inatia hasara sana mana unapokesea hamna msaada unaoupata toka kwao ni bora voda unawapata na ela yako inarudishwa jipangeni upya wateja wanawakimbia kwa kukosa msaada.
pia system zenu Tigo si za uhakika unarusha fedha inakwambia imeshindikana mteja anaondoka after ten min fedha inaondoka kwenda kwa mteja mteja keshaondoka hasara tupu mngejipanga kwa hilo kwanza jamani enyi Tigo
 
kweli tigo pesa wanazingua sana mm naweza kununua salio la elfu moja wakaniambia mtandao unasumbua naweza jaribu kama mara 3 bt baada ya muda mfupi unakuta wamekuongezea elfu 3 wakati hukuwa na budget hiyo na pia mtindo wa kukopeshana sh 1300 sio ishu ni hela nyingi sana en hela ya kukopa inaisha fasta sana
Ishu nyingine simu inasalio nikimpigia mtu inamtumia ujumbe wa tafadhali nipigie
 
Back
Top Bottom