Huduma ya Tigo Bima ikoje? Kuna mtu amewahi kunufaika nayo?

babu jeje

Member
Jul 16, 2023
27
18
Poleni na majukumu ya leo.

Leo nimepokea simu toka Tigo Bima kisha wakanieleza juu ya hizi huduma ambazo nitanufaika nazo pindi nitakapota matatizo.

Je, kuna aliyewahi nufaika na hii huduma kwamba hakuna longolongo? Je, mteja atapata pesa yake kwa wakati baada ya kupata ugonjwa na kulazwa? Kuna aliyewahi nufaika?

Naomba mnijibu.
 
Hapo kama Kuingia kwenye Mtumbwi wa Vibwengo,

Tigo Bima,Nina ushuhuda wa mtu wangu wa karibu yeye alikuwa akilipa kilamwezi kupitia namba yake ya simu ya Tigo Pesa,Kwanza Tigo sio mtoa hiyo huduma ya Bima hivyo kuna kampuni tofauti Hila wao wanawatumia Tigo kama kuitangaza huduma ya Bima, Mlengwa Baada ya kupata Ajari alilazwa Hospital,Baada ya kupata nafuu alifika Ofisi za Tigo kupata Muongozo,Alipo fika Ofisi za Tigo alipewa namba za hao BIMA,awasiliane nao kupitia WhatsApp,Baada ya kuwasiliana nao atume Taarifa za MEDICAL REPORT, DISCHARGE FORM,POLICE FORM,NIDA,Na Documents nyingine alizo fanya Malipo.Baada ya majibu yake kupewa hao TIGO BIMA,wamesema Wana Daktari wao wa kupitia hizo Taarifa walicho mjibu ni SIKU ALIZOLAZWA HAZIENDANI,HIVYO MADAI YAKE HAYATAWEZA KULIPWA.Kwa hiyo BIMA Haikuwa na Msaada wowote kwake amepoteza pesa za Bure na amelipa zaidi ya Miaka Minne,
Kama Kuna mtu mweye Ushuhuda aendelea kushusha NONDO.
 
Duh! voda bima vp au zote za mchongo tu.
Kwa Voda bima,sijapata Ushuhuda haya kwenye mambo mtu anapopatwa na Ajari,navyofahamu Mimi Voda wao bima yao kwa Ushirikiano wa Jubilee Insurance,Mo Assuarance na Milvik Tanzania,Kwa Mimi kwa Ushauri bima isiyo kuwa na Mkataba wa kimaandishi umeongea nao tu wakakushawishi kupitia simu sio, Mkataba lazima usomwe na Usainiwe hili, Tatizo linapotokea uanzie na Mkataba wenyewe kwanza.
 
Back
Top Bottom