Huduma mbovu zitolewazo Hospitali ya Rufaa mkoa wa Shinyanga

FCR

JF-Expert Member
Nov 7, 2018
213
177
Leo tarehe 11.06.2019 Kuna mgonjwa ameletwa tangu majira ya saa Saba mchana baada ya kufikishwa Kama kawaida alipitishwa kwa daktari ili daktari amuone hali yake pamoja na kuchukua particular zake. Baada ya kumuona daktari aliamuru mgonjwa apewe kitanda kulingana na hali yake ,shida inakuja hivi tangu mgonjwa amepewa kitanda alipewa paracetamol tu hata hivyo vipimo walimchukua vya mkojo na damu hadi Sasa hajapata majibuKumbuka muda huu ni saa tano usiku kasoro nne.

Mimi nilichojiuliza labda huenda vipimo vimechelewa kwa sababu wagojwa ni wengi pili kwa uzoefu wangu vipimo Kama hivyo saa moja haipiti bila kupewa majibu!

Hata hivyo labda mgonjwa amefanyiwa nongwa kwasababu ya bima yake!

Nachokiona takukuru wanakila sabab za kutembelea taasisi Kama hizi kujuwa huduma zitolewazo!

Mgonjwa yupo hoi bini taabani hajui hatima yake ya magonjwa yanayomkabiri (nimejaribu kumuuliza nerse kuhusu mgojwa huyo anasema tangu ameingia zamu hajaona dawa za mgonjwa huyo.
 
Hospital zote za Serikali ni njia ya kwenda kuzimu, ukienda ukiwa na hali mbaya na ukarudi salama bila wauguzi wako kotoa pesa ya kiwi, basi fanya ibada ya shukurani.
 
Mimi nitamtetea daktari. Shida ya ninyi relatives wa wangonjwa mnadhani daktari ni nabii atapata ufunuo papo kwa papo kuhusu tatizo la mgonjwa. Daktari anahitaji mda wa kutosha kuchukua comprehensive history ya mgonjwa ili aje na diagnosis sahihi. Mgonjwa wako kapewa paracetamol coz either yuko na pain au fever. Halafu kuwahi au kuchelewa kwa vipimo vya maabara hutegemea mgonjwa amewekwa kwenye category ipi? Je, ni emergency, urgent au kawaida?
Kama mgonjwa wako kawa mismanaged zipo mamlaka husika. Unaweza enda kwa ofisi ya mganga mkuu au muuguzi mfawidhi malalamiko yako yakasikilizwa.
Hospitali za serikali za mikoa na wilaya zote zinafanana
 
Nasimama na wewe.
 
Leo tarehe 11.06.2019 Kuna mgonjwa ameletwa tangu majira ya saa Saba mchana baada ya kufikishwa Kama kawaida alipitishwa kwa daktari ili daktari amuone hali yake pamoja na kuchukua particular zake. Baada ya kumuona daktari aliamuru mgonjwa apewe kitanda kulingana na hali yake ,shida inakuja hivi tangu mgonjwa amepewa kitanda alipewa paracetamol tu hata hivyo vipimo walimchukua vya mkojo na damu hadi Sasa hajapata majibuKumbuka muda huu ni saa tano usiku kasoro nne.

Mimi nilichojiuliza labda huenda vipimo vimechelewa kwa sababu wagojwa ni wengi pili kwa uzoefu wangu vipimo Kama hivyo saa moja haipiti bila kupewa majibu!

Hata hivyo labda mgonjwa amefanyiwa nongwa kwasababu ya bima yake!

Nachokiona takukuru wanakila sabab za kutembelea taasisi Kama hizi kujuwa huduma zitolewazo!

Mgonjwa yupo hoi bini taabani hajui hatima yake ya magonjwa yanayomkabiri (nimejaribu kumuuliza nerse kuhusu mgojwa huyo anasema tangu ameingia zamu hajaona dawa za mgonjwa huyo.

Serikali ya awamu ya 5 imebadilika? Si tunaambiwa kila siku kuwa huduma zimeboreka sana siku hizi kutokana na uongozi uliotukuka? Hao wote yafaa watumbuliwe maana wanashindwa kwenda na kasi ya Mheshimiwa Rais wetu mtukufu.
 
Sio kila mgonjwa anapata ‘emergency ‘ treatment. Lazima atakuja kuonwa haswa wakifanya ‘ward round’
 
Shida siyo kulazwa ward namba ngapi kwa sababu navyowajuwa watanzania wakishamjua mgonjwa wataanza kumkoromea mgonjwa kwanini unatuchoma kupitia kwenye media watamhoji anayekuja kumuona ninani badala ya kumfariji hata hiyo paracetamol ataikosa kimsingi daktari anawajibu wa kutembelea wagonjwa wake kujua aliyepata unafuu na malalamiko aliyonayo ma nerse wanaweza kuwa wanampa taarifa kuwa wagonjwa wanaendelea vizuri kumbe hamna!
 
Kama huamini nurses tufanyeje sasa? Unataka daktari ashinde wodini na mgonjwa?
 
Sio kila mgonjwa anapata ‘emergency ‘ treatment. Lazima atakuja kuonwa haswa wakifanya ‘ward round’
Ndiyo. Ataonwa during service ward round hii ni kila siku na pia major ward round ambayo ni mara moja au mbili au zaidi kwa wiki inategemea sera ya hospitali na idadi ya staff
 
Kwa kuongezea sio kila mgonjwa ni kukimbiza hospitalibya rufaa ya mkoa,je mlianza kwenye vituo vyenu vya afya au hospitali ya wilaya? Hospitali za rufaa za mikoa zinapokea wwgonjwa wwnaohitaji matibabu ya kibingwa,ambao wameshindikana ktk vituo vua afya na hospitali za wilaya. Siku nyingine anzia huko. Usiweke jam hospital kubwa kwa shida ambayo inaweza kutatuliwa hospitali za chini
 
Labda kaonyesha dalili za homa ya dengu, na hyo paracetamol na maji ndo dawa 😀 😀
Tchao, Muuza Nyanya Kijijini Doma
 
Back
Top Bottom