How much truth can you handle? Je waeza kuhimili ukweli wa mpenzi kiasi gani?!

chiko

JF-Expert Member
Feb 24, 2010
580
245
Nina rafiki yangu, yuko majuu kutafuta riziki, kaacha mke Bongo, jamaa ataka kila mara akimpigia simu mkewe, aambiwe kila kitu na mkewe, katongozwa, kachokozwa na watu na kila udaku mtaani. Mke hapendi na kanishtakia kwangu, mimi nikamuuliza swahiba, vipi haya mambo, utakuja zirai ama upate ugonjwa wa moyo, bwana kanambia, afadhali nijue hayo mambo kabla masela wanitangazie mitaani!!, kaongezea kuwa ashamwambia mkewe vibinti vyoote alivyo pitia akiwa hapa mtaani!!!.Yaani ametubia na hatarudia tena. Nilishtuka na sikua na la kusema.

Jamani wana jamii, ni bora kutoa ukweli wooote bila kuficha????, kuna ukweli mwengine mwenzio hawezi kuuhimili
 
Huyu rafiki yako yatamshinda mapema sana,yeye yuko huko majuu anayataka ya bongo anayofanya mkewe yeye alikua mchotaji mzuri ndio mana anaona mkewe atachotwa na wenzie,mwambie atulize roho yake tena ikizidi amwambia condom asisahau ndio muhimu kumchunga sana ndio atamfanya afanye vitu kwa sababu ya vituko vyake vyakumchunguza na watagombana kila siku.....
 
ukweli mwingine ni hatarishi kwa wapenzi ni bora hayaache tu na pia amuamini mkewe.
 
Huyu rafiki yako yatamshinda mapema sana,yeye yuko huko majuu anayataka ya bongo anayofanya mkewe yeye alikua mchotaji mzuri ndio mana anaona mkewe atachotwa na wenzie,mwambie atulize roho yake tena ikizidi amwambia condom asisahau ndio muhimu kumchunga sana ndio atamfanya afanye vitu kwa sababu ya vituko vyake vyakumchunguza na watagombana kila siku.....

Wasema kweli AF, mimi naona huyu bwana ataka kidonda cha moyo, alimkazania mpaka mke kamwambia kua shemegi ya Rafki yangu, mume wa dada ya bwana pia kesha mtongonza mke!!!!!!!
 
Siku zote mwizi huhic naye anaibiwa,mbona kabla hajaondoka hakuwa akimweleza mkewe ishu zake na hao mabint sasa kwa vile alikuwa mwizi anajihic naye anaibiwa kwa vile hayupo,mwambie atulie na kutafuta hela huko,kuuliza uliza kunaweza kumtia mawazo huyo dada wa watu na mpaka akapata hasira na kuamua kulipiza kisasi!
 
Aambiwe yote madhali anataka. Mtu mzima akisiwe dose kwa lipi?
Yakimshinda atasema basi
 
Nafikiri rafiki yako sio kuwa anataka ukweli kwa nia njema.
Hata hapo alipomweleza mkewe anayotenda ughaibuni, dhamiri yake ni kutafuta pa kutokea ili amtelekeze huyo dada.
 
Back
Top Bottom