Hotuba yangu jimboni Kigoma

Hapo ndipo Zitto onapoonyesha kuwa una uwezo wa kuelewa mambo, nakumbuka sana nilipokuwa KGM jinsi hali ya bara2 ilivyokuwa mbaya, hakika wanakigoma wataendelea kukumbuka siku zote kwa kuwaletea barabara.
 
Shapu,

Huyu ndugu Ogah msamehe..namuamini waga ni mtu makini sana. Sijui hii hoja leo ameingalia kwa kutokea kipande ipi. Otherwise hoja zake ni makini.

Nadhani muungwana Ogah hajawahi fika Kigoma na hii mikoa iliyo pembezoni mwa nchi yetu ajue hali halisi.

Ogah umeshaambiwa... tangu uhuru almost nusu Karne..Kigoma haijawahi kuwa na barabara ya lami!!!!!..sasa sijui kama hiyo serikali unayoisema ilikuwa likizo ama vipi.

Masanja:

Hile posti yako ya mwanzo katika thread imenikumbusha mbali sana. Nadhani wengi wetu hawajafika intilia za Tanzania na kujionea politics za huko.
 
Wakubwa salaam,

Ninawaletea hotuba yangu jimboni Kigoma. Asante


HOTUBA YA MBUNGE WA KIGOMA KASKAZINI NDUGU ZITTO ZUBERI KABWE KWENYE UFUNGUZI WA MKUTANO MKUU WA CHADEMA UCHAGUZI JIMBO LA KIGOMA KASKAZINI.


KALINZI, AGOSTI15, 2009.


Ndugu wajumbe, ninayo heshima kubwa kuwashukuru kwa jitihada mlizofanya kuhakikisha leo karibu viongozi wote wa vijiji vya jimbo la Kigoma Kaskazini tunakutana hapa kata ya Kalinzi kwa ajili ya Mkutano Mkuu wa CHADEMA. Natambua kuwa mnafanya kazi katika mazingira magumu, lakini mnafanya mambo makubwa sana..........


Asanteni kwa kunisikiliza.

Kabwe Z. Zitto, Mb
Mbunge wa Kigoma Kaskazini,
Kalinzi, 15/8/2008.

Mkuu Zitto je tarehe ya kwenye signature yako ni sahihi? Nadhani ni 15/08/2009.
 
Je huoni ulichofanya ni usaliti kwa wananchi wa maeneo mengine na kujifikiria wewe peke yako ubunge wako na wananchi wako pekee? Utaalamu wa kufumua bajeti umejifunzia wapi? Waamini ulichofanya ni sahihi?.

Mkuu kama wananchi wanawaweka wabunge sio wapiganaji wataendelea kula jeuri yao Tumechoka kuendelea kuwasemea kila kitu wanachagua Mbunge makazi na kitu chake Kipo Dar atawakumbuka vp kama anaonekana mara moja kwa kipindi cha uchaguzi na wananchi wanaridhika waache waendelee kuteseka si wameyataka wenyewe maana wananchi kila ukiwaelimisha tumia haki yako ya kura kupata maendeleo wao wanakimbilia kule kule ambako kwenye shimo na wanasalitiwa miaka nenda rudi Mbunge anashindwa hata kuitisha harembee jimboni kwake angalau wajenge shule! Bravo Zitto endelea kupigania haki za wapiga kura wako.
 
Masanja:

Hile posti yako ya mwanzo katika thread imenikumbusha mbali sana. Nadhani wengi wetu hawajafika intilia za Tanzania na kujionea politics za huko.


Mkuu ndo maana naamini mazingira tunayokulia yanatu-affect mbeleni. Ndo maana sielewi kwa nini watu waliokulia kwenye shida, WAKASOMA SHULE ZA WAMISSIONARY..leo tunawapa madaraka wanatusaliti. Kwa sababu hawa jamaa..na jeuri yao sasa..lakini walistruggle sana (baadhi) kufika walipo. Kwanini wasikumbuke walikotoka? Imagine mtu kama Mkapa..leo eti ni fisadi..Huyu Chenge..ni jirani yangu kabisa..anatoka familia choka mbaya kama wengi wetu humu..duh..hali inatisha..

Hii inanifanya niogope...itakuwaje hii nchi wakikabidhiwa watoto wa hawa mafisadi ambao wamekulia Oysterbay na Masaki? Kusoma wamesoma IST na Ulaya?? TANZANIA yao wanaoijua ni ile ya Dar Es Salaam? (akienda mbali ni Moshi na Arusha?). KAZI TUNAYO WADANGANYIKA...

Huu mjadala wa barabara ya Mwandiga na Manyovu..una expose mambo mengi sana. Watanzania wengi Tanzania halisi hatuijui. Mtu anadhani TZ ni Dar-Tanga-Moshi-Arusha. na sana sana Mwanza...Jamani kuna Tanzania nyingine ambayo ndo mh. Zitto anaiongelea hapa...na hiyo haijulikani!

na kuna Mwandiga-Manyovu nyingi tuu..sema hazina akina Zitto wa kuzisemea kunakohusika..
 
Dilunga umekuja "kuchafua hali ya hewa hapa nahisi,anyway kutoa maoni yako ni haki yako ya msingi na ipo ndani ya katiba!

Zitto kaza mwendo mkuu;tukijipanga vyema NEC-CCM itakutana sana 2011 kupanga tena kumdhibiti Spika,na wala si kukutana kupanga waone jinsi gani wataleta maendeleo kwa watz maana upinzani utakuwa unadhibiti bunge!

Tunahitaji akina Zitto wengi bungeni!

Malafyale
Mkuu ahsante kwa kutambua kwamba CCM itakuwa tena chama tawala 2010 na NEC-CCM itakutana 2011 kujadili jinsi ya kumdhibit spika...uhh...!!!

CCM kiboko yani hata ukijaribu kufurukuta unarudi palepale kwamba kitabakia kuwa chama tawala....

Zitto kaza buti ila usisahau where the leaders are!!??
 
Ogah,
Mkuu wangu tafadhali!...Swala la kuwapongeza Chenge na mama Meghji ni ustaarabu mkubwa hata kama watu hawa ni mafiisadi kwani Zitto hakupokea fedha toka mfuko wa mafisadi hao ila shukran anazitoa ni Upande wa pili wa wahusika hao hao kiutendaji kazi.

unajua fika kwamba ktk lugha ya ustraabu ya kisiasa ni lazima Zitto atoe shukran zake kwa viongozi waliokuwa madarakani na walimsaidia kuwezesha yaliyopatikana.
Ubunge Tanzania mkuu wangu ni Utumwa wa kimawazo, utalazimika kumwomba shetani kwa ajili ya watu wako kwani ukikaa mbali na mawaziri au taasisi zinazohusika na ahadi ulowapa wananchi wako mkuu wangu utakesha.

Kwa maana kwamba Ukienda Zimbabwe na ukapokelewa na Mugabe itabidi umshukuru Mugabe ktk hotuba zako mahala popote kwa fadhila zake..Kuna watu nawafahamu sana waliwahi kuishi kwa Idd Amin na wanamsifia ajabu kwa yale alowawezesha wao na sehemu zao siwezi kuwaita wajinga kwa sababu ya historia kubwa ya Idd Amin..kwani mkosefu hapa ni Idd Amin kwa madhambi aloyafanya na sii ukisha kuwa fisadi basi imekuwa laana kwa wote..

Ni wajibu wa CCM kupanga mikakati ya maendeleo ya Tanzania nzima, lakini ni watu wanaofikisha maendeleo hayo kwa wananchi hivyo haijalishi kuwa ni Chenge au Mwandosya aliyeshika mpini.. kumbuka tu ni yule aloyeshika mpini ndiye mwamuzi wa jembe litakita wapi ili upate kupandikiza mbegu..na wakati huo Chenge na Meghji ndio walioshika mpini, amsifie nani zaidi ya ukweli?..

Kisha Kisiasa ni lazima Zitto atambue WATU ktk MAZINGIRA.. wananchi wote (watu) ni ktk NDIVYO TULIVYO, ambao ni Reflection ya Viongozi wao..hapa ni lazima utumie lugha wanayoielewa wao..kuwa hata mwizi kama anajenga kwao huyo ni shujaa.
Kisha mazingira ya Kigoma na kutambua Ni majuuzi tu Pinda aliondoka jimboni hapo akijisifia kuwa ni serikali yake iliyowawezesha..Ni chama CCM kilichowawezesha kupata barabara hiyo, hivyo Zitto ni lazima awaambie wanannchi hatua alizochukua yeye hadi kufikia mafanikio ya barabara hiyo hata kama kuna mkono wa shetani. Ndio Ukweli na siku zote msema ukweli ndiye kipenzi cha Mungu kuliko Pinda anayeweza kupindisha Ukweli kwa wananchi ili mradi tu kumchafua Zitto.

Ndio hiyo Tanzania yetu babu, sasa hivi ni mateso matupu, na ukibahatika kupata afueni ya kusikilizwa ama kaupendeleo kama hako shukuru Mungu. Binafsi nampongeza sana Mh. Zitto kwa kuwa mfano bora kwa wananchi, Kwa sababu tumeipata hotuba hii hata kabla yeye mwenyewe hajaiweka hapa..na wala sii mara ya kwanza kupata hotuba za Zitto akiwa Kigoma.

Ni Ashirio moja kubwa sana kwetu kuwa Zitto anajali sana maslahi ya wananchi wake na hakika naweza sema sijaona Hotuba ya mbunge wala kiongozi mwingine yeyote ktk jimbo lake. Kwa hiyo tumpeni sifa zake...hakuna mbunge mwingine aliyefanya hivi na kwa Zitto sii mara ya kwanza kiasi kwamba tumeweza kufuatilia safari zake jimboni kwake na Tanzania nzima kuliko hata viongozi wa serikali tawala.
 
Last edited:
safi Zitto hotuba nzuri sana. Bravoooo, hamasisheni sana huko makwenu na kwingine mnakoweza ili Upinzani uimarike zaidi. Mko kwenye sala zangu
 
Hapo kusifia mimi binafsi sio tatizo lakini mbona wale wa upande ule wakisifia wanaitwa majina mengi sana?

Mfano Lowasa kafanya mambo kushughurikia maji ya ziwa victoria,hapa kosa aje mtu wa ccm amsifie kwa hilo.

Na hata hivyo mimi siamini na wala sitaki kuingia kwenye mkumbo wa kusifia watu wanaapotekeleza 1/1000 ya majukumu yao.

Nahisi itafikia kumshukuru mwalimu kwa kuingia darasani kufundisha kipindi chake
 
Bravo Mheshimiwa Mbunge Zitto Kabwe umefanya kazi nzuri sana.

Ndugu zangu kabla ya Zitto nani alikuwa Mbunge? ni vizuri tukijikumbusha aliyofanya yeye maana hapa wengine ni maadui wa mandeleo ya nchi.
 
MkamaP,
Mkuu wangu Zitto hakuwasifia Chenge na Meghji, ila kawashukuru kwa msaada wao. Tatizo la watu wengi wa CCM wanataka wananchi tuamini kwamba Mkapa alikuwa kiongozi mzuri, Lowassa, Chenge na mafisadi wengine wote ni viongozi wazuri hapa ndipo tunapogongana..kwani yapo matukio ambao tunaweza kuwasifia kina Lowassa ila tusiwapambe kuwa wao ni wasafi, viongozi wazuri kwa kutumia mifano hiyo. hapa wasomaji tutakuwa tunaitazama picha kubwa zaidi ya fadhila ndogo waliyoifanya.
Na mwisho mkuu wangu tanzania itabidi Umsifie mwalimu aliyehudhulia darasani kwa sababu nchi nzima ni kama vile ina Union iliyogoma..wee fikiria kuna Union ya walimu walogoma toka Nyerere alipoachia ngazi na contract haijaainiwa tena..Mkuu wangu elimu Tanzania sasa hivi ni deal ambalo hata nchi tajiri duniani haziwezi kuishi kama sisi. Nadhani Tanzania tuna lead duniani kwa kuwa na elimu ghali kuliko US, UK Canada aui nchi zote kubwa za Kibepari!..Sasa nambie utaachaje kumsifia mwalimu wa bure anapoingia darasani sii kama vile umeona Malaika wa Mungu akiingia..
Elimu ya Tanzania siku hizi wanasema ni negotiable! utaipata kwa uwezo wa mfuko wako yaani mind concept ya watu ni kwamba fedha inaweza kununua Elimu!
 
Last edited:
Sina wasiwawasi kwamba Mh. Zitto ni mchapakazi! Tena sana.

Ila Du! nimehudhunishwa na ugongwa ule unaosema Mbunge anafanya mambo fulani fulani kama Mbunge. Eti wabunge wanajenga zahanati, wanajenga shule, wanajenga barabara... etc. etc. na waliopongezwa mawaziri kupeleka barabara
Yaani kwa nchi yetu hakuna appreciation yoyote ya wataalamu wa mawizara na halmashauri... ati wabunge/mawaziri ndio wanaofanya.

oooo pu!!!!
 
Dilunga,

Naungana nawe 100%.

Mheshimiwa Zitto ametoa shukrani nzito sana kwa mafisadi kiasi cha kuwafanya wawe ni wa muhimu zaidi katika miradi hiyo kama vile walikuwa anatekeleza miradi hiyo kwa hiari yao. Ninadhani angewaambia wananchi wake straight kuwa alifanikiwa kuifanya serikali isikilize kilio chao na kutekeleza miradi hiyo anayotaja.


Mambo mengine aliyaweka vizuri sana isipokuwa hilo hapo ambalo Dilunga kaengua

Ndio maana tunasema Zitto anahitaji ukomavu wa kisiasa! Huwezi kuwasifia wapinzani wako tena wale ambao ni blacklisted! Pia unawashukuru nini wakati walikuwa wanatimiza wajibu wao? Wa kuwashukuru ni wananchi ama hata watendaji wizarani waliofanikisha kupatikana hicho kilichoweza kupatikana wizarani. Kwani angeliacha kuwataja ingelikuwaje? Afterall Chenge na Megji hawapo tena serikalini kusema kwamba huenda kuna siku ataenda kuomba msaada wa kiwaziri kutoka kwao! Big mistake to what might have been a good speech!
 
Je, ilikuwa lazima kuwashukuru hao, hasa Chenge na Mrema? Jamani alama za nyakati zinasemaje?
hivi kama kweli walifanya hayo mambo aliotaja zitto hawastahili asante japo kuwa wana maovu mengine? sidhani kuna ubaya wowote wa kuwapa asante yao hio inaonesha uungwana kwani hawa watu kama walifanya hayo kwa upande huo wana stahili kupewa hio asante na upande ule wamaovu wanastahili kukemewa.
 
Sasa hao wabunge wa mikoa ya kati ndo na wao wangehangaika wakapata barabara za kuwaunganisha na mikoa ya pembezoni kusudi wapiga kura wao wafanye biashara. Sijua RA mbunge wa Ndugu Sikonge anasikia huu ushauri wa bure?


Mkuu Masanja,

Kwanza sijui niseme Mwadila?

Sasa wewe na kufahamu kote Unyamwezini/Usukumani lakini Tabora huoni kitu? Umefahamu hadi kwa Zitto Kigoma? Sijui ulitumia Google Earth? Niseme ukweli hata mie nimechungulia huko. Ni kweli wenyeji wa Kigoma watakuwa wanakwenda Burundi kwa urahisi sana. Je wakumbuka zile Saa walikuwa wanauza wanafunzi wa Kigoma? Zile za kukonyeza........

Masanja mwana ...... Mie natoka Sikonge natoka wilaya/jimbo la Sikonge na mbunge wetu ni fisi fulani anayeogopa hata kivuli chake aitwaye Said Nkumba. RA ni mbunge wa Igunga na Igunga sijawahi hata kufika....
 
sehemu niliyopenda ni hio ya kutumia asilimia 30 ya mshahara wake kuwasomesha watoto wanaotoka lwenye familia duni.kama ni kweli huo ni mfano mkubwa wa kuigwa na wabunge wengine na zitto anastahili pongezi kubwa sana hapo kwa kuonyesha jinsi gani anawajali wananchi.sio kugawa gawa mipira na kanga alafu ukipata kura unatoweka.
 
Ahsante Kichuguu kwa kuliona hilo, aksante.

Zaidi ya Mkapa na Vithlani, hakuna kichwa kinachotafutwa Tanzania kikajibu shutuma za ubadhilifu kama kichwa cha Andrew Chenge.

Zitto Kabwe, mbunge kiongozi wa upinzani, ameenda kuwaambia wananchi kwamba kwa kushirikiana na Ephraem Mrema aliyeilipisha TANROADS Sh bilioni 3.3 kwa kampuni illegal ya Norconsult na Zhakia Meghji aliyesaini makaratasi ya Billal wa EPA, Andrew Chenge amewajengea mabarabara!

Kana kwamba kina Zhakia Meghji na Chenge walifanya hisani kutoa hela, hela zinazopita kwa idhini ya Bunge.

Unalalamika Buzwagi, Buzwagi, Buzwagi halafu wakina Chenge waliosaini mikabata unaenda kuwauza kwa watu? Unasimama mbele za wananchi wenye disapointment na frustration unataja ``Chenge`` kwa ufahari kabisa?

Labda ni Waganda walikasirika mwaka '79 wakatutafutia dawa, au Wakenya walinyunyiza kimiminika na helikopta ili tupwelee tuwaachie ardhi, lakini kuna mkono wa mtu, hatuwezi kuwa wazima. Anamsifu Chenge hadharani?

Watanzania tunajua sana plastic smile, hatuwezi kujieleza, halafu tuna a very complex communication system.

Kuelewa hiyo kauli ya Zitto inabidi uelewe culture yetu, hii culture inayomfanya mtu anayekufa na cancer kitandani akiulizwa unajisikiaje ajibu "najisikia vizuri".Kuna mambo fulani ambayo ni crucial sana -kama kum acknowledge mtu kama Chenge, regardless ya alichofanya- kwa sababu za ku play Mr. Nice Guy.This has more to do with our culture than Zitto personally.

But I wouldn't want to lose sight of the bigger picture due to this pandemic cancer afflicting the very fabric of our existence as a nation. Kwenye culture ya sounbyte society kumtaja Chenge tu watu wanaanza kuuliza "jamaa kawekwa mfukoni au vipi?"

Mimi nilifikiri watu tulivyoisema hotuba ya Zitto iliyomshukuru profusely Waziri Mkuu Pinda bila ya kuwa na sababu ya msingi, Zitto alielewa hii concept. Lakini inaonekana Zitto is too much of a philosophical above-politics "eminent criticism" policy wonk to sink down to our real-politik world (is this a compliment or dongo?)

All in all, after saying all that, kuna hoja na viroja, I don't wanna lose my trained sight on hoja for chasing viroja.
 
Back
Top Bottom