Hotuba ya Rais Mama Samia, nilivyoitafsiri

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,987
20,272
Hotuba ya Rais Mama Samia nilivyoitafsiri

Na Yericko Nyerere

Kwa mara ya kwanza kwa miaka 6 hivi nimeisikiliza hotuba ya Rais wa Nchi ambayo niliikosa kwa muda mwingi tangu kipindi kuanza kwa Bunge la Katiba na siku ya mazishi ya Hayati Nelson Mandela. Nilimiss sana hotuba ya Rais. Nimefokewa sana kwa miaka mingi. Naaam sasa naweza kushika rimonti ya Tv nikaweka TBC nikaangalia, Zamani nilibatiza jina kwamba TBC ni Tanzania Bustard Congregation. Naaam naiweka kwenye uangalizi angalau kwa miezi sita hivi mbele kabla sijaliondoa jina hilo na kurudi kuwa Tanzania Broadcasting Coparation.

Tuache porojo, turejee kwenye Hotuba ya Rais wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan aliyoitoa jana. Hotuba ilijaa mizazi yote ya kirais, Hotuba ilikuwa na haiba na mamlaka, na ilijaa hekima za kiutu wa pwani na bara. Mambo muhimu ambayo yalinifurahisha na yakanipa nguvu za kuitazama kwa jicho la uchambuzi, ni Vipaumbele vya Rais Mama Samia, Ambapo alitaja vipaumbele Sita ambavyo ni;

Kipaumbele cha Kwanza cha Mama ni Tunu za Taifa, hiki kipaumbele, kimekuwa kipaumbele cha marais wote waliopita,

Kipaumbele cha pili ni Kukuza uchumi mkuu na kuutafsiri kwa watu ili kuondokana na umasikini. Hii ni ingizo jipya ambalo naweza kusema limebomoa kabisa ile dhana ya maendeleo ya Tanzania ni Mabarabara, Mandege na maflaiova ambayo yalihubiriwa na utawala uliopita kwa nguvu zote hadi Magufuli akapiga marufuku kusema vyuma vimekaza (umasikini). Leo Mama anataka uchumi unaotafsiri maisha ya watu, Hili lilikuwa moja ya Sera ya Chadema iliyonadiwa na Mgombea Urais Mh Tundu Lissu.

Kipaumbele cha tatu ni Kupambana na Rushwa na Ufisadi, Hiki kimekuwa kipaumbele cha marais wote, Tatizo kubwa la Hayati Rais Magufuli alitangaza kupambana na rushwa kisha akaziba midumo ya umma, kinyume chake leo CAG anatuonyesha wizi na ufisadi ulivyotendeka katika utawala wa Magufuli, Dhana ya kupambana na rushwa na ufisadi huenda sambamba na uhuru wa vyombo vya habari na uhuru wa watu kusema.

Kipaumbele cha Nne ni Nidhamu na Uwajibikaji kwa Watumishi wa Umma na Kuboresha Maslahi ya Wafanyakazi, Kipaumbe hiki kiko kinyume na mtangulizi wake, Magufuli badala ya kujenga nidhamu yeye alijenga woga mahali pa kazi na majumbani mwa watumishi, Hakuna mtumishi aliyekuwa na uhakika wa kesho juu ya nafasi yake wala cheo chake. Utendaji kazi ukategemea zaidi katika matamko na madokezo ya Rais Magufuli. Mama leo ameongeza kwamba ataboresha maslahi ya wafanyakazi katika kipaumbele chake. Utawala uliopita haujuwahi kuongeza maslahi ya wafanyakazi isipokuwa Rais Magufuli alitangaza wazi kutoongeza mishahara badala yake akasema anajenga "Stigilazi Goji".

Kipaumbele cha Tano ni Kuboresha utoaji wa huduma za jamii kama afya, elimu maji nk, hili Utawala uliopita wa Hayati Magufuli ulilifanya kwa kiwango kizuri, licha ya CAG katika ripoti yake kueleza ubadhirifu mkubwa katika halmashauri kadhaa. Na Rais Mpya Mama Samia ameahidi kuwa sehemu ya kipaumbele chake cha Tano.

Kipaumbele cha Sita ni Kuimarisha misingi ya Utoaji HAKI, Uhuru na DEMOKRASIA nchini. Jambo hili kwa Hayati Rais Magufuli hakijawahi kuwa kipaumbele chake wala hata kulizungumza kwa bahati mbaya tu, Hili ni eneo kuu ambalo kwa namna moja Rais Magufuli alilivuruga taifa na watu wake na kusababisha manung'uniko katika nchi kwa kila tabaka nchini, kuanzia Wafanyakazi haki haikutendeka, Wafanyabiashara haki haikutendeka, Wanasiasa haki haikutendeka.

Kwaujumla katika taifa ukivuruga mfumo wa utoaji haki, umelivuruga taifa na watu wake. Magufuli alifikia hatua ya kuwaelekeza majaji cha kufanya ili awape pesa za kujiendesha, alifikia hatua ya kusema hakuna haja ya mfumo wa kimahakama kufanyika kwa mtu aliyekamatwa na kidhibiti, matokeo yake katika utawala wake japo hakuna yakwimu rasmi lakini ndio kipindi kesi zilikuwa nyingi mahakamani. Na kwa taarifa za kimahakama kwa jiji la Dar, Tangu Rais Mama Samia aingie Madarakani hadi leo zaidi ya siku 30, hakuna kesi ya Uchochezi iliyofunguliwa. Huu ni thibitisho kuwa Magufuli alivuruga eneo hili kwelikweli. Endeo hili Magufuli ALIPIGA MARUFUKU DEMOKRASIA nchini, akafunga shughuli halali za kisiasa, akaunda sheria haramu ambazo zilifanya shughuli ya siasa kuwa uhalufu hadi hivi sasa.

Ili Rais mpya Mama Samia atimize Kipaumbe hiki cha Sita, atalazimika kufuta sheria zote kharamu kama ile sheria ya mitandao kifungu cha 14, 15 na 16 hivyo vifungu leo vimejaza magerezani vijana wa nchi hii. Pia alazimika kufuta sheria ya vyombo vya habari kifungu cha 52 na 53 ambavyo vimekuwa vikitumiwa kukandamiza uhuru wa wanahabari, Pia sheria ya uchochezi ya kikoloni iliyomfunga Mwalimu Nyerere 1958 hadi leo ndio inatunyanyasa wanaharakati. Na sheria nyingi nyingi za ajabu ajabu zilizitungwa kwa lengo lilelile la kukandamiza watu.

Kisha Mama akawaambia makada na wananzengo kuwa Yeye na Mwendaka ni kitu kimoja, pia akasema Bunge linacheza ngoma na kudemka akiwaaza wabunge kufanya kazi za kibunge badala ya kushinda muda mwingi kulilia Legacy ya Magufuli, mara ya Samia. Lakini akaweka mkazo kwamba Mitandaoni kuna Uzandiki.

Nakubaliana nae kwamba yeye na Magufuli ni kitu kimoja, nikiwa na maana itikadi zao ni moja, hili hatuhitaji kujadili wale wote ni CCM, yaani ni zao la chama cha maoinduzi, Lakini Nakataa kata kata Rais Samia na Hayati Magufuli ni Mbingu na Ardhi, Rejea katika Vipaumbele hivyo uone utofauti wao. Rejea katika lugha na haiba ya kirais uone tofauti zao, Rejea busara na hekima zao uone tofauti zao. Kwaujumla kumlinganisha Samia na Magufuli ni kujipunja kimoyo na kiakili. Ibaki kusemwa taifa limejiponya.

Kuhusu Udandiki wa mitandaoni nakubaliana naye sana sana, ni kweli tupu, Mitandaoni kuna uzandiki mkubwa sana, na mimi ni mmoja ya wazandiki wa kubwa sana naweza kusema mimi ndio Mzazi wa Uzandiki huu kwa Tanzania hii, Yes ndilo sababu kuu ya ulimwengu kuleta mitandao ili wazandiki wa ulimwengu tupumue baada ya makofi na mapanga ya waserekare. Dunia ilikusudia hilo bahati mbaya Tanzania ilikuwa moja ya nchi za wajinga ikachelewa kupokea mageuzi haya ya kidunia. Nchi zilizoendelea wala haziumizwi na wazandiki isipokuwa serikali zao nazo zimepokea mageuzi na kuwa wazandiki wa kuu wa mitandaoni. Dawa ya moto ni moto.

Mtazamo wangu naweza sema, Rais Samia kusema yeye ni kitu kimoja na Magufuli ni lugha ya kisiasa tu, na kwa hili Samia siasa anaijua hasaaa na amecheza vizuri sana, amewachezea shere wanaCCM, Awali alitikisa kiberiti kwa kupima upepo pale alipoonza kufanya mambo tofauti na mtangulizi wake kama uhuru wa vyombo vya habari, sera ya uchumi na ukusanyaji kodi na kuonyesha umuhimu wa maridhiano katika taifa, akaona moto wa wapambe wa Magufuli yaani wahafidhina koko, lakini kubwa anatambua kuwa mwezi kesho kuna uchaguzi wa mwenyekiti wa chama (anakabidhiwa uenyekiti).

Kwahiyo kwa sasa hawezi kuonyesha misimamo yake thabiti, ashagundua wabunge wengi wako bungeni kwasababu ya Magufuli na wamekuwa royal kwa Magufuli hata kama kaondoka watu hawa akili zimeganda haziamimi kuwa hayupo. Ili kutoleta kura za maruhi keshokutwa, Mama ameamua kuwapaka mafuta kwa mgongo wa chupa waamini yeye ni jiwe kipeuo cha pili. Na walivyo wajinga wameshangilia.

Subiri mumuone sura halisi ya Mama baada ya kukabidhiwa uenyekiti kesho kutwa, Atasimama kama rais na ataamua kwa misingi yake na sio mashinikizo yenu kwamba avae viatu vya Magufuli mara vile mara hivi, ndiomana kwa maoni yangu nafikiri hawezi kupanguapangua serikali hovyo, hata ma RC na Madc anaweza kusubiri hadi akabidhiwe chama. Au anaweza kuwarejesha wote kwakuwahamisha vituo vya kazi tu, kisha miezi mitatu au sita hivi, tutauona moto hali.

Mama lazima atengeneze cream yake ya kiasa, hawezi kwenda na makokoro haya ya kikanda na kikabila. Kumbuka sasa nae anaifikiria 2025, kwa vyovyote vile anajua vita ya CCM kuwania madaraka hayo, na Mama anaijua CCM kuliko Hayati Magufuli aliyekuws haijui ccm na makandokando yake. Mama ni mwanasiasa wa nera.

Mama hawezi kuanzisha vita nyingine nje ya CCM (upinzani na wanaharati mitandaoni) huku ya CCM hajaimaliza au kujihakikishia ushindi, ikitokea hivyo anayemshauri katika siasa atakuwa anamwingiza shimoni.

 
Hivi vipaumbele ambavyo kila Rais anaeingia madarakani huja na vyake tofauti na wenzie ndio mwanzo wa hili taifa kudumaa kimaendeleo, kila siku tunaanza moja tu, kwanini pasiwepo na mpangilio atakaeondoka amuachie mwenzie muendelezo wa pale alipoishia?

Mfano, Rais wa sasa anataka kurekebisha hali za mifuko ya watanzania, haina kitu, napata shaka kama kwa huu muda wake mfupi anaweza kutimiza hilo lengo, kwani atatakiwa kuongeza mishahara watumishi wa umma na hapo hapo aajiri wengine wapya, tatizo la ajira kama tujuavyo ni mfupa uliomshinda fisi.

Tukumbuke vizuri, hili suala la Maisha bora kwa kila mtanzania lilianzia awamu ya Kikwete, akagonga miaka yake kumi likamshinda, vipi huyu wa sasa ataweza? kwa mazingira gani tuliyonayo sasa tofauti na ilivyokuwa wakati wa awamu ya Kikwete?

Lakini pia, kuna suala la utawala bora, Rais amesema atashughulikia hili, lakini juzi tu hapa tumeona Chadema wakinyimwa kibali cha kufanya mkutano wa siasa, sasa mtu utajiuliza, hivi vipaumbele kama sio mbwembwe tu za kitambulisha utawala mpya huwa vinatekelezeka kweli?

Binafsi nilipofikia sasa naona kuamini jambo linalosemwa litafanywa na serikali ya CCM ni kujidanganya tu, wameshazoea kutuliwaza kila mara kwa maneno mazuri mwisho wa siku wanatuacha kama walivyotukuta, au wakati mwingine ndio wanatuacha na hali mbaya zaidi ya ile tuliyokuwa nayo mwanzo.

Hawa watu ni kuwapiga chini tu hawana jipya tena, miaka zaidi ya 60 baada ya uhuru bado maadui wetu ni wale wale, ujinga, umaskini, na maradhi licha ya rasilimali zote tulizojaliwa na Mungu, zaidi wanachoweza ni kutubadilishia sura za marais tu kila baada ya miaka kadhaa, na uongo mpya wa vipaumbele vyao ambavyo vingi huwa havitekelezeki.
 
Kwa hiyo na wewe yericko umekua mataga sasa?
Au unataka hiyo buku saba?
Tupeane mchongo.
Au uko sokoni? Sema bei yako
 
Back
Top Bottom